Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Wakato nasoma ile likizo narudi dar kutoka mbeya..
Nikapanda magari ya wafanyabiashara wanaoemda kufunga mizingo yanaondoka mbeya saa10 jioni na kufika dar asubuhi saa11..kabla hatujaingia morogoro kuna tulikuta jamaa wamemwaga ulezi na maganda ya ndizi gari ili sleep sana watu konda akasema ficheni mali zetu tunatekwa..
Mbele kidogo wametandaza sijui ni mbao zile zinamisumali dereva alijaribu kutaka kurudi nyuma ikapigwa shaba kwenye tairi na taa moja ya mbele,gari ikasimama dakika o zinatoka njemba porini zimeshiba wamevaa mask wameshika bunduki,wakatoa amri kila mtu atoke kwenye gari akiwa na boxer kwa wanaume na wamama watoke na chupi na sidiria tu huku majambazi wengine wamelizunguka gari wengine wameshaingia kwenye gari..hapo dereva ameshakula kichapo cha mbwa mwizi kwanini alitaka kurudisha gari nyuma.
Unavyotoka nguo unaacha kwenye gari unasachiwa kwenye boxer na wamama wanasachiwa kwenye matiti na kwenye chupi ukishasachiwa tu unapigwa mkanda wa mgongoni ulale chini,
Kuna mshua mwingine alitaka kuwavimbia alikua na bastora wakamuwahi aisee alipigwa sana hadi kuvunjwa mkono wake jamaa wana roho mbaya sana
Baada ya lile zoezi kuna majambazi wengine wakawa wanapakia vile vitu kwenye gari lao wengine wanapekua kwenye siti za gari wanazichana chana na visu kama mtua!eficha pesa au simu kwenye siti ya gari..tumelala pale tunakuja kumashwa na madereva wengine wapita njia majambazi wameshaondoka. Tukaenda police kutoa taarifa wachache walipata msaada wa makoti na vikoi wengine tulishuka pale kidongo chekundu tukiwa na boxer na wamama wengine wakiwa na chupi wafanyabiashara wa pale kidongo chekundu walitununulia nguo na kutupa nauli.
Kwa hesabu za haraka hili tukio walilifanya halikuzidi dakika15
Ilikuwa usiku???hakuna mwanamke aliyebakwa???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haaaahaaaa[emoji28][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].....aki nimecheka kama mwehuu

[emoji1787][emoji28][emoji28][emoji119][emoji119][emoji119]

Sent using Jamii Forums mobile app
Cheka tu mama usiombeee uyakwaee
 
Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo nikiwa shule O-level ilikua boarding.
Siku hiyo ilikua week end tukatoroka shule kwenda mitaani kuinjoy, kula vitu adimu na kutafuta mademu.
Basi bhana tulikua wanne tumeenda mitaani tumefanya kila kitu mpaka mida ya saa tatu hivi usiku( ilikua ni kijisehemu kimechangamka sana, CENTER)
Wakati tunajiandaa kuanza safari ya kurudi shule mara ghafra wazee wa kazi wakavamia pale kwenye maduka, basi bwana purukushani za hapa na pale kila mtu akatoka nduki.
Wengi tulikimbilia makaburini coz hayakua mbali halafu ndo sehemu iliyokua walau mtu unaweza kujificha.
Basi bwana tumejificha kwenye makaburi wazee wa kazi wakaendelea kukiwasha duka baada ya duka, kati ya hayo maduka kulikua na frem ya salon na kuna wateja walikua wananyolewa(baada ya kuvamia jamaa walizima taa wakawa kimyaaa) basi majambazi si yakafungua mlango wa salon,hahahahaaaa!
Alitoka mshkaji mmoja amenyolewa upande na shuka jeupe shingoni nduki ya ajabu sana kama mshale, jamaa nae akakimbilia uelekeo wa makaburini, ile kufika akatukurupua( maana alikua nduki mbaya halafu anakimbia juu ya misalaba huku shuka linapepea kwa nyuma) kuona vile group lote tuliojificha tukadhani jamaa alikua kafufuka basi tulitoka nduki kumkimbia, na yeye kuona tunakimbia akadhani nyuma kuna jambazi linamkimbiza akaongeza spidi kutufuata, jamani jamani ilikua mshike mshike wa hatari, tulikimbia kama wendawazimu,.
Huku nyuma majambazi yameshaondoka sie tunakimbizana na jamaa. Tulijikwaruza sana kwenye vichaka pamoja na kuanguka kwenye makaburi, tuliumia sana.


Sent from my iPhone using JamiiForums
Hahahahaaaaaaa katika visa vyote hii funga kazi dah!!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani hii kama iliyotutokea sisi...sema mm walimnyanyua mtoto na mkono mmoja panga shingoni, mm nililia nkiwaambia mtaniulia mtoto bure ela sina naomba mchukue chochote ktakachowafaa ...bas akamuachia
Mwanangu mpaka leo anakumbuka..

Alafu nimekuwa mtu wa kuota ota usiku na kukurupuka kupiga kelele bila sababu , naweza nikasikia ata pikipik ucku mi nakurupuka na kelele najua n mwizi,

Hili tukio halinitoki kichwani kabsa

Sent using Jamii Forums mobile app
Duh Pole sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilihisi kuna mtu wa benki alinichoma, maana hakuna mtu aliyekua anajua naenda kuchukua hela pale.. Kuna jamaa zangu ni mabaka mabaka na mapolisi nikawaelezea nilivyoporwa... Wakaniambia tuandae mtego..

Baada ya wiki tatu nikarudi benki ileile kuchukua pesa.. Kweli bhana wale washenzi wakajilengesha, bila kujua 40 ndio zimefika.. Watatu walikufa palepale baada ya kupigwa risasi, wawili walikuja kufa baadae baada ya kutaja hela zinapokwenda... Hela walizochukua zilirudi na fidia juu...

Cc: Duke tuchaz, rikiboy...
Hawakuwataja waliowachoma bank????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha haya hatari sana..NAKUMBUKA MIAKA YA NYUMA BAADA YA KUMALIZA CHUO sina kazi yoyote nikawaza ntafanya kazi gani..Akili ikanijia nitafute kazi yoyote sasa ntafanyaje kazi yoyote na ninaona aibu mkoa huu huu nisome tangu primary,secondary,chuo LEO nianze kufanya kazi za ajabu?? HAPANA..

Basi nikaenda mwanza huko simjui Ndugu wala mtu yeyote yule nikasema kazi yyte huku nafanya hata ya kuzibua choo tena hivi sijulikani ndo poa kbsa,nakumbuka siku ya kwanza nilifika usiku palipokucha tuu Nikaanza kazi ya kutafuta kazi BAHATI YANGU mbaya mtu wa kwanza niliyemuuliza kuhusu KAZI ntapata wapi (Alikua kibaka/mwizi) akanambia unatafuta kazi gani nikamwambia yeyote ile mi nafanya.

Akaniuliza hata kuosha vyombo au u house boy? nikamwambia Braza namaanisha nikisema yeyote hata ya Kubembeleza mtoto mi sawa tu,Akanambia kuna mama wa kihindi yupo anatafuta house boy twende nikupeleke,basi nikaanza kumshukuru kabla hata hatujafika tukiwa njiani jamaa akawa ananipa maushauri hayooo, ma pointi kama yotee Na aliponifanya nimwamini zaidi ni alinambia natakiwa kua MWAMINIFU ktk kazi za watu maana nikiharibu LAWAMA atapewa yeye.

Nikamuahidi ntakua mwaminifu basi tukaendelea kwenda CHocho to chocho..road to road mara tuvuke mito mara madimbwi baadae tulitokelezea mtaaa uchochoro flani hvi hata ukipiga Mayoweee haskiii mtu Nilishangaaa wametokea wenzake kama watatu jamaa akkajiunga na wenzake wakantolea mapanga bwana walinichojoa kila kituuuuu..Niliachwa na BOXAA tuuu.

Sitokaa niisahau hyo siku na maishani mwangu mwote tangu siku hiyo SIAMINI MTU tenaaa
hahahahahahahahahahahaha
 
Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo nikiwa shule O-level ilikua boarding.
Siku hiyo ilikua week end tukatoroka shule kwenda mitaani kuinjoy, kula vitu adimu na kutafuta mademu.
Basi bhana tulikua wanne tumeenda mitaani tumefanya kila kitu mpaka mida ya saa tatu hivi usiku( ilikua ni kijisehemu kimechangamka sana, CENTER)
Wakati tunajiandaa kuanza safari ya kurudi shule mara ghafra wazee wa kazi wakavamia pale kwenye maduka, basi bwana purukushani za hapa na pale kila mtu akatoka nduki.
Wengi tulikimbilia makaburini coz hayakua mbali halafu ndo sehemu iliyokua walau mtu unaweza kujificha.
Basi bwana tumejificha kwenye makaburi wazee wa kazi wakaendelea kukiwasha duka baada ya duka, kati ya hayo maduka kulikua na frem ya salon na kuna wateja walikua wananyolewa(baada ya kuvamia jamaa walizima taa wakawa kimyaaa) basi majambazi si yakafungua mlango wa salon,hahahahaaaa!
Alitoka mshkaji mmoja amenyolewa upande na shuka jeupe shingoni nduki ya ajabu sana kama mshale, jamaa nae akakimbilia uelekeo wa makaburini, ile kufika akatukurupua( maana alikua nduki mbaya halafu anakimbia juu ya misalaba huku shuka linapepea kwa nyuma) kuona vile group lote tuliojificha tukadhani jamaa alikua kafufuka basi tulitoka nduki kumkimbia, na yeye kuona tunakimbia akadhani nyuma kuna jambazi linamkimbiza akaongeza spidi kutufuata, jamani jamani ilikua mshike mshike wa hatari, tulikimbia kama wendawazimu,.
Huku nyuma majambazi yameshaondoka sie tunakimbizana na jamaa. Tulijikwaruza sana kwenye vichaka pamoja na kuanguka kwenye makaburi, tuliumia sana.


Sent from my iPhone using JamiiForums
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Nmecheka sana mkuu
Kula like

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Awa wazee wetu walinzi wanapata masaibu sana.....mzee mmoja alikuwa analinda Mjini mahali kuna frame nyingi ila yeye analinda Moja Tu.

Majambazi wamekuja target ni kuiba frame yake anayolinda maana nyingine hazina walinzi, wakamtanguliza mmoja wao,jamaa akaenda akaanza kupiga stori na babu akamwambia kuna fuso anasubiri lipo njiani aje kushusha mzigo Wa dukani.

Badaye kidogo jamaa akamwambia anasikia njaa ngoja akacheki chips,Mzee machale yakamcheza lakini jamaa alivyorudi karudi na chips package 1 Tu kwani babu alihisi jamaa atarudi na package 2 na lazima atakuwa amemuekea madawa humo.kwa hiyo mzee akarelax.Jamaa akaendelea kula huku stori zikiendelea kisha akamkaribisha mzee kuku tu kwa maana kulikuwa na vipande viwili katika package 1 na hiyo ikampa matumaini mzee kuwa kile kipande hakiwezi kuwa na madawa.mzee akatafuna kuku na kupoteza fahamu palepale jamaa akaita wenzie sasa kumbe haya mageti sijui ya bati ya kwenye frame za maduka kumbe yanautaalamu wake wa kuyafungua bila shuruti kama ni mjuzi nayo.Jamaa wakafungua wanavyojua wao na kuhamisha mzigo wote dukani duka LA electronics alafu wakarudishia mlango wakasepa wakamuacha babu kalala.
Babu kuzinduka akajisachi akajikuta kama alivyo na asubui kafanya usafi kasepa Zake.
Mwenye duka anakuja fungua duka haamini anachokiona,ikabidi ampigie simu babu,babu kuja pale na yeye eti anashangaa.

Ikabidi mshikaji amkomalie babu asimulie mazingira ya usiku yalikuwaje.....babu kasimulia lakini anajitetea mbona kuku nliokula kamtoa mulemule alipokua anakula yeye.

Sent from my H8402 using JamiiForums mobile app
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
story yetu ilikua ya Kuhusu kukutana na majambazi...Anzisha THREAD itayonfanya nije na Muendelezo mkuuu😛😛
haya bana, nilikua nnawaza tuu ulivyorudi kwenye zile chocho kwa chocho na nguo mpya.
Pole sana mkuu.
 
2013 Dodoma hahahaa nicheke kwanza lol..nilikutana na vibaka wa4 sehemu mbaya sana aiseee siji kusahau mida ya kama saa 4-5 hivi usiku jinsi nilivyonasuka acheni tuu MUNGU aitwe MUNGU ule ni ushuhuda tosha kwangu maana wangeweza kunicheza karata zote na kuiuza roho yangu lakini niliona mkono wa Bwana wa majeshi,. ndipo ninapokumbuka neno la MUNGU lisemalo "adui zako wakikujia kukuangamiza watatawanyika kwa njia saba"...

Kumtumikia MUNGU kuna faida.
Walikuacha vipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi wakatimwingine nipo form 4 nilikua nakaba na kuchukua hell kunasiku nilimkaba babaake na rafikiyangu ananijua vizuri sababu nilitokea nyuma hakuniona nikaona Bora nimalize kabisa yani niuwe nilikaba mpaka akalegea nikajua tayari nimeua kumbe kazimia
[emoji1] [emoji1] [emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2012
Joka ndio nilikuwa moto kwa watoto warembo nikiwa kidato cha sita huko Kilimanjaro.

Nilitoka na manzi mmoja mkali mtoto wa Kigogo wa Chuo cha Polisi pale Moshi. Rafiki zangu walinionya kuwa niachane na Shani lakini Joka nilikuwa nimeshakolea.

Dogo alikuwa Mawenzi kidato cha tano Boarding. Kila ijumaa alikuwa akija Ghetto Na kurudi Jumapili. Kama unavyojua ujana basi nikawa najiona bonge la mjanja nikiwaoshea Washikaji. Manzi alikuwa amesimama haswa.

Siku moja tuliamua kwenda Waterfall ya Marangu. Na hapo ndipo nilipoonja Joto ya jiwe. Tuliondoka pale mjini mimi Na Shani. Tukafika Marangu Mtoni. Tukashuka. Tukaenda kuchukua Room kwenye hotel ya Kill Hotel kama unaenda kupanda Mlima Kilimanjaro kule.

Hao tukatoka. Tukachukua boda boda mpaka Waterfall ya Marangu. Ilikuwa mida ya jioni watu walikuwa wachache kama kumi na tano hivi.

Tukasaura nguo watu ndani. Punde walikuja washikaji wanne vijeba haswa. wakawaweka chini ya Ulinzi Wale waliokuwa nje ya maji. Walitoa Bastola na kutoa amri ya sisi kutoka ndani ya maji.

Nilikuwa mbishi. wakapiga Risasi moja juu ndipo nikaona hapa hawatanii. Tukatoka Mimi na Shani. Nilipigwa mitama nikahisi kiuno kimevunjika. Shani alipiga makelele tuu. Walipoona Shani anazidisha Kelele walimzaba Kofi akapoteza fahamu hali iliyonifanya nidhani Amekufa. Niliwabwatukia nikitumia nguvu kumfuata aliyempiga Shani. Ghafla nilihisi kitu kizito kichwani na papo hapo nilipoteza fahamu.

Nilikuja kuzinduka Asubuhi nikiwa kando ya Mto Karanga. Nikiwa sina nguvu kabisa.

Sitokuja kisahau. Mapenzi yaacheni tuu
 
Back
Top Bottom