Tukutane hapa tuliowahi kutoa na kupewa talaka, tujadili maisha baada ya talaka

Tukutane hapa tuliowahi kutoa na kupewa talaka, tujadili maisha baada ya talaka

Mkuu mimi nime move on japo sijutiii kuwa nae, aliniacha bada ya yy kupangiwa kazi serikalini Mwanza wakat mm npo Dar, so nikamkosa hivyo
Yani hivyo tu ndio upewe talaka?
Ebu kuwa mkweli hukuwahi kuchepuka mkuu?
Na sasa hivi jimbo liko wazi au lilishapata muwakilishi?
 
Upo sahihi, mwishowe watoto wanakuwa wahanga kwa mambo yasiyowahusu.

Hata kama ni lazima mtengane suala la watoto namna watakavyopata mahitaji yao lijadiliwe na lipatiwe ufumbuzi.
Wengine hata hawajali kuhusu watoto. Kabla hata talaka wameshaanza mahusiano mengine. Bora muache watoto wakue kwanza ndio muwe na mahusiano ya wazi.
 
Yaani navyozidi kuisoma jamii nyingi na dunia kuujumla. Najiona sikufanya chaguo baya kurudi home kuoa.
Sie huwa hakunaga talaka.
Yaani unamuacha mke anaishi tu na watt basi wewe unaoa mke mwingine maisha yanaenda.
Yule anakuwa jina kuwa Ni mke wa fulani.
Hata akienda kuolewa ama kula Bata maisha yake yote Ila mwisho wa siku atarudi tu kwao na mwanaume ndiko atakakozikwa.
Mana Tayari kwao walimfanyia Ile inaitwa send OFF.
Mnajua Mana ya Hilo neno lakini ama huwa tunalishadadia kuwa leo anafanyiwa send off jamani.
Kwa anayejua Mana ya English nadhani atanielewa.
😂😂
Utakuwa poti bila shaka..
Maana kwa lugha ile hata msamiati wa neno 'talaka' hakuna!
 
Mwanaume wa kweli hajutii maamuzi ya kuachana na mwanamke asiyeeleweka[emoji23][emoji23].

Kuna hawa wanao complain sjui kuhusu mgao wa mali na mazagazaga ya kiuchumi, hivi mwanaume uliyeteseka kutafta vitu vya thaman unaanzaje kugawana na mtu unayeachana nae ilihali umevitafta wew?

Ujinga ni pale mkiwa kwenye ndoa mnajisahau na kujikuta malaika kwa kuanza kushare kila kitu, mnajenga pamoja, mnanunua magari pamoja, wengine mpka card zenu za benk mnashare na wake zenu, si vibaya lkn hil jambo litakuja kukucost na utajuta sana.

Tunawashauri kila siku, owa ukiwa umetimiza angalau nusu ya ndoto zako, huyo mke unayeoa asijekuwa sehem ya wew kutimiza ndoto za mafanikio kiuchumi bali akute ushafanikiwa au aje amalizie gap dogo tu.

Owa ukiwa na mali zikiwa zimeandikishwa na wanasheria mmiliki halali weka hata wazaz, kama huna weka ndugu&jama unaowaamini ama baazi ya mali zako zifiche hata huyo msaliti wako wa baadae asijue unamiliki mali kiasi gani.

Dunia imeharibika siku hizi wanawake wanaingia ktk ndoa kimkakati sana, wapo wanaoingia kwa maigizo waje wachume na kupotea kuwarudia mabwana zao wa mwanzo(wadangaji)

Pia wapo wanaohusishwa na familia zao kuingia ktk ndoa kimkakati kwenda pia kuwinda mali, na baada ya kupata ni majuto kwa mwanaume hufuata kama sio kurogwa na kugeuzwa msukule ama kufa na vitu vyako vinyang'anywe.

Wapo ambao kwa tamaa zao tu za kingono huamua kujitoa ktk ndoa na kuingia kimahusiano na wanaume wengine, so hata hapa lazma mali zako zigawanywe kwa masingizio ya sheria na upuuzi mwingine.

Unatakiwa kujua mke uliyeoa si ndugu yako na hatowai kuwa ndugu yako kamwe ndiomaana unashiriki nae matendo ambayo huwezi kuyashiriki na ndugu zako, hivyo hata imani kwake iwe kwa kiwango ambacho hakitakuumiza.

Ishi nae kwa akili hatakama akili huna ila jitahidi kuelewa kuwa huyo hutoishi nae milele taka usitake kwa wanawake wa kizaz hiki, kuachana nikama sunna kwao.

Hakikisha furaha yako unaijenga nje ya mategemeo ya mtu, narudia tena, hakikisha mali zako hazitomuhusu siku mkiachana maana atakurudisha nyuma mafanikio uliyopambania muda mrefu.

Wabishi ndio waliwao

Copy that
 
Sasa oa kisa jogoo linawika Mara umeona tako,sura,paja,kwapa Safi,elimu, mshahara wake,utajiri wao,rangi yake,dini yake,
Hayo yote Ni temporary huwa Yana fade away.
Once we get used with something new we get bored with it.
Hata kazi ukishaizoea huwa unaichoka na inaboa. Biandamu ameumbiwa kuwa adventurer.
Na yeye akishakuzoea akaonja nje hauoni shida kukuondoa kisa Cha kufaidi penzi jipya.
Yaani Kuna mwanamke wa jamii fulani kukuachana na wewe/kukua/ kukuacha kisa Cha kupigika Ni rahisi mno Kama kubadilisha underwear jamani.
😅😅😅 Naona umetuchamba mno si viboro dinda
 
Kutoa talaka sio Jambo la kufurahisha hata kidogo, kwani mwenye anatoa anaumia na anaepokea anaumia vile vile, hakuna mtu ambaye Ni mbaya totally

Kunayo mazuri kadhaa anakua nayo lakini anapokua anakosea mtu unaamua kumhukumu kwa makosa yake ya mwanzo na mnadivorce ,

Soon mnapoachana ndipo utaanza kugundua gap imejitokeza,utaanza kugundua baadhi ya action nzuri alzokua nazo mtalaka wako,utaanza kuumia na wewe japo utajipa matumaini kwa kujikumbusha mabaya yake,
Apo Kama mlikua na watoto hio Ni mada nyingine kabsa na changamoto zake Ni hazielezeki,.

Talaka Ni chungu kwa anaetoa na anaepokea ,tofauti yake Ni mtoaji atakua anafrai wakati wa kutoa while mpokeaji anaumia ila baada ya muda Ni either wote watakua wanaumia au mpokeaji atakua ashapona na alietoa anajutia.
Maisha kabla ya ndoa ni mazuri sana kwa sbb ya uwepo wa nidhamu ya hali ya juu na maigizo ya kutosha.
Maisha baada ya ndoa kiburi, dharau, jeuri vinastawi na kuwa mahali pake, na kufuta uwepo au umuhimu wa ndoa.

Ukweli ni kwamba talaka, zina faida zake hasa nyakati zetu hizi. Badala ya kuishi kwenye mazingira hatalishi kwa afya ya akili, mwili na roho ni bora kila mmoja akatafuta njia yake.
TALAKA NI BORA KULIKO WATOTO WASIKIE BABAYAKO ALIUA MAMA YAKO!
 
Wengine hata hawajali kuhusu watoto. Kabla hata talaka wameshaanza mahusiano mengine. Bora muache watoto wakue kwanza ndio muwe na mahusiano ya wazi.
Yaani nikose kufurahisha nafsi yangu kisa watoto. Kwani maisha ni watoto tuu?
 
Huwezi endelea kukumbatia kifo eti kwa ajili ya mustahbali wa watoto.
Niliandika Ili watu wajue kuwa kutokuelewana ndani ya nyumba matokeo yatakuwa mabaya zaidi kwa watoto wao enfapo watafikia hatua ya kuachana, kama ni ndoa iliyoshindikana baaasi sijahimiza watu waendelee kuwa pamoja
 
Mkioana nyota zenu zinafanana ni ngumu talaka mtazisikia kwa wengine.Mtaishi zaidi ya ndugu plus kufanana sura.
Mkuu ni kweli kabisa nasaidiki, lakini nadharia hii hukutana na kizingiti cha muda na mazingira yenu, kadri muda unavyoenda ndipo picha halisi kati yenu huonekana. Pia mazingira mnayoishi, wanandoa mnapoelewana huwaga kuna hasadi, fitna na husda sana toka kwa watu wanaowazunguka kwa maana ya majirani, marafiki na ndugu bila hata ya kujua zimetokea vipi.

Mtajikuta siku mnaingia mtego kirahisi sana na kisha mkaachana, huwezi amini anaewaachanisha anaweza kuwa hata mama au baba yenu mzazi, eti kwasababu ya mambo ya kijinga. Katika maisha yenu ya ndoa omba sana muishi katika misingi ya dini haswa ( kwa kumuogopa Mungu), hekma, uvumilivu na ustahamirifu pamoja heshima.

Ndoa ni nzuri sana lakini haijawahi kuwa rahisi hata kidogo ina mambo mengi na mitihani mingi sana, kuivuka inahitaji nguvu ya Mungu pekee pamoja na hekima iliyopitiliza. Talaka haijawahi kuwa suluhisho la matatizo kwenye ndoa bali ni tatizo haswa mnapokuwa mmeshazaa. Talaka ni halali kutolewa endapo tu kuna ulazima na mazingira ya kufanya hivyo, vinginevyo talaka si kitu cha kukimbilia kabisa.
 
Talaka isikisge kwa mtu mwingine tena bora mpeane talaka kabla hamjachuma mali nyingi au za gharama kubwa ambapo kiuhalisia mwanaume ndiye huwa amevujisha jasho jingi! Tena itokee mwanamke alikuwa na ajira hata kama ni ps wa mlinzi (salary kima cha chini kabisa) na wewe ofisa wa ngazi flani ya juu!

Sote tunajua wanawake wengi hata awe na ajira mshahara wake ni kwa ajili ya nguo na vipodozi, lakini wakifika mahakamani hao huongea uwongo mkavu anaweza hata kusema ulikuwa ulishamnyanganya kadi ya benk na mshahara wake hakua anagusa hata mia!

Mgao wa mali katika mazingira kama hayo huwa unauma sio mchezo!
Ni hatari sana..!! Nina ndugu yangu, maneno ambayo mwanamke aliyaongea mahakamani hakutegemea hata kidogo..!! Mwanamke ndo aliyekuwa anadai talaka kwa nguvu zote. Ilifika point akatakiwa aeleze sababu za kudai talaka. Moja ya sababu aliyoitaja ilikuwa ni kutakwa kinyume na maumbile..!! Jamaa yangu ilimshitua ile mbaya..!! Wala hakutegemea hilo..!! Na kile kitendo cha kujikusanya baada ya kutawanywa na maneno hayo, watu wote pale mahakamani walipigwa na butwaa wakiamini madai hayo ni ya kweli..!! Mwishi wa siku waliachana na athari zake kila mmoja kwa wakati wake anazipata hadi hivi sasa.
 
Talaka isikisge kwa mtu mwingine tena bora mpeane talaka kabla hamjachuma mali nyingi au za gharama kubwa ambapo kiuhalisia mwanaume ndiye huwa amevujisha jasho jingi! Tena itokee mwanamke alikuwa na ajira hata kama ni ps wa mlinzi (salary kima cha chini kabisa) na wewe ofisa wa ngazi flani ya juu!

Sote tunajua wanawake wengi hata awe na ajira mshahara wake ni kwa ajili ya nguo na vipodozi, lakini wakifika mahakamani hao huongea uwongo mkavu anaweza hata kusema ulikuwa ulishamnyanganya kadi ya benk na mshahara wake hakua anagusa hata mia!

Mgao wa mali katika mazingira kama hayo huwa unauma sio mchezo!
50/50 kesho kutwa nauza nyumba za wanandoa na kiwanja, ni kizuri balaaa, mahakama haijawaji kosea, huwezi mfubaza binti wa watu ukamzalisha akakondeana afu unataka aondoke mikono mitupu
Hapana ni 50/50

Athante mahakama
 
Roho ya talaka haiwezi kuja kama hamjapata watoto. Lengo la talaka ni Ili watoto waharibike kwa kukosa msingi uwepo wa baba na mama Ili waweze kubalance saikolojia yao maishani.
 
Niseme ukweli nipo katika harakati za either nitoe talaka ama nipewe talaka nikiwa nimezaa nae watoto wawili.

sasa tumetengana imetimia mwaka tangu mgogoro uanze kimsingi napitia wakati mgumu saana kwakua tuna watoto wadogo wawili na mwenzangu anashindwa kujizua na kutumia watoto kama sehemu ya kuniadhibu baada ya kuona sijaonesha uteyari wa kuridisha moyo kutoka na kiburi chake na mabaya aliyonitendea...

katika mapenzi hamna kitu nakumbuka saana kwake zaidi ya kusema tungekua pamoja watoto wasingekua katika hali ya mfadhaiko wa kisaikolojia walio nao sasa hasa binti yetu wa miaka 7.
Nakiri kabisa TALAKA ni uzoefu MBAYA MNOO niliyo na ninao pitia kuliko
Umeandika kwa huzuni sana bro toa talaka tembea mbele nakuhakikishia ukirudisha moyo eti kwa kuwa mna watoto utapigwa tukio ambalo duniani na mbinguni hutasahau huyo mtoto wa miaka 7 sheria inakurusu kuwa nae miaka hii kwa sasa walezi wa watoto wamekuwa ni wanaume na sio wanawake.
Mwanamke ambaye mmetengana mwaka then leo umrudishe eti watoto bro nimekaa pale episode ya pili itakayokukuta ni balas
 
Back
Top Bottom