Tukutane hapa tuliowahi kutoa na kupewa talaka, tujadili maisha baada ya talaka

Tukutane hapa tuliowahi kutoa na kupewa talaka, tujadili maisha baada ya talaka

Mwanaume wa kweli hajutii maamuzi ya kuachana na mwanamke asiyeeleweka[emoji23][emoji23].

Kuna hawa wanao complain sjui kuhusu mgao wa mali na mazagazaga ya kiuchumi, hivi mwanaume uliyeteseka kutafta vitu vya thaman unaanzaje kugawana na mtu unayeachana nae ilihali umevitafta wew?

Ujinga ni pale mkiwa kwenye ndoa mnajisahau na kujikuta malaika kwa kuanza kushare kila kitu, mnajenga pamoja, mnanunua magari pamoja, wengine mpka card zenu za benk mnashare na wake zenu, si vibaya lkn hil jambo litakuja kukucost na utajuta sana.

Tunawashauri kila siku, owa ukiwa umetimiza angalau nusu ya ndoto zako, huyo mke unayeoa asijekuwa sehem ya wew kutimiza ndoto za mafanikio kiuchumi bali akute ushafanikiwa au aje amalizie gap dogo tu.

Owa ukiwa na mali zikiwa zimeandikishwa na wanasheria mmiliki halali weka hata wazaz, kama huna weka ndugu&jama unaowaamini ama baazi ya mali zako zifiche hata huyo msaliti wako wa baadae asijue unamiliki mali kiasi gani.

Dunia imeharibika siku hizi wanawake wanaingia ktk ndoa kimkakati sana, wapo wanaoingia kwa maigizo waje wachume na kupotea kuwarudia mabwana zao wa mwanzo(wadangaji)

Pia wapo wanaohusishwa na familia zao kuingia ktk ndoa kimkakati kwenda pia kuwinda mali, na baada ya kupata ni majuto kwa mwanaume hufuata kama sio kurogwa na kugeuzwa msukule ama kufa na vitu vyako vinyang'anywe.

Wapo ambao kwa tamaa zao tu za kingono huamua kujitoa ktk ndoa na kuingia kimahusiano na wanaume wengine, so hata hapa lazma mali zako zigawanywe kwa masingizio ya sheria na upuuzi mwingine.

Unatakiwa kujua mke uliyeoa si ndugu yako na hatowai kuwa ndugu yako kamwe ndiomaana unashiriki nae matendo ambayo huwezi kuyashiriki na ndugu zako, hivyo hata imani kwake iwe kwa kiwango ambacho hakitakuumiza.

Ishi nae kwa akili hatakama akili huna ila jitahidi kuelewa kuwa huyo hutoishi nae milele taka usitake kwa wanawake wa kizaz hiki, kuachana nikama sunna kwao.

Hakikisha furaha yako unaijenga nje ya mategemeo ya mtu, narudia tena, hakikisha mali zako hazitomuhusu siku mkiachana maana atakurudisha nyuma mafanikio uliyopambania muda mrefu.

Wabishi ndio waliwao
Talaka ni mbaya sana

Hivi majuzi nimeona mtu akifilisika kabisa baada ya talaka.

Sasa hivi anasambaza hizi bidhaa za GNLD.
 
Mkuu usipende kuandika majina ya ndgu zako kwenye mali zako iwe wamejua au hawajajua, kama una watoto waandike watoto sababu haohao ndgu wanaweza kukugeuka kabla hata hujafa au ukiondoka hapa dunian hakuna atakaejua hata kumlipia mwanao ada wala kumsaidia. Yunaona sahv watu wanalia sana ndgu wamewafanya ndivyo sivyo, utataman bora ungemwamdika mke au watoto kama humuamin mke wako

Sent from my SM-G930V using JamiiForums mobile app
 
Ndoa ni hiyari iliyo halalishwa na Mungu.
Tena ndoa ni kiapo mbele za Mungu.
Binadamu tumekuwa na kawaida ya kuvunja,
-- ndoa zetu,
--Ndoa za ndugu zetu,
--Ndoa za marafiki na jamaa zetu bila kujali.
Elewa tunafanya makosa makubwa sn mbele za Mungu.

Ni kweli kuwa ndoa inafika mahali inafifia na kukosa mapenzi ya mke na mume.
Lakini ni vizuri zaidi wahusika wakakaa na kujadili jinsi gn wataweza kurudisha mapenzi kwenye ndoa yao,
na sio kuvunja ndoa,
Tena bila sababu za msingi.,,

Talaka sio kitu kizuri ndg zangu,
Kitendo cha mwanaume kutoa talaka,
au mwanamke kuomba talaka,
Ni Sawa na kuvunja ahadi ambayo mliiweka mbele za Mungu kwamba mtapendana kwa shida na raha kwa maisha yenu yote.
Talaka huwa ina kawaida ya kurudi kwa wanandoa na kumuhukumu yule mkosefu,

Kuna mwanamke ambaye yeye ndy chanzo cha ndoa kuvunjika,
Lakini bado anadai talaka kwa nguvu zote,
tena kwa kashfa na vurugu.
Mwanamke huyu hatopata faraja ya ndoa huko aendako.,
Talaka itamrudia na kumchapa haswa.

Kuna mwanaume ambaye yeye ndy chanzo cha kuvunjika ndoa,
Na bado anatoa talaka kwa kosa alilofanya yeye.
Huyu mwanaume hatobaki salama huko aendako.
Talaka itamchapa haswa,
Mwishowe kujutia maamuzi ya talaka.

Talaka unatakiwa uitoe ukiwa upo very calm na sio hasira .
Unahitaji umakini Sana kwenye hili.
Talaka inaweza ikawa ndy mwanzo wa kuvurugikiwa maisha yako au mwanzo wa mafanikio,
Inategemea ni Kwa jinsi gani mmeachana.

Ushuhuda
Nilibahatika kuoa mwanamke fulani mrembo sn miaka 17 iliyopita.
Nikiwa bado kijana mdogo sikuwa na kipato kizuri ,
nilikuwa na kipato cha kawaida cha kuunga unga.
Yule binti alinisumbuwa sn sababu ya uzuri wake.

Nilijitahidi kumtunza kwa kadiri ninavyoweza,,
lakini mwisho wa siku alianza visa na kuomba talaka,
Tena kwa vurugu,
kashfa nyingi,
Alikwenda mbali zaidi na kusema mimi sio type yake,
ninamfuja na kumbana bana ili asiolewe na wanaume wenye pesa.

Alilazimisha talaka kwa matusi na kashfa ,
Alikuwa akitoka asubuhi na kurudi jioni tena amelewa na sijuwi pombe amenunuliwa na Nani,
Nikiuliza atajibu kashfa tupu,

"Nilishakwambiya niache na maisha yng wewe unaning'ang'ania nini?"

Aliponambiya maneno haya nilipata uchungu Sana moyoni
Nikiifikiria ndoa yng bado hata mwaka haijafikia,
Sababu nilikuwa na mapenzi mazito Sana kwake ,
nilishindwa kufanya maamuzi ya haraka,
Kwa kweli nilimpenda sn mke wangu.

Nilijitahidi kuwaeleza wazazi wake tatizo,
Lakini kwa majibu aliyonijibu mama mkwe nikagunduwa ,
hata mama mkwe pia hanitaki niishi na binti yake.
Sababu ya kipato changu duni ,,

Yaani mke wangu nimekuoa kwa mahari halafu Leo unambiye hunitaki?
Kwamba siyo type yako?
Hunipendi tena?

Niliitoa talaka kwa uchungu Sana.

Now ni miaka 17 ya talaka lakini still yupo mitaani anahangaika kupata Mwanaume hata wa kuishi nae store hamuoni.,
Hata mtoto wa dawa hana,
Kapauka kama mguu wa Teja.

Tusipende kutoa/ kuomba talaka kama wewe ndy mkosefu.
Jishushe/ omba msamaha maisha ya ndoa yaendelee..

Sent using Jamii Forums mobile app
Duuh ya kweli haya?

Kwahiyo we umeoa na watoto, yy kakosa?
 
Pole sana. Ni kweli kabisa, kama wewe ndio chanzo cha kuvuruga mahusiano yenu mara nyingi utaharibikiwa huko mbeleni. Mimi wa kwangu alipata mchepuko , akawa anarudi asubuhi, akija ukimsemesha anasema bora tuachane. Baadae akahamia huko miezi 3 anasema yuko Msata kwenye shughuli zake, kumbe yuko kwa mchepuko hapa Dar. Bahati nzuri siku nikamuona anapita na gari, kumpigie anasema bado yuko huko. Nikavumilia nikaona huu ni ujinga. Kikaitwa kikao cha familia mara 2 hakutokea. Wazazi wake wakaniambia kwa uliyotueleza una haki ya kuondoka. Nikaanza mchakato wa talaka ndio ikawa hivyo tena. Kuona nimeondoka akapangisha nyumba akahamia kwa mwanamke. Baada ya miezi 6 akafukuzwa kwa mchepuko baada ya hela alizouza gari yangu kuisha. Yupo tu sasa hivi , baba yake kamuambia kama unataka amani ya hii dunia aniombe msamaha maana alifanya dhulma ya wazi. Ila Mungu ni mwema maisha yanasonga
Huyo hawezi kuinuka tena...unless akuombe msamaha wa dhati
 
Ameshaolewa, ila alianza kwanza kuzalishwa nje ya ndoa then jamaa nd kamuoa, after two years akampa talaka lkn wakarejeana so wapo wte na watoto wa 2,na mm pia nmepata watoto wa 2.hatuna mawasliano japo wte tunatoka kijiji kimoja
Nashukuru kwa majibu mazuri, nakushauri kuwa karibu na watoto wako ili sumu za wamama zisikuhairibie.Jitahidi kuwaunganisha watoto wako.Tukionana tutaongea zaidi mkuu.
 
Yaani kwa upendo kwa watoto wako usitoe talaka. Kubalianeni na huyo mke arudi Ila kama mmeshindwa tenganeni vyumba Kwa muda huku mkitafuta Suluhu. Talaka ni mbaya mno. Huyo mtoto wa like ataumia Sana. Unajua mabinti zetu wanatupenda Sana Sisi Baba zao. Please, tulia. Ndoa si lelemama. Tunamshukuru Mungu tumetoka huko na sasa tumezeeshana. Ndoa mwaka wa 1-5 ni Shida, 6-10 umakini zaidi, 11-15 mnazoea kiasi vurugu, 16-20 mnaanza kukomaa, 21-25 unaanza kutua mizigo ikiwemo kusomesha bàadhi ya watoto, 26 plus yaani mnaanza penzi upya maana wote mnakuwa stress free. Hapa hata mwenzio akisafiri utatamani umfuate huko aliko. Hivyo ndoa siyo peremende na lazima mwanaume uwe ngangari.
Nimejaribu nimeshindwa kabisa... Ingewezekana kama mke angekua tayari kujishusha kuliko kuharibu aharibu yeye na ubabe (kiburi) afanye yeye... Kifupi kama kwao watoto wakike kuanzia mama yao ndoa hazidumu mi ni nani niwaweze kudumu nae?
 
Bora kukaa mbali mbali kuliko talaka. Kukeep distance haithiri watoto, upepo ukipita mnaungana tena kwa faida ya watoto. Zipo ndoa zinadumu kwa wawili kuwa mbalimbali.
Madhara ni yale yale... Unadhani watoto hayatowaathiri hayo mazingira?
 
Ukweli ni kuwa hapo palipofikia ni bora na hekima zaidi kila mtu akatafute sehemu inayompa FURAHA na AMANI kwani hakuna na hakutakuwa na mwanaume ataishi na mwanamke mwenye KIBURI||JEURI||na ASIYEKUBALI KUSHINDWA__Na ni mwanamke ndiye awezaye KUITUNZA na KUILINDA NDOA YAKE[emoji848]...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na ndivyo wengi wanafanyiwa lakini bado hawajifunzi.....kuna dada mmoja jirani yangu yeye aliona hawara anafaa zaidi kuliko ata ndugu na watoto ukiachilia mume maana ni mke wa ndoa kabisa, katafuta kwa jasho anajenga kisirisiri eti mumewe asijue hati si akaandika jina la hawara, akanunua gari mnunuzi si jina la hawara, wakati huo kijana Mario hajaoa, amesubiri vimekamilika vizuuuuri kaoa nyumba anaishi yeye na mkewe, gari anatembelea yeye, kiujumla uyu mama amedhulumika kila kitu na biashara imekata saivi anauza mkaa wa mafungu gengeni nyieeeee kila nkimfikiria adi naogopa....usiishi na mtu unamuwazia negative tuuuu hata hajakuonesha ubaya wowote ila we unawaza mabaya tuu ndo hayo yanawakuta
Mbona sheria ya ndoa iko wazi kabisa. Kila mwana ndoa anaweza kumiliki mali zake binafsi. Ni suala la kuwa muwazi tu. Na hakuna kitu kama 50/50 mahakamani. Mimi siwezi eti kuandika majina ya ndugu zangu kwenye mali zangu, kwani wamezitafuta wao. Tatizo binadamu tuna tamaa mtu unaingia kwenye ndoa umemkuta mtu na mali zake halafu unataka ziwe zako.

Kuna dada mmoja kahangaika mahakamani miaka anasubiria mgao, hadi anashindwa kufanya shughuli nyingine. Kosa alilolifanya ni kuwa na boyfriend waziwazi wakiwa wametengana vyumba huku kesi iko mahakamani. Mwisho wa siku hakupata kitu. Sasa hivi kutwa kuongozana na boy friend . Yaani mtu una watoto 3, badala kuwa buzy na wanao unahangaika mtaani.

Kuna mwingine walitengana, mwanamke akahama mkoa. Watoto mpala leo hawajui kinachoendelea, likizo wanaenda kwa mama yao. Mkiwa na watoto ni bora kuangalia maslah yao kwanza maana hata ukiolewa au kuoa kwingine watoto ndio watapata shida. Ni wachache ndio wanabahatika kupata watakao kubaliana kuishi na watoto wa mwenza bika ubaguzi
 
Mbona sheria ya ndoa iko wazi kabisa. Kila mwana ndoa anaweza kumiliki mali zake binafsi. Ni suala la kuwa muwazi tu. Na hakuna kitu kama 50/50 mahakamani. Mimi siwezi eti kuandika majina ya ndugu zangu kwenye mali zangu, kwani wamezitafuta wao. Tatizo binadamu tuna tamaa mtu unaingia kwenye ndoa umemkuta mtu na mali zake halafu unataka ziwe zako. Kuna dada mmoja kahangaika mahakamani miaka anasubiria mgao, hadi anashindwa kufanya shughuli nyingine. Kosa alilolifanya ni kuwa na boyfriend waziwazi wakiwa wametengana vyumba huku kesi iko mahakamani. Mwisho wa siku hakupata kitu. Sasa hivi kutwa kuongozana na boy friend . Yaani mtu una watoto 3, badala kuwa buzy na wanao unahangaika mtaani. Kuna mwingine walitengana, mwanamke akahama mkoa. Watoto mpala leo hawajui kinachoendelea, likizo wanaenda kwa mama yao. Mkiwa na watoto ni bora kuangalia maslah yao kwanza maana hata ukiolewa au kuoa kwingine watoto ndio watapata shida. Ni wachache ndio wanabahatika kupata watakao kubaliana kuishi na watoto wa mwenza bika ubaguzi
Mahakama inaweza kuvunja ndoa ya kikristo?
 
Back
Top Bottom