Tukumbushane wahenga vitu tulivyonunua enzi hizo na bei zake

Me nakumbuka tu nauli ya daladala enzi niko dent ilikua sh 50
Ah...sh 50 juzi tu hp wewe uzao wangu hii mada ya wakongwe tukae pembebi ushasikia feni 600 hamsini tumeoanda daladala toka shule wao walikodia teksi kariakoo hadi temeke khatari!
 
Nimesafiiri MORO - DSM kwa mabasi ya MORETCO nauli ilikuwa 1½ Tshs! Pia kulikuwa na Basi binafsi linaitwa MZALENDO! Nauli ilikuwa TShs 2
 
Nilinunua Nyumba Morogoro Mjini ktk ile project ya Mwl ya Urbanization kwa bei ya TSHS 240! Mtaa wa Konga. Mwaka 1974
Sasa hivi ata sembe robo upati tuko kimwendo kasi zaidi
 
Nakumbuka fan langu la kwanza nilinunua sh. 600 Kariakoo na nikiwa na rafiki yangu tukakodi tax kutoka Kariakoo mpaka Temeke sh. 50 enzi hizo Uda sent 20 hebu kumbuka na wewe vijana mtuache kidogo.
nakumbuka gari ya jeshi 109 land rover fixed for radio ilikuwa Tsh.58000 na kuna maandishi yaliyo andikwa mbele ya dereva kumsisitiza Aitunze!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…