Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Dah pole sana hao wapuuzi wanakera sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namshukuru Mungu sijawahi kupigwa tukio ila hawa watu wanaoitwa majambazi ni wakulaaniwa,eneo nakofanyia shughuli zangu kuna siku niliona wakimpora mtu aisee wale jamaa ni wanyama maana walimwambia awape bag ila yeye akawa kama hajawaelewa na ni mtaa wenye pilika za watu nadhani ile kuogopa raia kushtuka wakamchapa jamaa risasi ya kiuno wakampora kisha wakatembea.

Ile picha jamaa alivyokuwa analia kwa maumivu makali na uchungu wakuibiwa ilikuwa inajirudia rudia kichwani karibia miezi mitano.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Nimesomaaa kwa kuogopaaaaa mnooooo uwiiiiiii[emoji119]mm majambazi wakiingia watakuta nimeshajifia kwa presha[emoji22]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri,kipindi cha mvua ni kipindi cha kuwa makini sana,wezi/majambazi hutumia mwanya wa hali ya hewa kutekeleza yao
 

Sema kosa alifanya ni kusahau nyumbani ..haikutarajiwa kukutwa vile mahali aliko toka
 
Mkuu umemtaja marehem MASUBO umenikumbusha mbali sana asee! MUNGU amlaze mahali pema
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanikute kwani umesikia mimi ni kibaka au mwizi?

Mdogo wangu, I have my own life, nina kazi yangu nzuri ya kusukuma mkokoteni na kuzoa taka inanilipa vizuri, naishi vizuri.
Jamaa kauliza Wewe ni mtinduaji na umejitangaza sasa Hao majambazi wakikukuta wewe wakufanyaje licha ya kukupora?
 
Da nakumbuka mwaka 1999 ....nikiwa na mama wadogo zangu wawili walisafiri kwenda kijijini mi niligoma nikabaki na mama

Mama alikuwa kaajiriwa duka moja la tajiri kuuza sement....!! Katika biashara siku moja aliuza sement kama za Milion 9 ...kutokama na MEM ilikuwa imepamba moto

Wakati akitoka dukani kuna watu walikuwa wanamfatilia kwa nyuma bila kujua alipofika zile hela akanipa mimi zikiwa kwenye jagi ...la maji likuwa tupu nikachukua kama natoka kwenda kununua kitu dukani nikazipeleka zile hela mpk kwa tajiri yake mama ...

Maana ilikuwa desturi kunituma mm mida ya saa moja na nusu nilifika akahesabu akaniandikia kitabu cha risiti cha kupeka hela nikarudi

Tukalal mm nikuwa nalala sebleni ...mama alikuwa nalala chumbani. ..mida ya saa saba usiku nikasikia mlango ukipigwa kwa nguvu !! ...aise na nilikuwa bado chali mdogo nikiwa darasa la V

Mlango ulipasuka mbao zikaachia watu kama nane waliingia ndani , ......wakapitiliza mpk chumbani kwa mama !!

Wakaanza kumuomba hela huku wanampiga kichwani ubavuni.......!! Mama alilamika sana akawa anawaambia mbn sina hela nimezipeleka kwa tajiri yangu

Mwingine kwa nje akawa anasema kama hela muueni ...sauti yake niliitambua alikuwa ni polisi ....kabisa tena jirani yetu !! Nyumba km ya tano ..


Nilishikwa na uchungu nikarusha taa ya chemri ilikuwa karibu na kitanda nilipigwa risasi mkono !! Nilianguka chini kutokana na damu nyingi kutoka nilizima kabisa

Yaani walichoambulia ni laki mbili tu !! Ila walimpiga sana mama na walijua wamemuacha wamemua pamoja na mm

Nilikuja kushituka mchana tokea saa sita mchana nipo hospital watu wamenijalia ndugu ...muda huo nilikuwa nimewekewa damu katika mshipa wa mguuni na kwenye mkono wa kushoto

Yaani nilivyoomuona mama alikuwa amevimba mpk nilimsahau .....alipona , japo kuna ukilema walimuachia

Na mm nilipona ila mkono ulibaki na kovu kubwa yaani huwa nikiangalia mkono napata uchungu kabisa na majambazi na vibaka

Yaani nikikamata naua kabisa kama kesi nitaikuta ....mahakamani!!
Yaani nawachukia sana na kamwe siitakuja kusahau tukio lile ...japo majuzi juzi nilivamiwa tena ila niliwazidi nguvu






sent from toyota Allex
 

Kama hujawahi kukutana na hizi harakati za hawa jamaa huwezi kuiamini hii story.

Mimi kisa changu sitakiandika, ila jamaa wa kumi nje kumi ndani walishanitembelea.

Story haipishani sana na ya jamaa.
 

Polee sana mkuu, japo hii picha ni ya Mguu na sio Mkono, vile vile ni ya Kudownload.
 

Pole sana
 
Chai umeipika vizuri ila hapo uliposema walianza kufyatua risasi nje ndio umetia magadi kwenye chai, kitu cha mwisho ambacho jambazi hakitaki ni kuleta attention za majiranj kwenye tukio
Unabisha ww ndiye ulikuwa jambazi ? Wakati nilipigwa risasi mkono !!! Au unabwabwaja mdomo usichache

sent from toyota Allex
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…