Tukumbushane: Wimbo bora wenye jina la kike...

Tukumbushane: Wimbo bora wenye jina la kike...

Waungwana mie kuhusu swala la kumi bora naomba mnitoe...
Coz nilikuwa nimeziorodhesha zikafika 7 kisha nikalikumbuka jiwe moja la Bimalee, goma lilikuwa linaitwa Makulata.
Basi ikabidi nivuruge top ten nzima...

''haki ya mama eeh
Nakupenda makulata
Nachotaka njoo unishike mkono twende mbele ya wazee...

Usifanye mchezo na pendo leetu eeh nakuupenda aaa mamaaa.....................

Popote ulipo nakuhitaji uje unihakikishie mapenzi yetu, kama kweli tutaoana, uendelee na tabia zako za ukarimu, tamaa mbalimbali nawe. Pesa mbalimbali nawe.......

Dah jamani mie hizo top ten simo.
 
Halafu kuna kitu jamani cha kuitwa Grolia...

Wanipa uchungu ooh mamaa
Iyo grolia mamaa eeeh

Hakimu alipoamuru nipelekwe gerezani
Kwa utapeli wangu ''aah mamaaa'' ulitoa kauli nikitoka gerezani hunitaki tena tusijuane tena...

Wanipa uchungu...................
 
Mimi Kumi Bora yangu Ni:

1. Selina - Muhidin Mwalimu Gurumo/Mlimani park Orchestre
2. Georgina - Marijani Rajab/Safari Trippers/wanaSokomoko
3. Mariam Cleopatra - Zahir Ally Zorro/Orcherstre Sambulumaa
4. Maumivu Makali - Kasongo Mpinda 'Clayton'/Issa nundu/MK Group (japo haukuwa na jina la kike!)
5. Dada Lidya - Patrick Balisidya/Montgomery Makangila/ Afro 70 band wana Afrosa
6. Christina Bundala - Muhidin Maalim Gurumo/Mlimani Park Orchestre
7. Christina - Marijani Rajab/David Mussa/Safari Trippers wana Sokomoko
8. Hanifa - " " " " " " "
9. Nzowa - Chinyama Chiyaza/Motombo Lufungulo 'Audax'/Orchestre Marquiz Du Zaire Wana kamanyola.
10. Betty - Mbaraka Mwishehe Mwaruka/Morogoro Jazz Band
 
Selina wa Mlimani Park hadi kesho kutwa huu wimbo bado unanigusa sana kwa jinsi ulivyopangwa na kupangika siyo hizi Bongo flava...ingawaje ziko chache ambazo ni nzuri kiasi chake. Lakini kamwe huwezi kulinganisha na Dar Jazz, Moro Jazz, Magoma kita kita, Mlimani, Vijana, Jamhuri Jazz, Butiama Jazz, Marquiz na nyingi nyinginezo ambazo zilivuma sana katika anga ya Muziki wa Tanzania na hata Afrika ya Mashariki kama siyo Afrika nzima.
 
My top ten:

  • uniambie kama ni kweli - Marques du Zaire (Kiki)
  • Salama – Marijani
  • Neema - Mlimani Park
  • Imaculata - Vijana (dudumizi)
  • Theresa – Vijana (dudumizi)
  • Hiba – Mlimani
  • safari siyo kifo – Tancut almasi
  • Bela – Bimalee (Roy + Kakere)
  • Nzela – Banana
  • Neema – Diamond sound
 
sasa mbona tena msikitini unaingia na viatu?
ktk top ten yako hao watu wa mwisho wamefuata nini?
Yaani ni sawa na pilau kutia mlenda.....
 
Selina wa Mlimani Park hadi kesho kutwa huu wimbo bado unanigusa sana kwa jinsi ulivyopangwa na kupangika siyo hizi Bongo flava...ingawaje ziko chache ambazo ni nzuri kiasi chake. Lakini kamwe huwezi kulinganisha na Dar Jazz, Moro Jazz, Magoma kita kita, Mlimani, Vijana, Jamhuri Jazz, Butiama Jazz, Marquiz na nyingi nyinginezo ambazo zilivuma sana katika anga ya Muziki wa Tanzania na hata Afrika ya Mashariki kama siyo Afrika nzima.

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=hT90oQU4Jpo[/ame]
 
Kipenzi changu editha sikia nikupe ukweli niliokuwa naao...
Kusema kweli nimechoshwa na tabia yako...

Ni siku nyingi nimeelezwa mengi nimeyapuuza, nilijua ni fitina za majirani tu wanataka kututenganisha...

Nitokapo kazini sikukuti...
Nikuulizapo ulikuwa wapi...
Nilikuwa kwa shangazi kariakoo...
 
Jamani nimeangalia huu wimbo wa Akon mpya wa oh Africa,je huyo alopaka rangi ya Bondera ya tz ni mtz?maaana wengi wao wamerepresent nchi zao,actually ameongelea mlima mrefu africa..big up akon swali angu ni...mpaka tutangaziwe mlima wetu na wengine jamani?kwa hakika tunaweza wenyewe wakuu au sio?yangu hoja tuu wazee
 
Wale ambao tunaingia kwenye utu uzima bila shaka mtakumbuka bonge la wimbo miaka ya katikati ya 1980 ulioitwa MAWAZO. Nadhani uliimbwa na kutungwa na Emmanuel Joseph ambaye aliwahi kuanzisha bendi ya EJO Star. Ukisikiza ule wimbo utadhani ni stori ya ukweli ingawa sina hakika kama ni wimbo tu au ilikuwa kweli.

Mashairi

Nilitembea Jijini Dar esalama nikakutana na msichana mmoja,
Nikamwuliza waitwa nani akaniambia jinalake Mawazo...

Nilipofika nyumbani kwakee, eeeh,
Nilikutana makundi ya watuu, uuh
Wakanieleza eti amefariki usiku wa jana kuamikia leo... Mawazooo, ooh, Mawazo ooho!
 
Wakuu mupo????,naona thread imedoda...Tumeitelekeza..hahaaaaaaaaaa
 
kuna nyimbo ziliimbwa na John Kitime akiwa na Vijana Jazz(Pambamoto awamu ya pili) zaitwa Malaine na Nyongise...Zilikuwa nzuri sana
 
Maria wangu.....
hata mtunzi si mkumbuki mamake ni wa zamani sana RTD waliupenda sana wakati wa kile kipindi cha salamu asubuhi nadhani kilikuwa kinaanza saa mbili. Enzi hizo bwana, ujamaa uko juu na sukari mpaka mkanunue RTC marufuku kuzidisha kilo moja!
 
Kuna wimbo mmoja naona wote tumeushahu nadhani ulipigwa na OSS- Ndekule; uliitwa Aminani Mandari yaani utadhani ni kisa cha kweli jinsi MAx Bushoke alivyokuwa analalamika... "anakumbukwa na ndugu na jirani zakee eeenhe then Mola mlaze pema peponi roho yake, Aminani Mandari mpenzi sitamsahahu...
 
Wakuu mupo?.........kitambo sana..........Leo nimeshinda naukumbuka na kujiimbia kitu Hiba cha Nginde,Utunzi na uimbaji wake Hassan Rehani Bitchuka..................dah!!!

Hiba nimelibeba pendo lako,kama mwana na mbeleko,Hiba nimelibeba pendo lako,kama mwana na mbeleko,
Nina maana kukwambia mchana usiku silali natafuta pesa,Nina maana kukwambia mchana usiku silali natafuta pesa,
Ili tuishi vizuri na kujenga familia bora yenye thamani na penzi,Ili tuishi vizuri na kujenga familia bora yenye thamani na penzi
Hiba mekuwaje mpenzi mbona umebadilika aaaaaa,Hiba mekuwaje mpenzi mbona umebadilikaaaaaaaaaaa(bridge)

Aaaa Hiba hiba hiba.........Nimekukosea nini mpaka kufika kunikataa Hiba....ehh..........Hiba

Ili tuishi vizuri na kujenga familia bora yenye thamani na penzi(iiiiiii),Ili tuishi vizuri na kujenga familia bora yenye thamani na penzi
Hiba mekuwaje mpenzi mbona umebadilika aaaaaa,Hiba mekuwaje mpenzi mbona umebadilikaaaaaaaaaaa

Kiitikio(wote): Hiba oooh Hiba imekuwaje Hiba Hiba ooh Hiba nieleze leo,Hiba oooh Hiba imekuwaje Hiba Hiba ooh Hiba nieleze leo

Bichuka: Badiliko la pendo lako lanitia wasiwasi,lipi nililokuudhi ooh ooh Hiba, Badiliko la pendo lako lanitia wasiwasi,lipi nililokuudhi ooh ooh Hiba..Ninapokuuliza hutaki kusema nami Hiba,ninapokuuliza wewe unanunanuna,..ninapokuuliza hunisikii hata kidogo Hiba,....ninapokuuliza wewe unanunanuna,....Unanisikitisha sana unapokataa kula nami Hiba....

Kiitikio(wote): Hiba oooh Hiba imekuwaje Hiba Hiba ooh Hiba nieleze leo,Hiba oooh Hiba imekuwaje Hiba Hiba ooh Hiba nieleze leo

Ninapokuuliza hutaki kusema nami Hiba,ninapokuuliza wewe unanunanuna,..ninapokuuliza hunisikii hata kidogo Hiba,....ninapokuuliza wewe unanunanuna,....Unanisikitisha sana unapokataa kula nami Hiba....

Back
Top Bottom