Tukutane hapa tuliowahi kutoa na kupewa talaka, tujadili maisha baada ya talaka

Tukutane hapa tuliowahi kutoa na kupewa talaka, tujadili maisha baada ya talaka

Mmoja akishashitaki mahakamani na kufungua kesi rasmi tayari mpaka hapo talaka haikwepeki labda tu kabla ya kesi kufika mwisho ninyi wenyewe muamue kuiondoa kesi mahakamani! Hapa ninamaaisha mahakama ndio itakulazimisha kutoa talaka kwa mujibu wa sheria na itazigawa mali zenu hata kama utazuia vipi!

Kule mahakamani wakigundua kuna mali huwa wanafurahi sana. Wanajua watapiga hela kutoka kwa mtoa na mpokea talaka.
 
Ni hatari sana..!! Nina ndugu yangu, maneno ambayo mwanamke aliyaongea mahakamani hakutegemea hata kidogo..!! Mwanamke ndo aliyekuwa anadai talaka kwa nguvu zote. Ilifika point akatakiwa aeleze sababu za kudai talaka. Moja ya sababu aliyoitaja ilikuwa ni kutakwa kinyume na maumbile..!! Jamaa yangu ilimshitua ile mbaya..!! Wala hakutegemea hilo..!! Na kile kitendo cha kujikusanya baada ya kutawanywa na maneno hayo, watu wote pale mahakamani walipigwa na butwaa wakiamini madai hayo ni ya kweli..!! Mwishi wa siku waliachana na athari zake kila mmoja kwa wakati wake anazipata hadi hivi sasa.

Wanawake ikishafika kwenye talaka na mko kwenye kugawana mali ni wabaya sana. Jambo kama hilo lilimtokea jamaa baada ya mke kusema mahakamani kuwa jamaa hamtoshelezi kimapenzi hana nguvu za kiume. Jamaa alichanganyikiwa sana. Na sijui kwanini, mara nyingi wanawake ndio wanaonekana victims ikifika hiyo stage. Jamaa alikuwa na malinyingi waligawana pasu pasu.
Chanzo kilikuwa mume kugundua kumbe mke ana maisha yake nje ya ndoa yao, biashara, majumba bila mume kujua.

Kikubwa ikishafika huo wakati wa mahakama na mke anadai talaka, jitahidi malizana nae tu.. anaweza kukudhalilisha ukapoteza mwelekeo kabisa... hakawii kusema alikufumania una liwa na mwanaume mwenzio... pata picha unakutana na statement kama hiyo mahakamani ... watu wamejaa ndugu na jamaa zako?

Hapo anakuwa ameshapikwa na marafiki na wanasheria kwa mpango kuwa akipata mali anawakatia cha kwao.
 
Habari wanabodi wenzangu, Katika maisha kuna kuoa na kuolewa, hivyo kuna kutoa talaka na kupewa talaka.

Katika hali zote hizo maisha yanaendelea, kuna ambao hufanikiwa zaidi au kurudi nyuma kimaisha chanzo kikiwa ni talaka. Changamoto na faida pia hujitokeza, wengine hufikia hali kujuta kwanini wametoa talaka au kupewa talaka, lakini pia kuna wengine hufikia mahali husema bora alivyoacha au kuachika.

Wengine wanashindwa kumove on wanabaki na majeraha milele, wengine hupoteza watoto, mali na kazi bada ya talaka.

Karibuni wadau tuliowahi kuingia kwenye ndoa na kukutana na talaka au kuachana na wenza wetu ambao tulidhani tutazikwa nao.

Pia wapo watoto humu ambao walishuhudia wazazi wao wakipeana talaka, je maisha yalikuaje?

ukuryani sisi hatunaga talaka
 
Teheeeeee walishasema muishi nao Kwa akili . Mwanamke akisha Anza maisha yake ya nje bila baraka za mume trust me every thing will fall apart
 
Back
Top Bottom