Jamaa alitegeshwa,
Siku moja kajibebea kama kawaida yake, kumbe Malaya keshawatega wahuni.
Anaingia tu loji hata hajaoga Bado, anagongewa hodi.
Kufungua tu,
Kakutana na njemba zinajitambulisha kua uyo Dem alokua nae Ni mke wa mmoja wao.
Jamaa alichapika ipasavyo ndani ya ile loji, baada ya hapo alipotea km wiki 2 kibaruani haonekani anauguza tu vidonda.
Mwezi mmoja baadae,Akapona kabisa.
Jamaa kasahau Tena yaliyomtokea na kurejea Tena kwny tabia yake.
Akarudi kijiwe kile kile na kuopoa Malaya,
Sasa yule Malaya akamshawishi wakafanyie mapenzi kwake kuokoa gharama za gesti.
Jamaa akakubali na kwenda anakoishi Malaya.
Alipoingia TU,
Binti akamwambia, Leo ndo utakua mwisho wa uzulumaji wako na unaenda kuozea jela.
Hajakaa sawa, akaona binti anachukua kisu na kuchana chana nguo zake.
Kisha akaanza kupiga yowe za kubakwa.
Watu walijaa sana pale, Simu zikapigwa polisi jamaa akabebwa mpk kituoni.
Binti ikabd akapimwe,
Ushahidi wa daktari ukaonyesha Ni kweli binti kaingiliwa masaa 6 yaliopita.
Kesi kila ikipelekwa mahakamani inapigwa kalenda, mara Upelelezi haujakamilika Mara shahidi Ana udhuru, Mara hakimu hayupo.
Jamaa alisota rumande Miezi 7
Kesi ikaunguruma na dalili zikaonesha kabisa kesi hii anashindwa.
Na akishindwa, lazima Miaka 15 jela imhusu.
Basi,
Ikabidi ndugu zake jamaa wakaombe msamaha kwa wale Malaya ili yaishe nje ya mahakama.
Familia yake ikachangishana,
Wakahonga Hakimu, karani mpk polisi ili kesi izimwe.
Familia ilikua masikini, Wakauza hadi mashamba ya familia.
Wale Malaya walikula mgao wa million 3
Hakimu million 2
Polisi, karani na wapuuz wengine wakala Kama million 1.5
Kesi ikafutwa,
Jamaa anarudishwa uraiani.
Sent using
Jamii Forums mobile app