Mazee sikiliza. Mimi adhabu ya mke anayechepuka ni moja tu. Bye bye, nenda ukaishi salama. No compromise no discussion! Hii ni kanuni ambayo nilishajiwekea. Halafu: mimi nina experience ya maisha. Katika migogoro mingi ya mke kuchepuka niliyoshohudia, mara nyingi unakuta mwanaume mhusika ni mtu anayemfahamu mume wa mwanamke, na pengine yuko karibu naye eg mtaani au kazini. Kwa kifupi anakuona kama mjinga na yeye ni mjanja. Hapo ndipo suala la adhabu kwa mgoni linapoingia sasa. Kwa kifupi mke atafurumishwa na wewe utapata stahiki yako kwa wakati nitakaopanga mimi. Hata ikichukuwa miaka mitano, nitakunyemelea polepole nikupe stahiki yako. Mind you siyo laima iwe ni kutifua mtaro.