Mwaka sitautaja. Saa tano usiku nimeshuka bus la kiwanda cha ALAF njia panda Mwananyamala naelekea Kinondoni B. Dereva kagoma kunipeleka hadi pale mitambo ya umeme Bagamoyo road, bus likaelekea Mwananyamala. Nilitembea kama dakika kumi mita ishirini mbele vibaka watatu wametanda barabarani. Sina kitu mkononi lakini muguuni nimevaa buti nzito za kiwandani. Nilipata mstuko, uchaguzi wa kurudi nyuma au kukimbia haukuwa sahihi, maana ingekuwa rahisi kwao kunifikia. Kwa haraka niligundua tunalingana vimo, na hapo ni miezi minne tangu nimalize mwaka mmoja wa JKT kwa mujibu wa sheria, nikajesemea moyoni ntakufanao. Nilichofanya ni kuongeza kasi ya kuwafikia na kukita buti kwa nguvu, mikono kama nacheza paredi.
Plan yangu ilikuwa atakaenisemesha ni kumpa pigo la kuzirai, atakae nishika ni kumtoa nyama kwa meno. Nilipo wakaribia niliwasikia wakisema he mtu mwenyewe kama askari walinipisha bila neno lolote. Hata hivyo, kasi ya mapigo ya moyo ilikuwa juu sana, sijui pangetokea nini kama wange anza vurugu.