Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Hiyo katuni ya spinach nadhani si nyingine ila POPEYE..........na katoto kake juniour.......basi na mimi walinichotaga akili bi mkubwa akipika mchicha nachukua kikopo naweka mcicha halafu naubwia kama popeye eti niwe na nguvu....loh[emoji23]

Halafu hiyo uliyoandika KIMBA nadhani ni SIMBA the white lion.
Ni Kimba the white lion
 
The Bold and the Beautiful ,bi mkubwa alikua akimpenda Richie na Stefan

Taxas Reangers ,The Crow
Halafu hivi unajua movie ya the crow ilikuwa ichezwe na mtoto wa bruce lee (brandon lee) ambaye alifariki on the set yaani akiwa katika kurekodi vipande vya hiyo filamu ya the crow. So haikutoka maana jamaa alidedi kabla haijakamilika.
 
Katika matangazo nilokuwa nayapenda moja wapo la revola.
'Tueleze siri ya mafanikio,
Sio siri, ni revola,
Revola pekeyake?
Ndio, kwani marashi yake ni tulivu na huniweka fresh mchana kutwaa.
Yalikuwa kama matatu tofauti, ila me nilikuwa nalipenda la yule mdada alokuwa anafanya mazoezi, ile lafudhi yake ilikuwa tamu na mbwembww zake.
Jengine la maji ya kilimanjaro.
'Maji safi kilimanjaroooo'
Tangazo la colgate la watoto, na tangazo la fanta la watoto pia.
Tamthilia nilokuwa naipenda ni Acapulco bay.
Anaitwa Mariam Hassan Nusu Mbongo Nusu Msomali... Alikua anasisimua sana yule dada
 
Mkuu enzi zile kibonde c alikuwa CTN na alikuwa akitangaza kipindi cha habari michezo
Kabisa kibonde ndio alikuwa anatoka halafu alikuwaga hana matani miaka ile mi sikujua jamaa ni mchekeshaji balaa hadi alipotua clouds
 
Je unalikumbuka tangazo la seven up la fidodido lilikuwa poa pia
Aisee hivi jamaa kwanini hawamtumii fido dido now days maana yule katuni alikuwa amenishika sana na watoto wengi alikuwa amewashika....... ingawa mimi nilikuwa naenjoy kunywa soda ya fahari kama mtaikumbuka ilikuwa kama pinaple ila yenyewe ni taamu sana kama juice kemikali zilikuwa hakuna kabisa.
 
Wow mi pia revola ndio maana hata id yangu nimeiweka hovyo coz hadi Leo natamani IPP media warudie aisee yule Dada alikuwa na sauti nyororo sn
Halafu alikuwa mkenya kama sikosei.........alikuwa anatamka maneno kama " MMMMMMHMN KILA SIKU" halafu kamlio ka levola kanalia tangazo linaisha.
 
Hahaha sisi home tulikuwa na Tv aina ya National nchi 21 mzee ilikuwa akifika tu saa nne anaanza hayahaya kama mwanafunzi kulala sasa afu ndio inaanza daaah tulikuwa tunaibeba tunaenda nayo chum bani kimyakimya
Washua miaka ile walikuwa wadwanzi.....yaani mtoto wangu simpi hiyo taabu nampa uhuru wake ila tu asiutumie vibaya kuangalia mambo ya ajabuau kufeli darasani........nilikuwa napatashida sana kipindi naanglia kitu ninachokipenda halafu mzee anasema haya kulala kesho shule.........bi mkubwa tu ndio alikuwa anatuelewa anatuachia tunalizie kamani movie au tamthiria.
 
Vipindi hivyo vingine ni vya uchochezi kwa vijana wetu...hatuvitaki virudi.tuwekewe vipindi vya kilimo vya kufuga...vya PowerTilla zinavyolima na hotuba za rais.
wewe namashaka kama hata mwaka 2000 kama ulikuwa umeshazaliwa unashangaa tu tunaongea vitu ambavyo haukuviona......hebu toka hapa usituharibie mahaba ya muda tuliouishi kipindi hicho utoto wetu ulikuwa wa kipekee sana wakati ule.
 
Tangazo la Revola da sijui kwanini walilitoa bora hata wangeliacha you tube alikua miriam odemba yule nazani
Ha ha ha ha ha wewe miriam odemba wa wapi ha ha ha ha ha ha kipindi kile hata sidhani kama alikuwa kaanza mambo ya ulimbwende..........yule alikuwa ni mrembo tokea kenya na nasikia alifariki yule dada
 
suzan mongi nadhani alikuwa mtangazaji wa dtv
Suzane Mongi.....Faudhia Tabood.......john ngayomah......othman njaidi......ahmed kipozi.....Tumain meshain na mdada mrembo mannuel Elias ndio walikuwa watangazaji wa kwanza wa I.T.V .

Suzane Mongi hakuwahi kuwa D.T.V.
 
Mwenye email au simu ya itv nataka niwashauri wamepoteza mashabiki sana zamani walikuwa super kweli sikuhizi ikiisha tu habari basi zamani walikuwa na vipindi vizuri mno wao ndo walileta tamthilia za kikorea zilipata mashabiki sana hata katuni za watoto enzi hizo kina ed edd eddy dexter powerpuf girls ben ten etc
Hizo katuni umetaja zilikuwa zikionyeshwa cartoonnetwork ya CTN tu na C2C (miaka ya 1999) but si I.T.V
 
Sabuni kodrai DTV
Mamaaaaaaaaaa[emoji31] .......daaaaaaah jamani tutauwana unajua hivi vitu vitamu tunavyokumbushiana[emoji16] .......yaani nakumbuka kuna tangazo la sabuni ya kodrai la kipindi kama sio kuanzia 1992 hadi 1995 hivi lilikuwa linasauti ya mwana mama anaimba. Dah nikilisikia naweza kulia.
 
Anaitwa misanya Bingi saizi yuko university of dar es salaam ni Dr pale anawapiga vijana wetu shule
wewe ha ha ha ha ha ha ha[emoji23]

Mwenzako anamaanisha kipindi cha kutoka marekani na mtangazaji ni m'marekani anaitwa sinbad jamaa tolu hivi halafu kama halfcast.
 
Back
Top Bottom