Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Kumekuwa na tabia ya kushabikia, kuona inastahili au kuchukulia jambo la kawaida tu kile kinachoitwa "kupakwa mafuta" kwa wanaume na wanaotembea na wake za watu wengine. Huu ni upuuzi mkubwa sana hasa kwa jamii inayojinasibu kwa sehemu kubwa kama ya kidini na inayopinga ushoga. Hata kama mtu ametembea na mke wa mtu ni wendawazimu kuona adhabu inayomfaa ni "kumpaka mafuta"/ulawiti. Jambo la kusikitisha kuna raia wengi kwa maoni yao mtandaoni wanaona hili jambo stahiki kwa watu wanaochepuka na wanandoa wa watu wengine!