Tukumbushane: Wimbo bora wenye jina la kike...

Tukumbushane: Wimbo bora wenye jina la kike...

Enzi za Vijana Jazz walikuwepo akina Jerry Nashon 'Dudumizi'. Beno Anthony Villa na wengine, waliporomosha kibao kimoja kinaitwa 'Theresa'. Nilikipenda sana. Walikuwa wanasema demu alimkataa jamaa siku ya harusi, Nimesahau mashairi yake.
 
Wimbo ulikuwa mzuri sana huu aisee,utunzi wake Jery Nashon 'Dudumizi' (R.I.P)

Najiuliza kila mara na kujuta moyoni
ni penzi gani analokupa huyoo
Ni dawa gani aliyokunywesha
Ukachanganyikiwa na kuisahau sura yangu siku ya harusi

Bibii,hoteli gani hujalala maama,kinywaji gani hujakunywa mama,chakula gani hujakula maama,basi sema raha ipi unataka ili nielewe niiponye Roho yangu,Theresa

Theresa, penzi gani analokupa huyo kijana
sema nitakupatia mpezi theresa
kama gari na mi ninalo mpenzi theresa,sema nitakuachia mpenzi Theresa
Akikupa wali kwa kondoo mpenzi Theresa,nitakupa wali kwa kuku mpenzi Thersa
Akikupa busu la shavu mpenzi Theresa,nitakupa la kinywani mpenzi Theresa...Mamiii

Najiuliza kila mara na kujuta moyoni
ni penzi gani analokupa huyoo
Ni dawa gani aliyokunywesha
Ukachanganyikiwa na kuisahau sura yangu siku ya harusi
 
Enzi za Vijana Jazz walikuwepo akina Jerry Nashon 'Dudumizi'. Beno Anthony Villa na wengine, waliporomosha kibao kimoja kinaitwa 'Theresa'. Nilikipenda sana. Walikuwa wanasema demu alimkataa jamaa siku ya harusi, Nimesahau mashairi yake.

Hii albamu yenye nyimbo ya Theresa ilikuwa na nyimbo tamu kama V.I.P,Shoga na Mama Chichi
 
Jamani kuna wimbo nimelala naukumbuka nikasema leo nijiniwaulize kama kuna mtu anao maneno yake yote hapa aweke
Ni wa bendi ya RAINBAW kama sikosei Marehemu Eddy sheggy aliimba pia baadhi ya maneno yake...........

...........Umekua kama Helkopta...ndege isiyochagua mahari pa kutua eee...........!!!!

sasa i cant connect the following words tafadhali wakulu puliziiiiiiiiiiiiiiiii..................

..Haya Mzee. marehemu Eddy Sheggy, marehemu Emma Mkello na Kundi zima la Super Rainbow: Ni wimbo mrefu kidogo.

Milima ya Kwetu 1

Nikitazama milima ya kwetu ee,
machozi yanitoka kwa uchungu na mawazo,
tulitoka wawili ninarudi peke yangu,
baba na mama wataniuliza bibi yako yuko wapi ee,
Ndugu jamaa wataniuliza bibi yako yuko wapi eee,

japokuwa ninakaribia kufika nyumbani ee,
Ninatamani gari isifikie upeesi,
kwa ile aibu nitakayopata mbele ya wazazi ii,
kwa vile ni miezi michache imepita nilitoka na bibi yangu,

(Eddy)
Nitasema nini kwa baba mimi najuta aa,
kwa pesa zake nyiingi alizopotezaa,
harusi ilifanyika kwa gharama kubwa sana,
watu walikula na kunywa na kusaza mamaa,

Nikaenda kuishi na bibi yule mjini,
kazi yake ilikuwa ni vituko,
nikaenda kuishi na bibi yule mjini kazi yake ilikuwa ni vitiimbwi,

Alianza kuweka sukari kwenye mboga,
nikaonja haviliki tukalala na njaa,

kafuatia na kuweka chumvi kwenye chai,
nilikuwa na wageni wakatoka bila kuaga,

kafuatia kuchelewa akienda sokoni,
nikimuuliza anitukana hadharani aibu,

kuna gari imekuja hadi mlangoni,
kujitetea akasema mjomba wake kaja,

hivi juzi kavunja kioo cha dirisha,
apate kuchungulia wapitao njiani,

hatimaye kunibeza na kunidharau,
shikamoo ikaisha ikabaki
Vipi babu, mambo zakoo ee x2

Nilishindwa kumuuliza ee sikutaka kumuudhi,
sababu nilikuwa nampenda nampenda saana x 2

chorus:

walisemaa dalili ya mvua ni mawingu,
niliyempenda kanitoroka mama,

(Eddy Sheggy)
Nilinyang'anywa tonge mdomoni,
nilinyang'anywa tonge kinywani,
niliyempenda kanikimbia mama yoyo,
niliempenda kanikimbia masikini nifanye nini mama,

(chorus)

Vituko ee, vituko vya bibi huyoo,
sitaweza kusahau mimi oo mama ee,
sitaweza kusahau mimi oo sheggy ee,
alikuwa kama helikopta, ndege isiyochagua mahali pa kutua ee,
kila mtaa hapa mjini jamani tazameni oo,
ana bwana mmoja ama wawili mama mama oo,
nifanye nini mama oo,

(chorus)
 
Mwanakijiji, nilikuwa sijasoma hii thread lakini kichwani nikiwa kwenye shughuli zangu nuilikuwa nazipanga nyimbo
bora zenye majina ya kike na mtiririko wangu ulikwenda kibendi-bendi. Best kwangu ni:-

DDC Mlimani Park
1. Neema
-utunzi wa Chidumule; huu ni best kwa maoni yangu hadi leo.
2. Hiba- H. R. Bitchuka alikomesha " ili tuishi vizuri na kujenga fammilia boraa, yenye thamani na penziii! Hadi leo bado nasikia mrindimo wake
3. Conjesta; Nimetembea pando zote za dunia, mashariki na magharibi jaman-iBenno Villa

JUWATA/ MSONDO
1. Fatumaa Nasafiri mama
! Ubaki salama......- Shaaban Dede aliimba sana!
2. Jane- nilpokutana na Jane, nilimshauri, akubaliane na mawazo ya wazazi wakee! Ni wao walikulea, wakakupeleka shule, ukapata mafunzo ya kila namna! (Shaaban Dede akichombeza)
3. Solemba- Nic0 Zengekala alikomesha!
4. Tuma- nimesimama kwenye kona, ya Uhuru na Msimbazi... TX
5. Pamela, sikijui cha kukulipa Pamela..-Fresh Jumbe
6. Sakina tulia dada nikuelezee, nimepata barua kutoka nyumbani, inayoeleza umepata mchumba...- Huu Baba Desi pekee ndo tunaweza kuwa pamoja
7. Faulata

MWENGE JAZZ/ PASELEPA
1. Rehema
- huu ni wa 1980

JKT MAFINGA/ KIMULIMULI
1. Sakina
- Zahir Zoro anasema anaapa kwa jina la Mungu aliyesimamisha mbingu bila ya nguzo!
2. Zinduna (photo album) Zoro anataja mitaa ya Mwanza kwa umaikini mkubwa

Dar International/ SUper Bomboka
1. Vicky
- Marijani si mchezo!
2. Zuwena- Selander Bridge by Marijani
3.Mwanameka- Jabali la Muziki (huu wimbo tulifanyia mtihani wa Form 4, (1991) nikaondoka na 'D'! Sikutegemea kabisa
4. Mama Maria- hao ndio wenye kukaanga mbuyu, kuwaacha wenye meno watafune!

Super Matimila/ Talakaka
1. Mariamu wangu!-
Dk. Remmy analalamika "mwenzenu sina pumuzi kujizuia siwezii! Mariamu wang, Tanga mbali!

TANCUT Almasi-Iringa
1. Pili-
Kasaloo na Kyanga Songa

Les Cuban- Morogoro
1. Mtoto Jackie
, mpenzi wangu, najaribu kukusahahu lakini nashindwa, hasa ni ile ndoto inayonisumbua, naota waniletea kifunko cha zanmbarau- Nico Zengekala alipagawisha!

WASHIRIKA STARS- WATU NJATANJATATA
1. Julie eeh
, ehee nikupe nini ...- Utunzi wa Madaraka Morris. Huo wimbo ukipigwa hata leo utadhani ni wa jana. Alikuwepo Abdul Salvadol, Eddy Shegy, Adam Bakari (Sauti ya Zege) na Hamza Kalala
2. Stella, Ming'ombe, jamala madundo! Nalila masumbanga huku-huka-H. Kalala

VIJANA JAZZ- Awamu ya Pili/ Pamba moto!
1. Stella
- By Hamza Kalala kibwagizo: hata jirani zangu dirishani niliwasikia, wakikusiu kwa ukarumu, Stellaa ee, ee eeh , Mwadila
2. Maria ee, sikiliza muziki wa awamu ya pili Maria, unavyolalamika juu yako- Hemedi Maneti

BIMA LEE
1. Celina;
si kosa langu ee Celina ni lako mwenyewe, unayofanya Celina, nui aibu yako mwenyewe. Endelea na mambo ya mjini, na matokeo yake utayaona Celiona mama....

Orchestra Safari Sound/ Ndekule
1. Christina Moshi
- Skassy Kasambula

MAQUIZ Du Zaire
1. Mainda-
Mafumu Bilali Bombenga
2. Ni wangu, Angelu ni wangu mama
3.

JAmani, sina hakika kama enzi za Miziki ya akili kama hii itarudi tena maana bendi nyingi zimekufa zimebaki Mondo na Mliamani Park zinachechemea, zikifa na hizo mbili ndo basi tena, Muziki wetu wa TZ utakuwa kwisha habari!
 
  • Thanks
Reactions: Iza
Nkwingwa, kuna jamaa mmoja anaitwa Nkoi Wa Bangoi. Sijui alikuwa akipigia bendi gani (nadhani Makassy)...unajua alipo sasa hivi?

Huyu ni Nkurlu Wabangoi. kama sikosei alianza na Marquiz Du Zaire ile ya kamanyola bila jasho na nafikiri pia alipita Orchetre Safari Sound ile ya dukuduku. kwamba sasa yuko wapi, sina hakika sana ingawa kumbukumbu zangu zinaniambia kitu ambacho kwa vile sina uhakika nacho naomba nisikiseme wazi mpaka mwenye uhakika aje atueleze.
 
Paulina, sijui umeimbwa na nani - Marijani Rajabu? una maneno haya... Paulina mamaa shemeji naleta mashitaka ee sielewi lengo la nduguyo ooh... kiitikio... Paulina mimi ninakwita, nimeshayakubali makosa, njoo mama tulee watoto... mimi naapa sitarudia tena...

Annina
 
Mkuu, Umechanganya nyimbo mbili hapo. Paulina wa Les Wa Nyika ambao ulikuwa unaanza na;
Paulina mamaaa,
shemeji naleta mashitaka,
sielewi lengo la nduguyo oo,
ni baya sana mamaa,
naona imani yake oo ni ndogo kwangu mamaa,

ambao kiitikio chake kilikuwa: Ingawa ndugu yako hanitaki mamaa,
naomba picha yake oo Stela mamaa,

na Paulina wa jabali la Muziki Marijani Rajabu ambao kiitiki chakr kilikuwa:

'Paulina mimi ninakwita,
nimeishayakubali makosa,
njoo mama tulee watoto,
 
Hii albamu yenye nyimbo ya Theresa ilikuwa na nyimbo tamu kama V.I.P,Shoga na Mama Chichi

Wimbo wa Shoga ulikuwa hivi

Nimeshtushwa na ujumbe ulionitumia kupitia kwa jirani yetu ambaye huwa anatusuka,umesema ukiniona ama zangu ama zako aaaa sababu eti namfuatafuata mumeoo

Nimeshtushwa na ujumbe ulionitumia kupitia kwa jirani yetu ambaye huwa anatusuka,umesema ukiniona ama zangu ama zako aaaa sababu eti namfuatafuata mumeoo

Shoga ee ee ukinirudi utanionea buree,shoga ee ee jeuri hiyo mimi sina eee

Shoga ee ee ukinirudi utanionea buree,shoga ee ee jeuri hiyo mimi sina eee

Shoga utanionea bure(oo mamaa) shoga sina kosa na wewe,ushoga wetu ulianza tangu utoto,tulichezea vifuu na sasa tuna wajukuu ooo sipendi matata...mmmh kuvunja heshima oo sipendi matata...mmmh kugombanisha watu oo sipendi matata,mmh jeuri hiyo sinaa oo sipendi matata....mmh nalia oo oo sipendi matata,cha mtu sikitaki ooh sipendi matata..aaah naogopa,hata michokochoko nakataa ooh sipendi matata,za uninja mimi nakataa ooh sipendi matata,naogopa aa..sikuzoea aa nakataa sipendi matata

Shoga ee ee ukinirudi utanionea buree,shoga ee ee jeuri hiyo mimi sina eee

Shoga ee ee ukinirudi utanionea buree,shoga ee ee jeuri hiyo mimi sina eee
 
Mwanzoni mwa miaka ya 80, Juwata jazz 'msondo Afya' walikuja na kibao cha

ETE

Ndugu yangu Ete pole kwa yaliyokukuta,
Ete ulipoolewa ulimkuta mwenzako nyumbani,
Pendo lako kwa mume wako oo,
Lilisababisha mwenzio kuachika bure,

Nyumbani alipoondoka,
Alikuendea kinyume yakakufika maradhi x 2

(chorus)

Mapenzi ya wake wawili haywezi kuwa ya ukweli,
Yangelikuwa ya ukweli Etee, yasingekufika x 2

Tutajitahidi nduguzo maradhi yakutoke,
Mola atakusaidia ndio mwenye uwezo,
(chorus)

Ungeyajua mama mapema katu usingejitosa,
ukeweza umekuponza Ete ee wateseka,
(chorus)
 
Wimbo wa Shoga ulikuwa hivi

Nimeshtushwa na ujumbe ulionitumia kupitia kwa jirani yetu ambaye huwa anatusuka,umesema ukiniona ama zangu ama zako aaaa sababu eti namfuatafuata mumeoo

Nimeshtushwa na ujumbe ulionitumia kupitia kwa jirani yetu ambaye huwa anatusuka,umesema ukiniona ama zangu ama zako aaaa sababu eti namfuatafuata mumeoo

Shoga ee ee ukinirudi utanionea buree,shoga ee ee jeuri hiyo mimi sina eee

Shoga ee ee ukinirudi utanionea buree,shoga ee ee jeuri hiyo mimi sina eee

Shoga utanionea bure(oo mamaa) shoga sina kosa na wewe,ushoga wetu ulianza tangu utoto,tulichezea vifuu na sasa tuna wajukuu ooo sipendi matata...mmmh kuvunja heshima oo sipendi matata...mmmh kugombanisha watu oo sipendi matata,mmh jeuri hiyo sinaa oo sipendi matata....mmh nalia oo oo sipendi matata,cha mtu sikitaki ooh sipendi matata..aaah naogopa,hata michokochoko nakataa ooh sipendi matata,za uninja mimi nakataa ooh sipendi matata,naogopa aa..sikuzoea aa nakataa sipendi matata

Shoga ee ee ukinirudi utanionea buree,shoga ee ee jeuri hiyo mimi sina eee

Shoga ee ee ukinirudi utanionea buree,shoga ee ee jeuri hiyo mimi sina eee

Mkuu Balantanda, hiki kilikuwa kifaa halafu kama nakumbuka kuwa wengi wa walioshiriki kukiweka hewani ni marhum kama Fred Benjamin, Athmani Momba,Suleiman Mbwembwe na wengine nimewasahau.
 
Jamani kuna mtu anaufahamu wimbo wa Patric Balisidya unaitwa Kuoana ni jambo la sifa na tena ni jambo la fahari ........naomba lyrics tafadhalini. Shukrani
 
Hii albamu yenye nyimbo ya Theresa ilikuwa na nyimbo tamu kama V.I.P,Shoga na Mama Chichi

Mama Chichi nacho utunzi wake Suleimani Mbwembwe hiki hapa

Mara nyingi duniani mtu hukisifu kilicho chake,ni vizuri duniani mtu kukisifu anachopenda

Mara nyingi duniani mtu hukisifu kilicho chake,ni vizuri duniani mtu kukisifu anachopenda

Kwa hiyo na mimi aa kwako Diana sina budi kufanya hivyo,Kwa hiyo na mimi aa kwako Diana sina budi kufanya hivyo.
Kwa vile unatimiza yale yote amabyo anayostahili kuyatenda mke wa mtu

Mara nyingi duniani mtu hukisifu kilicho chake(kilicho chake),ni vizuri duniani mtu kukisifu anachopenda(anachopenda)

Aiyolele iyo mama Chichi yeye(we mama),aiyolele iyo mama Chichi mama

Aiyolele iyo mama Chichi yeye(we mama),aiyolele iyo mama Chichi mama

(Mbwembwe)Barafu ya roho yangu mama Chichi mama mwenye mahaba ya Kipangani mama Chichi,yanayofanana na yale ya njiwa manga tunduni,sikiliza ninayosema mama Chichi mama

Aiyolele iyo mama Chichi yeye(we mama),aiyolele iyo mama Chichi mama

Aiyolele iyo mama Chichi yeye(we mama),aiyolele iyo mama Chichi mama

Barafu ya roho yangu mama Chichi mama mwenye mapenzi ya Kizamani mama Chichi,yanayofanana na yale ya njiwa manga tunduni,sikiliza maneno yangu mama Chichi mama

Aiyolele iyo mama Chichi yeye(we mama),aiyolele iyo mama Chichi mama

Aiyolele iyo mama Chichi yeye(we mama),aiyolele iyo mama Chichi mama

(Momba)Maisha ni safari ndefu itabidi tuheshimiane tujichunge na vizabizabina(zabina),maisha ni safari ndefu itabidi tuelewane na kila kwenye makosa tukosoane mama Chichi ee

Aiyolele iyo mama Chichi yeye(we mama),aiyolele iyo mama Chichi mama

Aiyolele iyo mama Chichi yeye(we mama),aiyolele iyo mama Chichi mama,malkia wa nyumba yangu mama Chichi mama

Maisha ni safari ndefu itabidi tuheshimiane tujichunge na vizabizabina(zabina),maisha ni safari ndefu itabidi tuelewane na kila kwenye makosa tukosoane mama Chichi ee

Aiyolele iyo mama Chichi yeye(we mama),aiyolele iyo mama Chichi mama

Aiyolele iyo mama Chichi yeye(we mama),aiyolele iyo mama Chichi mama,malkia wa nyumba yangu mama Chichi mama

Kasoro za binadamu tangu enzi na enzi ni kutopenda maendeleo ya mwingine(kama kiwangawanga) lakini sisi tupendane mapenzi ya njiwa kwani upendo na uaminifu ndiyo heshima ya ndoa

Nawe nami bara mpaka pwani,pamba moto shambliaa
Nawe nami bara mpaka pwani,pamba moto shambliaa
Nawe nami bara mpaka pwani,pamba moto shambliaa

Saga saga rhumba,saga saga rhumba
 
Mkuu Balantanda, hiki kilikuwa kifaa halafu kama nakumbuka kuwa wengi wa walioshiriki kukiweka hewani ni marhum kama Fred Benjamin, Athmani Momba,Suleiman Mbwembwe na wengine nimewasahau.

Yeah mkuu,kikosi kilikuwa kimetulia hasa...Walikuwepo Jery Nashon Dudumizi,Suleiman Mbwembwe,Fred Benjamin,Athuman Momba,Abdallah Mgonehazelu,Rahma Shally,Shabani Yohana 'Wanted',Bakari Semhando,Abuu Semhando,Omari Jamwaka(sina uhakika naye sana)...Kikosi kilikuwa kinatisha hiki aisee
 
Jamani kuna mtu anaufahamu wimbo wa Patric Balisidya unaitwa Kuoana ni jambo la sifa na tena ni jambo la fahari ........naomba lyrics tafadhalini. Shukrani

Patrick Balisidya, Owen, Jacky, Monte na Shebby Mbotoni na Afro 70 'Wana Afrosa' na Kibao cha HARUSI:

Kuoana ni jambo la sifa,
Na tena ni jambo la fahari kubwa,
Katika historia ya binadamu,

Ni shangwe isiyo kifani,
Kwa watu wawili waliopendana,
kuoana katika ndoa kamili,

Hivi leo Ndyanao na Saibaa mnaona,
Kumbukeni wazi mmetimiza ahadi yenu kwa mungu,\

Harusi mliyofanya ni kiapo kitakachowahukumu,
mara mtakapo jaribu kutengana,

Katika hali yoyote kaeni kwa amani nawausia,
Mpaka kifo kije kuwatenganisha x 2

(chorus)

Jaribuni kuwaepuka marafiki wabaya,
kwani huenda wakaipotosha ndoa yenu,
mkatenganaa, wakawadharau,

Wakumbukeni wazazi wenu wa pande zote,
watapopatwa na shida yoyote ile,
wasaidieni, mtapata baraka,

Kuweni na moyo wa mapenzi kwa mtu,
tena muwe wacheshi kwa kila mtu,
ni sifa kubwaa, mtaheshimiwa,

Kuweni wakarimu wakubwa nyumbani mwenu,
mzaapo watoto wenu muwatunze vyema,
wawe na adabuu, na heshima nyingii,
ndivyo walivyoishi wazazi wetu x 2

Patrick Balisidy aliutunga na kuuimba huu wimbo kwa ajili ya harusi ya dada yake Ndyanao kwa Saibaa kama anayowataja kwenye ubeti wa tatu.
 
Dalili zote zinaonesha kuwa wanamuziki wetu walikuwa na matatizo sana katika mapenzi!!! gademu!!

Mzee, si wakumbuka kibao cha JKT Mafinga, Wana Kimuli-muli alivyoimba mika iole?

Kitu mapoenzi kilianza zamani, tokea enzi za mambabu zetu
Na hata hao mapenzi waliyakuta, tokea enzi za Adamu na Eva....
 
Mkuu Balantanda, hiki kilikuwa kifaa halafu kama nakumbuka kuwa wengi wa walioshiriki kukiweka hewani ni marhum kama Fred Benjamin, Athmani Momba,Suleiman Mbwembwe na wengine nimewasahau.

Eeh! Jamani hivi na Fred Benjamin naye alishatutoka! Nilikuwa sina habari, Wanamuziki wengi sana wametangulia hadi mara nyingine nakuwa na hisia mbaya pengine wamepitiwa na umeme has nikiikumbuka orodha ya OTTU- Momba, Mwanyiro, TX, Mbwembwe... Inatisha
 
Back
Top Bottom