Tukumbushane wahenga vitu tulivyonunua enzi hizo na bei zake

Tukumbushane wahenga vitu tulivyonunua enzi hizo na bei zake

Tusisahau tulipo shindana kuvaa Pekosi, laizoni, kaptula na stoking, kuchana na kuweka way...
Wenzetu siku hizi wananyoa kama kichwa cha jogoo, na kuvaa kata K! kweli kila zama na ujinga wake 😀😀😀
 
Nakumbuka fan langu la kwanza nilinunua sh. 600 Kariakoo na nikiwa na rafiki yangu tukakodi tax kutoka Kariakoo mpaka Temeke sh. 50 enzi hizo Uda sent 20 hebu kumbuka na wewe vijana mtuache kidogo.
Hii ni chai.
 
Wakati tunasoma sekondari miaka ya 60 - 70 tulikuwa tunasafiri kwa warrant za serikali; na tukifika shuleni tunarudishiwa pesa zote tulizotumia safarini. Tulikuwa tunafuta nauli kwenye tiketi na risti zingine za gari na mapochopocho ya njiani na kuweka namba kubwa ili turudishiwe pesa zaidi. Ufisadi na upigaji vilianzia hapa [emoji16][emoji16][emoji16]
Sekondari miaka ya 60-70.
Ninakataaa
 
Chips yai sh 5 enzi hizo ndio Chips za mitaani zinaanza,Kwenye mabaa ilikuwa ni mwendo wa Ndizi choma na kuku au nyama choma, Kwa mpemba pale karibu na Hongera baa Chuo cha Ustawi lazima ukutane na foleni ya watu wanasubili Oda yao na enzi hizo Chips ilikuwa km appetizer tu ,unagonga chips yai hlf ukirudi Home Menu kama kawa.
 
  • Thanks
Reactions: amu
Kweli hiyo razoni na pekos buga
Tusisahau tulipo shindana kuvaa Pekosi, laizoni, kaptula na stoking, kuchana na kuweka way...
Wenzetu siku hizi wananyoa kama kichwa cha jogoo, na kuvaa kata K! kweli kila zama na ujinga wake [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom