Tukumbushane: Wimbo bora wenye jina la kike...

Tukumbushane: Wimbo bora wenye jina la kike...

Mwimbaji alikuwa Komandoo Hamza Kalala. Sina uhakika na bendi aliyokuwa wakati anaimba wimbo huu. Itakuwa kati ya Uda Jazz Band au kikundi chake cha Bantu Group.
Nakumbuka hiki kibwagizo, natumai wadau wengine watakuja na mashairi ya wimbo huu.

Aliimba akiwa na Washirika Tanzania Stars 'Watunjatanjata" baadaye Wimbo huu ulirudiwa na mwanawe Komandoo aitwaye Kalala Junior
 
Nimekuwa nikitafuta wimbo zilipendwa unaitwa 'Roza' ama 'Mpenzi Roza' ulioimbwa na Tanga International. Cha ajabu nikiulizia huwa nakuta watu hawaufahamu. Niliwahi tembelea banda la TBC pale Mnazi Mmoja nikaiulizia hawakuufahamu. Wakati nausikiliza nadhani nilikuwa kwenye teens yaani late 70s ama early 80s. Nani anaweza kunisaidia nipate wimbo huu kwani wakati ule unapigwa niliupenda sana?
Nafikiri utakuwa ni huu.
"Mapenzi yetu yalikua ni hasara Roza, Mganga aliekupa dawa ni hadui yangu, dawa ahaliokupa ni sumu mwezangu ..............,
hivi ndivyo hulivyotaka kunitoa roho yangu.........."
 
Aliimba akiwa na Washirika Tanzania Stars 'Watunjatanjata" baadaye Wimbo huu ulirudiwa na mwanawe Komandoo aitwaye Kalala Junior
Nilikua na nakusubiri uweke maneno ya huo wimbo wa rainbow mbona kimya mtu wangu,yaani nina kiu ya ajabu ya hilo songi
 
Mwanakijiji naomba offpoint kiduchu balatanda na babadesi Sikonge naombe mistari song moja .nilikumbwa na mikasa nikawa napenda kuliimba ila sijui heading wala mtunzi

"nimekusamehe lakini sitokusau visa ulivyonitendea mama ee eeh ulinikana wakati nilpokuwa na shida ukasahau yote nilokutenda wakati unaelewa hakuna komandoo wa shida "

Here we go;

Nimekusamehe lakini sitokusahau visa ulivyonitendea Kalala ee eeh,visa ulivyonitendea Kalala ee eeh

Ulinikana ee wakati mi na shida,ukasahau yote tuliyofanya nawe,wakati unaelewa hakuna Komando wa shida,wakati unaelewa hakuna Bingwa wa shida,leo nakukumbusha shida huja na kupita,yaliyopita si ndwele tugange yajayo kakaa mimi nakusamehe lakini sitokusahau,lalalala lalalala laaaa,lalalala lalalala mimi nimekusamehee,lalalala lalalala laaaa,lalalala lalalala mimi nimekusamehee

(Eddy Sheggy)Nimekusamehe lakini sitokusahau

Nimekusamehe lakini sitokusahau visa ulivyonitendea Kalala ee eeh,visa ulivyonitendea Kalala ee eeh

Ulinikana ee wakati mi na shida,ukasahau yote tuliyofanya nawe,wakati unaelewa hakuna Komando wa shida,wakati unaelewa hakuna Bingwa wa shida,leo nakukumbusha shida huja na kupita,yaliyopita si ndwele tugange yajayo kakaa mini nakusamehe lakini sitokusahau,lalalala lalalala laaaa,lalalala lalalala mimi nimekusamehee,lalalala lalalala laaaa,lalalala lalalala mimi nimekusamehee

Rafiki wa kweli ni yule asiyekutupa ee kwenye dhiki na faraja mko wote mko wote,kwenye dhiki na faraja oooh oooh,uliniacha nateseka peke yangu peke yangu,pasipo msaada wowote kaka oo oooh,pasipo msaada wowote kaka oo oooh,lakini mola muweza wa yote(wa yote) kaninusuru na matatizo yamepita o kaka,kweli nimekusamehe lakini sitokusahau,yaliyopita si ndwele tugange yajayo kaka,kweli nimekusamehe lakini sitokusahau,yaliyopita si ndwele tugange yajayo kaka,lalalala lalalala laa,lalalala lalalala mimi nimekusamehe,alalala lalalala laa,lalalala lalalala mimi nimekusamehe
 
Nilikua na nakusubiri uweke maneno ya huo wimbo wa rainbow mbona kimya mtu wangu,yaani nina kiu ya ajabu ya hilo songi

Kiongozi,kwa kweli siukumbuki kabisa huu wimbo ninaoukumbuka ni ule wa Milima ya kwetu(walisema dalili ya mvua ni mawingu nilyempenda kanitoroka mama) ambao Eddy Sheggy aliuimba akiwa na Orch. Super Rainbow
 
Mkulu,
Heshima Mbele!

Umenikumbusha 92' Hotel na akina Eddy Sheggy RIP.
Watu njat njata (Ushirika Tanzania Stars)
Mwanangu wewe mkali pia

Nakumbuka sigara zangu za mwanzo mwanzo!

Ha ha ha ha .......!!!!

Sasa enzi hizo hotel 92 wanapiga Njata na pale legho ikaanzishwa bendi ya kuitwa Legho star chini ya Asosa.
Hawa jamaa waliwahi kutamba na nyimbo kama Francisca na Leila...
Lakini leo ntawadokeza kuhusu francisca...

''jamani makubwa yamenipata eeh eeeh
Sijui nifanye nini francisca anielewe mamaa...Hata kama ni hasira jamani hizi zimezidi...

Mkimuona huko aliko mwambieni kweli natesekaa eeeh mamaa

Jamani francisca kumbuka utu wangu eeh
 
Ewe ngulupaamba lee,ewe ngulupamba Francisca,ewe ngulupaambaa lee ewe ngulupamba Francisca,ukimuona huko aliko muelzeni kweli natesekaa,nafasi yake bado iko rohoni mwangu oo ngulupamba Francisca kumbuka utu wangu mamaa

Mkimuona huko aliko muelezeni kweli nateseka,hata kama ni hasira jamani zimezidi...Jamani Francisca kumbuka utu wangu mama

Sopabangoo sopabangoo,sopabangoo

Mkubwa,umenikumbusha mbali sana hapo yaani maana enzi hizo Legho Stars chini ya 'Mutoto Muzuri' Tshimanga Kalala Assossa akisaidiwa kwa karibu na mtaalamu wa Kinanda Anania Ngoliga ilikuwa inatisha babaake...Muziki ulikuwa kipindi kile bwana....Hmaana Ukienda Vijana Socia Club unawakuta Pambamoto,ukija Shekilango 92 Hotel unawakuta Watunjatanjata,ukienda pale Legho unawakuta wana Sopabango Legho Stars,ukija Lang'gata unawakuta Marquis...Ukienda Amana Msondo...DDC Kariakoo ama Magomeni Kondoa unalikuta Nginde baba,Safari Resort Kimara unawakuta OSS,New Afrika unawakuta watoto wa ngoma za maghorofani MK Group...Kipindi hicho hakuna Twanga,Ngwasuma wala Pekecha pekecha,ilikuwa ni Pambamoto,Watunjatanjata,Sendema,Magnet Tingisha,Ngulupa Tupatupa Dansi,Sikinde ngoma ya ukae,Msondo magoma kitakita,Sopabango,Ndekule(baadaye Power Iranda na Rashikanda wasaa),Kiny kinye kisonzo tisa kumi mangara,paselepa,Mkote ngoma,Tukunyema n.k...Ilikuwa raha sana aisee
 
Mkulu,
Heshima Mbele!

Umenikumbusha 92' Hotel na akina Eddy Sheggy RIP.
Watu njat njata (Ushirika Tanzania Stars)
Mwanangu wewe mkali pia

Nakumbuka sigara zangu za mwanzo mwanzo!

Ha ha ha ha .......!!!!

Hapa kulikuwa na vichwa babaake...Komandoo Hamza Kalala,Eddy Sheggy(R.I.P),Adama Bakari 'Sauti ya Zege'(R.I.P),Mhina Panduka 'Toto Tundu',Emma Mkelo 'Lady Champion',Madaraka Morris,Robert Mabrish,mtaalam wa kinanda Abdul Salvador 'Father Kidevu' na wengine

Hawa jamaa walikuwa wakali bana..Sema ndo hivyo tena ilikufa na baadhi ya wanamuziki kwenda Bantu Group na Komandoo Hamza Kalala na wengine wakaenda kuanzisha bendi ya MCA International wana 'Munisandesa'
 
Salama by Jabali la Muziki

Wapi salama, salama nakuomba
salama nakwita mamaa
umenipa machozi, machozi yasiyokwisha
nifanyeje mwana mamaa

nikilala naota sura yakoo
nikitembea nasikia waniitaa
nageuka sikuoni mwana mamaa
nauliza uko wapi mwana mamaa
This was late seventies/earlier eighties when I was a little kid!Nyimbo hizi ziko so emotional. They bring back those glorious, sweet memories of the past. They also remind me once again, that I should not take things for granted...if there is a possibility of doing anything to the best of my ability I should do so because after many years later, when they same issues come to the surface, I would cry either for joy or regrets of the way I handled matters at that particular time.
Hii ndio JF maana kila kukicha kuna kipya cha kujifunza nje ya topic iliyozoeleka, ufisadi! Lol
 
-Ashura-Magereza Jazz(wana Mkote ngoma)
-Edina-Magereza Jazz(wana Mkote ngoma)
-Ngalula-Marquiz
-Stella-Bantu Group Band
-Afro-Les Wanyika
 
Kiongozi,kwa kweli siukumbuki kabisa huu wimbo ninaoukumbuka ni ule wa Milima ya kwetu(walisema dalili ya mvua ni mawingu nilyempenda kanitoroka mama) ambao Eddy Sheggy aliuimba akiwa na Orch. Super Rainbow

Mkulu wimbo ndio huo huo embu lete vituz kidogo.huko nilikukua kazi hazikufanyika akili yote ilikua kurudi hapa.

MILIMA YA KWETU-Super rainbaw

katika baadhi ya maneno Sheggy ndio anasema "umekua kama helkopta ndege isio chagua mahari kwa kutua........."

So many memories..........!
 
Hapa kulikuwa na vichwa babaake...Komandoo Hamza Kalala,Eddy Sheggy(R.I.P),Adama Bakari 'Sauti ya Zege'(R.I.P),Mhina Panduka 'Toto Tundu',Emma Mkelo 'Lady Champion',Madaraka Morris,Robert Mabrish,mtaalam wa kinanda Abdul Salvador 'Father Kidevu' na wengine

Hawa jamaa walikuwa wakali bana..Sema ndo hivyo tena ilikufa na baadhi ya wanamuziki kwenda Bantu Group na Komandoo Hamza Kalala na wengine wakaenda kuanzisha bendi ya MCA International wana 'Munisandesa'

ha ha ha ha,
mie nilikuambia wewe mkali.......
hao jamaa ndio walikua vichwa vya muziki wa dansi,ukiondoa wakina bichuka,tx,Gurumo,na wengine .
Salvador sijui alikwenda wapi yule bwana ha ha ha!
 
....Mwingine ni Ngalula wa Remmy Ongala...Kumradhi kama ulishatajwa hapa....
 
Sasa enzi hizo hotel 92 wanapiga Njata na pale legho ikaanzishwa bendi ya kuitwa Legho star chini ya Asosa.
Hawa jamaa waliwahi kutamba na nyimbo kama Francisca na Leila...
Lakini leo ntawadokeza kuhusu francisca...

''jamani makubwa yamenipata eeh eeeh
Sijui nifanye nini francisca anielewe mamaa...Hata kama ni hasira jamani hizi zimezidi...

Mkimuona huko aliko mwambieni kweli natesekaa eeeh mamaa

Jamani francisca kumbuka utu wangu eeh

Sikuwahi kuwa na hamu ya kuwaona watu wa hapa JF ukiondoa mwana KJJ,ABTBCT,BRUREY yaani wewe na BALANTANDA mmeingia kwenye list
 
Back
Top Bottom