Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Duhhh...
Pole sana mkuu.
Pale Mecco, vijana wengi wazee wao walijiweza miaka ya nyuma na wakajenga majumba makubwa na mazuri miaka ile kabla ya ule mtaro kujazwa na taka na kuiunganisha Kangae.
Mbaya zaidi, vijana wengi wa maeneo yale wali acha kusoma na kuendekeza urahabu kwa jeuri ya pesa za baba zao hadi wakajisahau kwamba wazee wao wamesha choka na pesa zimewaishia na nyumba zao zilisha kuwa chakavu.
Mwisho wa siku vijana wamebaki kuwa wezi, vibaka na wakabaji tupu.
Nakumbuka marehem Masubo aliwahi kuwacharanga vijana flani na beto pale Cheers

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hiyo mitaa ya buzuruga, memo, had I national vijana wezi sana. Mimi mwaka Jana mitaa niliyokuwa naishi national nyuma ya comfort hotel walinipulizia dawa wakaiba flat screen,jiko, nguo na via zangu kwenye nlishtuka SAA 3 asubuhi. Hata job nilishindwa kwenda sumu Kali sana ile.
Lakini miaka 25 iliyo pita, hiyo ndio ilikuwa mitaa ya wastaarabu na watu walio jiweza kimaisha, yaani hapa namaanisha Barnaba, Buzuruga, Nundu, Mecco, Nyakato sokoni na Neshono
 
Duhhh...
Pole sana mkuu.
Pale Mecco, vijana wengi wazee wao walijiweza miaka ya nyuma na wakajenga majumba makubwa na mazuri miaka ile kabla ya ule mtaro kujazwa na taka na kuiunganisha Kangae.
Mbaya zaidi, vijana wengi wa maeneo yale wali acha kusoma na kuendekeza urahabu kwa jeuri ya pesa za baba zao hadi wakajisahau kwamba wazee wao wamesha choka na pesa zimewaishia na nyumba zao zilisha kuwa chakavu.
Mwisho wa siku vijana wamebaki kuwa wezi, vibaka na wakabaji tupu.
Nakumbuka marehem Masubo aliwahi kuwacharanga vijana flani na beto pale Cheers

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu u mwenyeji sana huko eeeh dah kitambo hicho ilikua mitaa yetu nyakato, mecco, buzuruga, mha’ndu, gedeli n.k
 
ilikuwa ni majira ya usiku mnene miaka ya 99 nikiwa mdogo katika mji wa tarime
mvua ikiwa ya rasharasha ikipiga mara vishindo vikali vya kuvunjwa ukuta vinasikika kila mtu anatahamaki ni kitu gani hicho
kuchakata akili kumbe ni majambazi yanatumia jiwe la fatuma kuvunja geti pamoja na ukuta
kulikuwa na frem ya duka pembeni ya ukuta mangi akaanza kupiga yowe wale jamaa wakamwambia atulie kama uji otherwise wakiingia wanaanza na yeye

usiku nikamuona mzee wangu kaamka kabeba upinde na mkuki
akawaamsha wanaume wawili wakaenda hadi getini kusubiri majambazi wavunje waingie wale nao sahani moja asee wale majambazi hawakutarajia ambush ile ile fatuma imedondosha geti tu wanakutana na mvua za mishale na mikuki hahaha
hawakutarajia iyo ambush
mzee wangu alikuwa shujaa sana r.i.p
 
Huu ni uongo tosha
Majambazi hawana muda wa kujibishana na wewe. Eti hela nimepitisha kazini

Majambazi hujawahi kutana nao.

Umesema uliwekwa uvunguni, akaletwa na HG naye uvunguni...
Baadae unasema Mdogo wako aliwekwa chooni na HG

Mkeo hujasema alikuwa wapi

Majambazi hawama sababu ya kurusha risasi kama hakuna kilichotokea nje ya eneo la wizi.

Majambazi sio wajinga una bastola wakuachie wakiwa wanaondoka.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hiyo mitaa ya buzuruga, memo, had I national vijana wezi sana. Mimi mwaka Jana mitaa niliyokuwa naishi national nyuma ya comfort hotel walinipulizia dawa wakaiba flat screen,jiko, nguo na via zangu kwenye nlishtuka SAA 3 asubuhi. Hata job nilishindwa kwenda sumu Kali sana ile.

Pole mkuu.
 
Pongezi nazipeleka kwa walinzi wetu(polisi) kwa kuweza kufanikisha upelelezi ambao ulizaa matunda, na kuwakamata wahusika wote.

Ila mkuu vipi hiyo bastola yako ilibaki salama!!!

5/5

Ndio mkuu hawakuiona

Pona yangu niliwapa ushirikiano mkubwa .
 
Duh jamaa Alitaka kumla shem kimasihara!?
Sio experience nzuri Kukutana nayo, pole Sana, ila ilitakiwa ujue walijuaje una hizo fedha, lazima kuna sehemu ulifanya nazo show off wakaziona thus why walikadilia kuwa ni more than 5 million.

Cassino mzee
 
Duh aisee Pole sana. Majambazi na vibaka walaaniwe kwakweli.

Ila pesa zako ulizipata?

Na unahisi ni nani aliye kuwa anajua kwamba una kiasi hicho cha pesa.... Maana huyo ndie atakae kuwa mhusika no moja

Sent using Jamii Forums mobile app

Baada ya kukamatwa kuna jamaa yangu ndio alionekana pesa ilitumwa kwake


Alikua na duka la simu mitaa ya dampo/ngokozi ndio mfadhili wao alikua

Ni jamaa tunaejua fika.
 
Back
Top Bottom