Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Jamaa wa Vibe huyu hapa
Wote mmesahau kipindi cha jamaa mmoja sijui dj yule bonge sana kinaitwa vibe

hqdefault.jpg

Huyu hapa jamaa wa Vibe... Alikuwa anaitwa sinbad
 
Nakumbuka ITV kulikuwa na tangazo ka CHAI BORA kilele cha ubora, pia kulikuwa na tangazo la bia ya ndovu ,simba alikuwa anatanu mdomo huku ana unguruma akisema "kunywa NDOVU kilele cha ubora"
 
Hi
Kuna kipindi itv walikua wanaonesha series ya kisayansi (sci fi) inaitwa EARTH FINAL CONFLICT ya aliens wanaoitwa taelons aka companions walikuja duniani wakiwa na teknolojia ya hali ya juu katika nishati, usafiri na utibabu. Walitoa bure huduma hizo kwa nia safi, ila kukawa na upinzani wa dhidi yao ukihoji hasa nia ya hao taelons kwa dunia.

Ilikua series nzuri, ya kufikirisha bahati mbaya itv waliikatisha kabla ya kufikia mwisho....

Wasioikumbuka nii hii hapo


hii naikumbuka kuna alien mmoja ana para hivi...
 
Mambo ya enzi zetu hayoo tukiwa vijana wadogo, kweli tunazeeka
"Hata babu alikuwa kijana na Bibi alikuwa binti"
 
Channel 10 kulikuwa na movie ya Mr T na Knight Rider (maarufu kama maiko, maiko - jamaa ana gari lake hilo lina fujo balaa) pia kulikuwana igizo la kutisha lilikuwa linaitwa Mmsai na Ng'ombe Wake

ITV kwanza picha linaanza matangazo yanafunguliwa saa 12 jioni hadi saa 6 usiku, walikuwa na vichekesho vya Perfect Strangers, Hang in with Mr. Cooper pia kulikuwana movie ya TimeTrax, Beast Master, Pointman na kipindi cha Jackpot Bingoooo!!!

Dah kulikuwaga raha sana.
Kaka Channel 10 ni ya juzi tu..labda una maanisha DTV
 
Nani anakumbuka matamasha ya CORA africa toka bondeni aisee yalikua yananoga.

Nakumbuka kwa Mara ya kwanza Tanzania tuliwakilishwa na msanii flani wa kike matata na kibao chake cha "ngoma inogilee ngoma imekolea ngoma ya pwani tatata mdundikooo"

Nimemsahau ila alikuaga US na alishaokoka na kuacha secular.
Anaitwa Enica
 
Back
Top Bottom