Tukumbushane wahenga vitu tulivyonunua enzi hizo na bei zake

Nakumbuka fan langu la kwanza nilinunua sh. 600 Kariakoo na nikiwa na rafiki yangu tukakodi tax kutoka Kariakoo mpaka Temeke sh. 50 enzi hizo Uda sent 20 hebu kumbuka na wewe vijana mtuache kidogo.
Duuuuhhhh wewe kweli muhenga
 
Nakumbuka chupi za VIP ikikatikΓ  inapanda juu kiunoni...ni wahenga tu ndo wanajua ikikatika nini na kwa nini ipande juu kiunoni[emoji1595]
 
Tulitoka shimoni kivipi??
Kwani hujui kila zama na ujinga wake??
 
Lah we Mhenga
Huku ambako sasa kuna parking za magari kwenye uwanja mpya ndiko foleni ilikuwa ya hatari, ukikata tiketi yako kuingia kuna mageti 3.

Moja huku linatazama indoor stadium kuingia mzunguuko ambako mnakaa mashabiki wote mnachanganyika Simba/Yanga .

Hakuna kusumbuana, mambo ya utofauti ni jukwaa kuu na jukwaa la kijani ambalo nalo kwa kiasi kikubwa likikuwa linatawaliwa na Yanga.
 
Nilianza darasa la kwanza shule ya msingi serikali ada shilingi 200
Kabla ya hapo ilikuwa sh.20/=. Sijakosea namaanishi ishirini tu.
Nauli ya mzunguko dar ilikuwa dala yaani sh.5 na ndiyo kisa cha jina daladala.
 
Nimepanda nauli shs 5 wakati huo mtu mzima shs 30. Moshi mjini hadi Kiborloni kulikua na mabasi yanaitwa Mapigo 6, Maranzana na Asante Babu tale πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Shikamoo muhenga πŸ˜€πŸ™ŒπŸ™Œ
 
Ng’ombe wa kwanza nilipewa hela na mzee nilinunua kwa shilingi Mia na alikuwa mkubwa sana
Naomba shikamoo za kumwaga
 
Nilinunua biskuti ya marie mwaka 1976 nikiwa kwenye bus natoka arusha nahamia kikazi peramiho dah siku zinakimbia

duh, UMENIKUMBUSHA BIBI YANGU LAZIMA ALIKUWA AJE NA BISKUTI ZA MARIE,

Enz hizo tunaingia kutazama filamu kwa sth.20.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…