Nadhani shida ilianzia hapa ".... alikua anachake na mimi nina changu ...."
1. Hivi mlikua mnaoana ili iweje ? Kama kila mtu ana chake, hamkuwahi kusoma "mume atawacha wazazi na mke atawacha wazazi nao watakua mwili mmoja ambayo ndio maana ya ndoa, sasa nyie mlikua mnaoana kama fashion au ?! Mwili mmoja gani kila mmoja ana kwake, ana chake ana mamlaka yake ?! Ebo !!
2. Bila shaka mlikua watu wa 50/50 haki sawa. Yeye chake mewe chako si ndio ? Ndoa za hivi lazima zivunjike hata zisipovunjika ni maisha ya mitifuano na minyukano ya kufa mtu.
Ndoa kudumu, tena zaidi kua tamu LAZIMA KUWE BAYANA KIONGOZI NI MUME, MAMLAKA YOTE YAKO KWA MUME na kwa UPENDO mume ajue wajibu wake kwa mke na atimize kwa upendo. Haya mambo yenu ya women empowerment, 50/50 yeye ana kwake na wewe una kwako, superwoman bla bla blah yanawatokea puani wengi.