Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Hahahahaha JKT Oyeeeeeeeh
 
Hahahaha ulijiongeza sana mkuu.
Ungetembea kilainilaini ungechezea mabapa Hadi basi.
 
Mimi nilikuta mifuko ya suruali iko nje kwamaana kama ningekuwa na pesa wangesepa nayo
 
Mi nilikutana na kibaka mchana wa saa sita anafukuzwa...mkononi kashikilia chupa tupu ya bia...alipokaribia akaishika vizuri mkononi...mmmh mbona nilimpisha njia!
 
[emoji23]
Mstari gani unaotofautisha jambazi na kibaka. Afanyacho kibaka ni sehemu ya ujambazi, maana kibaka anaweza kukwapua, kupora, kupiga, kuuwa, n.k

MTU akikwapua Sh. 1,000 hutasita kumuita jambazi, akikwapua Sh. 100,000,000 ni rahisi kumwita ni jambazi.
 
Hii naweza kuchangia na mimi.

Mwaka 2016, nilikua nakaa Karibu na Kiwanda cha Azam Juice kule Kongowe (ya Mbagala) Hafu mbele kidogo.

Basi siku iyo natoka job Ubungo sina nauli ya kutosha. Nina kama Buku tu. Nilipofika Mbagala nina chini ya mia 4, kumbe kuna gari pale za moja kwa moja hadi Kule vikindu ila me sizijui kwakua mgeni so napanda hadi Kongowe hafu nikifika pale napanda gari jingine. Ila kwakua siku iyo sikua na hela nikapanda hadi Kongowe hafu pale nikaanza kutembea. Ilikua kama saa 5 usiku hivi.

Mbele kidogo kuna sheli mkono wa kushoto, na shule ya sekondari. Nafika pale, kuna bodaboda ikaja wamepakizana jamaa watatu. Eti wananiuliza uwanja wa mpira upo wapi. USiku saa 5 uwanjani wakafanye nn. Kwakua mgeni nikawaambia upo uko (nikapoint uelekeo wa Kongowe ili waende huko). Me nikaendelea na safari. Nageuka wajamaa wakazuga wanaenda wakageuza tena hafu wakazima taa ya Bodaboda. Wawili wakashuka sijui wameshika kama panga au fimbo au gongo hivi ilikua giza. Duh, hapo nilikua usawa wa shule, aisee niliparamia ukuta wa ile shule nikaingia ndani, nikalala chini uku naita walinzi. Walinzi wakaha wakaniuliza uliza maswali wakachukua ID nikawapa namba kama za watu wanne wakawapigia wakaprove aisee.

Dah nililala darasani humo shuleni hadi asubuhi. Aisee usiku mrefu. Ila kukakucha aisee.
 
😂😂😂😂😂Nakufaaaa
 
Hahahaha walivyo wengi ungepigika tu.
 
Huu uzi maisha yake mengi huwa mida hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…