Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

2013 Dodoma hahahaa nicheke kwanza lol..nilikutana na vibaka wa4 sehemu mbaya sana aiseee siji kusahau mida ya kama saa 4-5 hivi usiku jinsi nilivyonasuka acheni tuu MUNGU aitwe MUNGU ule ni ushuhuda tosha kwangu maana wangeweza kunicheza karata zote na kuiuza roho yangu lakini niliona mkono wa Bwana wa majeshi,. ndipo ninapokumbuka neno la MUNGU lisemalo "adui zako wakikujia kukuangamiza watatawanyika kwa njia saba"...

Kumtumikia MUNGU kuna faida.
 
mkuu ulishirikiana na majambazi. Ila story yako imenichekesha
 
Kawe ukwamani,
Nilikua nipo Jambo Lee na mwanangu mmoja tumekula ugimbi wa kutosha pale, tukahamia La Roca tukala mundende hadi mida ya saa 8 usiku. Yule jamaa yangu alikua anaishi kawe kulekule halafu Yuko tipsy balaa nkaona sio kesi ngoja nimsindikize magetoni kwake (mitaa ya nyuma ya myfair,ccm) mimi nirudi niendelee na cnn. Jamaa nkamfikisha salama lakini kwa taabu saana maana kuna chochoro sio za nchi hii.
Basi wakati narudi, npo kwenye chocho moja mara ghafla naona kwa mbele kundi la mtu kama 7 linakuja wengine Wana nondo, wengine visu, wengine mawe. Mmoja wapo akarusha jiwe nikakwepa, bahati nzuri hua natembea sana nunchuks zangu kiunoni muda wote. Basi nkazichomoa, nkakaa kibadachi stance nikiwasubiri wasogee...........

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hahahaha ameen.
 
Du mnamo Mwaka 2007 jijini Dar kulikuwa na Ujambazi Sana

Siku mmoja tupo na washikaji mtaani tunapiga stori kwenye uwanja wa Mpira ambao upande wake mmoja una Gema/Mmomonyoko wa udongo wenye kina sio chino ya Futi 12-15

Sasa bhana wakati stori zikinoga tukasikia Mlio wa SMG zikamiminwa kama tatu hizi za Mfululizo juu kisha ikasikika sauti mmoja Kaa chini Kumbe bwana Bar iliyomita chache sana na uwanja ilikuwa imevamiwa

Yaliyojiri sasa

Sisi tuliokuwa tumekaa uwanjani tukapata na mfazaiko mkubwa maana Risasi zilipigwa kama mita 7 kutoka sisi tulipokuwa tumekaa ghafla tukakimbilia kwenye Gema lenye futi sio chini ya 12 tukajirusha kwaajili ya kunusuru Maisha yetu

tulivyofika chini halo ya kuwa tumeseleleka sana kwenye hayo maporomoko ngozi zetu zikawa zimechubuka chubuka kufika chini tukambia mbio ilipofika kesho yake kila mtu alishindwa kutembea kutokana na maumivu na michubuko na vidonda tulivyovipata!!!

Shughuli ilikuwa pale Bar sasa jamaa mmoja katika Yale majambazi akawa anapita na kiroba /salfeti akikusanya Fedha, Simu, pochi na vitu vingine vya thamani

Sasa bwana wakafika ktk meza ya mama mmoja wa Kichaga yeye na bwana wake wakagoma kutoa hela na simu jamaa wakaamua kuanza kumkata Vidole bwana wake kimoja baada chengine akakatwa vidole viwili fasta akatoa wallet na simu

mama wakichaga naye akapigwa na mapanga kichwani wakamuumiza sana akawa anavuja damu nyingi sana tukawa tumepata funzo kuwa wazee wakazi wakikutait kubali tu kuwapa kama ni pesa au simu

Aisee sito sahau


Sent using Jamii Forums mobile app
 
hahahaha malizia
 
Nshoo Nshooo Nshoomiileeee.
 
daaaah yaani hadi uumizwe ndio utoe kitu? wachaga bhanaa wabahiri sanaa.
 
Stori ndio ishaisha hapo au kuna muendelezo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbeya barabara ya kwenda chunya miaka ya nyuma maeneo ya kona za mkoa kabla barabara haijafanyiwa ukarabati, majambazi walikua wanatega magogo barabarani halafu wao wanajificha, ilikua haiwezekani gari kupishana kwenye eneo hilo mpaka mpigiane simu kua nani atakaeanza kupita pale hata kurudi rivasi ilikua sio rahisi na ukicheki chini kuna bonde la usangu hapa kitonga ikasome

Kwa mazingira hayo ukitumia mbinu ya huyo jamaa ya kushuka kwenye gari ni ngumu kupona maana watajua kua umejipanga kupambana nao, hivyo unaweza ukapigwa shaba ukiwa huko huko mbali kabla hujawakaribia

Sent using unknown device
 
Daah bahati umeifanya kuwa muujiza aisee

Sent using unknown device
 
Picha imeisha hata popcorn haijaisha
Sent using unknown device
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…