Patrick Balisidya, Owen, Jacky, Monte na Shebby Mbotoni na Afro 70 'Wana Afrosa' na Kibao cha HARUSI:
Kuoana ni jambo la sifa,
Na tena ni jambo la fahari kubwa,
Katika historia ya binadamu,
Ni shangwe isiyo kifani,
Kwa watu wawili waliopendana,
kuoana katika ndoa kamili,
Hivi leo Ndyanao na Saibaa mnaona,
Kumbukeni wazi mmetimiza ahadi yenu kwa mungu,\
Harusi mliyofanya ni kiapo kitakachowahukumu,
mara mtakapo jaribu kutengana,
Katika hali yoyote kaeni kwa amani nawausia,
Mpaka kifo kije kuwatenganisha x 2
(chorus)
Jaribuni kuwaepuka marafiki wabaya,
kwani huenda wakaipotosha ndoa yenu,
mkatenganaa, wakawadharau,
Wakumbukeni wazazi wenu wa pande zote,
watapopatwa na shida yoyote ile,
wasaidieni, mtapata baraka,
Kuweni na moyo wa mapenzi kwa mtu,
tena muwe wacheshi kwa kila mtu,
ni sifa kubwaa, mtaheshimiwa,
Kuweni wakarimu wakubwa nyumbani mwenu,
mzaapo watoto wenu muwatunze vyema,
wawe na adabuu, na heshima nyingii,
ndivyo walivyoishi wazazi wetu x 2
Patrick Balisidy aliutunga na kuuimba huu wimbo kwa ajili ya harusi ya dada yake Ndyanao kwa Saibaa kama anayowataja kwenye ubeti wa tatu.
Na huyu Ndyanao ndiye mtunzi wa kitabu cha SHIDA, ambapo wahusika wakuu ni Matika "Shida" na Sefu "Chonya of Chilonwa me"