Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Walimuua???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unakaa porini mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakichukua hela???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmmh hatari sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 98 nikiwa kijijini nikaamua kwenda kusalimia kwa ndugu wa karibu mbali kidogo na nilipokuwa. Huko niliwahi kwenda na wazazi zamani hivyo sikuwa napakumbuka vizuri. Nikafika kwenye kamji mida ya usiku wa saa 4 hivi na enzi hizo hakuna bodaboda na usafiri tegemeo ni lift za watu wa misheni. Kwavile mwendo wa kufika kule kutoka kwenye hako kamji ni kama 1 hr nikaona nitembee tu nikalae huko. Wenyeji pale wakanishauri nichukue gesti nilale maana kuna ujambazi wa kutisha na hasa kuna kundi la majambazi wakiongozwa na mtu anayeitwa Mwamba ni hatari ukikutana nao. Huyo Mwamba unaambiwa akitaka hela anakuja anakutaarifu hadi sehemu ya kumuwekea aje achukue mwenyewe. Ile kibishi na umjini nikawaambia nitatembea bado mapema. Mdogo mdogo after kama 25 min kwenye kimteremko giza nene na misitu nikaona mtu anatembea kuja nilipo, sikuhofu wazo likaja nimuulizie wenyeji wangu ili nijekupitiliza. Alivyofika nikasalimia nikamuuliza bahati nzuri anawafahamu akasema umefika twende nikupeleke. Hatua kadhaa akaniambia lete mzigo nikusaidie nikashukuru na kuanza kujiongelesha nikamwambia nasikia huku kuna jamaa anaitwa mwamba anaogopwa kijiji kizima kuwa ni mtu hatari, na jinsi watu walivyoshauri nilale town niondoke asubuhi nijekukutana nae. Basi najiongelesha njemba inatembea tu sigara mdomoni. Baada ya mwendo kidogo tukafika kwa wenyeji wangu nikagonga mlango. Mtu wa kwanza kufungua mlango na kutuona alitoka nduki na kushtua wengine kwa kile kishindo ikabidi waje mlangoni kutuona wote wakawa wanatetemeka huku wanatukaribisha. Nikashangaa ile hali ya wenyeji wangu alafu ile njemba ikaaga ikaondoka zake. Ndugu zangu wakaanza kunihoji unajua umekuja na nani, huyo ni kiongozi wa majambazi maarufu kwa jina la Mwamba! Dah, nywele zilisimama hasa nikumbuka nilivyokuwa nikipiga nae stori. Dah kila nikumbuka nacheka sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hahahahaha unabahat sanaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Gahawa bila kaandazi inachoma kooo
 
aisee Mungu akubariki sanaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…