Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Unabisha ww ndiye ulikuwa jambazi ? Wakati nilipigwa risasi mkono !!! Au unabwabwaja mdomo usichache

sent from toyota Allex
Sio wewe ni Huyu muanzisha thread namnukuu "Wakawekwa chooni wakafungiwa huko na beki 3 huko nje wanapiga risasi hovyo, zinaaunguruma balaa."
 
Da nakumbuka mwaka 1999 ....nikiwa na mama wadogo zangu wawili walisafiri kwenda kijijini mi niligoma nikabaki na mama

Mama alikuwa kaajiriwa duka moja la tajiri kuuza sement....!! Katika biashara siku moja aliuza sement kama za Milion 9 ...kutokama na MEM ilikuwa imepamba moto

Wakati akitoka dukani kuna watu walikuwa wanamfatilia kwa nyuma bila kujua alipofika zile hela akanipa mimi zikiwa kwenye jagi ...la maji likuwa tupu nikachukua kama natoka kwenda kununua kitu dukani nikazipeleka zile hela mpk kwa tajiri yake mama ...

Maana ilikuwa desturi kunituma mm mida ya saa moja na nusu nilifika akahesabu akaniandikia kitabu cha risiti cha kupeka hela nikarudi

Tukalal mm nikuwa nalala sebleni ...mama alikuwa nalala chumbani. ..mida ya saa saba usiku nikasikia mlango ukipigwa kwa nguvu !! ...aise na nilikuwa bado chali mdogo nikiwa darasa la V

Mlango ulipasuka mbao zikaachia watu kama nane waliingia ndani , ......wakapitiliza mpk chumbani kwa mama !!

Wakaanza kumuomba hela huku wanampiga kichwani ubavuni.......!! Mama alilamika sana akawa anawaambia mbn sina hela nimezipeleka kwa tajiri yangu

Mwingine kwa nje akawa anasema kama hela muueni ...sauti yake niliitambua alikuwa ni polisi ....kabisa tena jirani yetu !! Nyumba km ya tano ..


Nilishikwa na uchungu nikarusha taa ya chemri ilikuwa karibu na kitanda nilipigwa risasi mkono !! Nilianguka chini kutokana na damu nyingi kutoka nilizima kabisa

Yaani walichoambulia ni laki mbili tu !! Ila walimpiga sana mama na walijua wamemuacha wamemua pamoja na mm

Nilikuja kushituka mchana tokea saa sita mchana nipo hospital watu wamenijalia ndugu ...muda huo nilikuwa nimewekewa damu katika mshipa wa mguuni na kwenye mkono wa kushoto

Yaani nilivyoomuona mama alikuwa amevimba mpk nilimsahau .....alipona , japo kuna ukilema walimuachia

Na mm nilipona ila mkono ulibaki na kovu kubwa yaani huwa nikiangalia mkono napata uchungu kabisa na majambazi na vibaka

Yaani nikikamata naua kabisa kama kesi nitaikuta ....mahakamani!!
Yaani nawachukia sana na kamwe siitakuja kusahau tukio lile ...japo majuzi juzi nilivamiwa tena ila niliwazidi nguvu




View attachment 1328397

sent from toyota Allex
Pole. Upelelezi ulifanyika? Na yule polisi-jambazi alikamatwa? Au uliogopa kutoa ushahidi?
 
Pole. Upelelezi ulifanyika? Na yule polisi-jambazi alikamatwa? Au uliogopa kutoa ushahidi?
Niliogopa kumtaja !! Kuepusha uhai wangu but mwisho wa siku alikuja kukamatwa ......kuna tukio walilifanya mwanza mjini akakutwa kwake na smg akiwa ameificha katika tenki la maji ...ndio ikawa mwisho wake alihukumiwa miaka 20 jela......wakati mwingine wabaya wetu tunao mtaani hapo hapo

sent from toyota Allex
 
Ni story ndefu lakini usiombe kuvamiwa maana mungu tu ndio atakunusuru.

2017 walinivamia na kufanikiwa kuiba simu smartphone 4, kiasi cha fedha na kumjeruhi kijana mmoja nilikuwa naishi nae, ila walichokipata nao hawatosahau maisha yao huko walipo.

Ila tukio hili lilinipa somo kubwa sana maishani mwangu, lilinipa heshima pia ila lilisababisha nikawa na maadai wengi sana japo walikuwa wakiniogopa tu lakini walikuwa wakinichukia.

Sent using Jamii Forums mobile app
fafanua zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliogopa kumtaja !! Kuepusha uhai wangu but mwisho wa siku alikuja kukamatwa ......kuna tukio walilifanya mwanza mjini akakutwa kwake na smg akiwa ameificha katika tenki la maji ...ndio ikawa mwisho wake alihukumiwa miaka 20 jela......wakati mwingine wabaya wetu tunao mtaani hapo hapo

sent from toyota Allex
Kweli
 
Kanuni ya kwanza ukiwamiwa na majambazi na ukaona wamekuwahi basi unatakiwa kua mpole na kuwapa ushirikiano wote wanaouhitaji.

Majambazi hua na siraha ila huitumia tu pale wakiona usalama wao uko hatarini, zaidi zile ziraha hua ni kwa ajili ya kukutishia ili uogope, sasa ukileta mgomo hapo ndio hulazimika kutumia siraha.

Siku zote usibishane na jambazi, mpe ushirikiano wote unaohitajika, fuata maelekezo wanayokupatia.

Pia siku zote usidharau mlio/kelele yoyote isiyo ya kawaida wakati wa usiku unaousikia jirani au nyumbani kwako, hakikisha unaamka kuangalia ni kitu gani. Juzu mwezi wa 11 mwaka jana, nikiwa macho, taa inawaka chumbani kwangu na tena dirisha moja nimefungua pazia hivyo ukiwa nje unaniona, nikiwa nachat jamii forum sa 7 usiku nikasikia mlio wa kama dirisha la jikoni kwangu linavunjwa, nikapuuza nikasema itakua labda jirani yangu karudi, nikapuuzia, kumbe vibaka wanavunja dirisha waeeze kufungua mlango wa jikoni wazame ndani.

Baada ya kushindwa wakavunja grill ya jirani yangu, wakavunja mlango, wakaingia wanachukua laptop, flat ya samsung nchi 55 nshikaji alikua kainunua hata wiki haijaisha, wakachukua hela, wakaondoka, kumbe walikuja na gari hapo nje geti kubwa.

Bahati mbaya kwao ni kua niliamka kwenda kukojoa nizime taa nilale ila kabla sijapanda kulala nikaenda jikoni kuangalia, nakuta dirisha limevunjwa, mlango umelegea kama vile ulikua unachezewa, kufungua nakuta grill hangu imeng'olewa, kuangalia kwa jirani mlango uko wazi, grill imevunjwa, hapo ndio nikastuka, jirani amelala fofofo, nikamamuasha hakuamka, nikaachana nar kwanza, kisha kwangu nilikua na mshikaji kalala roon nyingine nikamuamsha, kutoka nje gari ikakimbia wakaacha mazaga yote waliokua wamekusanya nyumba za jirani zote. Hiyo ndio ikawa pona ya vitu vya mshikaji na majirani.

Vibaka wengi wa siku hizi ni washkaji tu, hawa vijana waliopenda kazi ila wanapenda kunywa na kula vizuri, kumiliki mademu wazuri nk. Mimi nikikamata kibaka/mwizi hawa masharobaro sitamuua wala kumpigia kelele, namuingiza room nampiga mashine ya kueleweka huku namchukua video kisha namuacha.
Ha ha ha...hapo mwishoni kweli umevurugwa[emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh jamaa Alitaka kumla shem kimasihara!?
Sio experience nzuri Kukutana nayo, pole Sana, ila ilitakiwa ujue walijuaje una hizo fedha, lazima kuna sehemu ulifanya nazo show off wakaziona thus why walikadilia kuwa ni more than 5 million.
Kama sio kuondoka nae casino Basi dereva tax alimuuza, hasa alipoamua kupita ofisini, jamaa akajua katoka kuchukua mpunga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mwaka 2013 niko zangu chuo,nilikuwa nasoma night maana kuna kikazi nlikuwa nakifanya mchana,
Nmetoka zangu chuo saa 3 usiku niko hoi,ni mmoja ya wale vijana ambao si maskini sana lakini mpenzi sana wa kubadilisha mavazi na kujipenda nisiyependa kujichanganya.
Basi nmerudi zangu nmechoka hatari na siku hyo dada yangu mtoto wa baba yangu mkubwa alikuwa ndo ameetoka kupewa mkopo wake wa almost 30m sema alichukua kama 2m nyingne akaiacha kwenye a/c yake.Basi mi sku hyo mapema tu kwenye saa 5 nkalala zangu,sasa majira ya kama saa 8 nkasikia mlio mkubwa mno akili yangu ikanambia hapa itakuwa ni transformer ya mtaani imebutuka ghafla kidogo tena naskia buuu na kishndo cha mlango kuanguka hapo sasa ndo nkashtuka na kujua sasa tumeingiliwa.Waliingia ndani kama 10 wengine wanaweza kufika hata 20 walikuwa nje na silaha na wengine na mapanga,walivyoingia kituo cha kwanza ni chumba cha wanawake,wakavunja mlango ote wakawalaza chini,then ndo wakaja na kwetu sasa ote tukawekwa barazani,dah nakumbuka walisafisha nyumba maana walibeba mpka raba zangu,lakini cha ajabu hawakutupiga hata kofi,na walivyoingia walikuwa wanajua taa zinawashwa wapi na kila chumba anakaa nani,basi majirani wakataka kutoka wakaambia atakayetoka tu anakula shaba ya kichwa,basi mwisho wa siku wakaiba mikufu ya dhahabu,pesa then wakaondoka dah hakuna siku niliyojiona mjinga kama siku hyo,mwenye nyumba alikasirika mno maana mpka alikuwa analia basi,majirani ndo wakatoka wakawa wanatupa pole pale,kuna baadhi ya vitu walishindwa kubeba hvyo waliviharibu tu kama Tv kubwa ya chogo na hata vioo vya gari walivunja kama kukomoa tu na tv walilibamiza chini.Ilivyofika asubuhi saa 12 tukaenda polisi kitunda tukakuta kituo bado hakijafunguliwa wakati tunasubiria tunaona wanakuja watu wngine wamekatwa na mapanga wanavuja damu,kumbe kila walivyoondoka kwetu kila waliyekutana nae njiani alikuwa anaporwa vitu vyake na kuchezea mapanga,pale polisi tulikaa mpka saa 1 ndo wakaja polisi cha ajabu hawakutupa hata uzito wa kusema waje eneo la tukio kukagua na mengineyo mengi yalitokea nisingependa kuyaandika basi mzee kwa hasira akaamua kuipotezea kesi but siku ile ile tukawapigia ndugu simu na kuwaelezea kilichotokea walikasirika mno,akapigiwa simu marehemu babu yetu mzaa mama akaja alivyoambiwa alikasirika mno.Kikafanyika kikao kidogo nakumbuka kulikuwa na ndugu walokuja kutuona tu sku hiyo si chini ya 30,na kilikuwa kipindi mvua inanyesha.Basi mzee akawaambia wale ndugu mpka saa 8 mchana kila mwenye mtoto kati ya wale waliokuwa pale na yupo dar basi anahitajika amlete pale kabla ya hiyo saa 8,na kweli kwenye saa 8 ote walikusanywa then ikaanza kusomwa dua ndani ya nusu saa kwanza mvua ikakata then tukatoka nje ote dua ikaendele dua inasomwa watoto wanaitikia,dua inasomwa watoto wanaitikia lakini kadri dua ilivyokuwa inasomwa ndivyo radi zikawa zinazidi haliyakuwa mvua imekata na jua limechomoza majirani wakawa wanatuangalia tu tunachofanya maana ilikuwa tunafanyia barabarani kabisa ya nyumbani,akaletwa mbuzi akachinjwa alafu akaachwa bila kichwa kumalizwa,unaambiwa mbuzi alikuwa anaruka zaidi ya nusu saa mwsho kabisa akafa akifa amesimama yah ndiyo alikufa akiwa amesimama kabisa huku shingo inaninginia baada ya dua tukamwachia mungu atupe majibu yake,lakini tukaambiwa kilichoibiwa kimeibiwa hvyo hata kikirudishwa haturuhusiwi kukipokea.

Kilichofata usiku ule ule majirani zetu wawili ambao siku ya tukio walikuwa mwanza walichomana visu vya moyo nakufa ote,Asubuhi kuna mzee mmoja jirani yetu ambae pia siku ya tukio alikuja kutupa pole alipata maumivu makali ya kichwa na kujipiga kichwa ukutani mpka mauti,inshort mpka siku ya 5 baada ya tukio walikuwa watu 10 ambao nawajua mtaani maana ilikuwa ni aliyeiba,aliyeshiriki,ote mungu awaadhibu naam ilikuwa ni adhabu mpka leo ukisahau simu yako barabarani unaikuta.
Hyo ndo experience yangu ya kuvamiwa na majambazi japo kuna baadhi walikuja kuomba msamaha na kurudisha vitu na hata kutoa fidia lakini hatukuweza kuvichukua au kuweza kusamehe tena japo roho ziliturudi ila ndo hvho vifo viliendelea ndani ya siku 10 mfululizo i hope kama binadamu unaweza kujua tulikuwa katika mtihani gani japo tulifanya kwa hasira ambayo iligeuka huzuni
asante mungu yalipita

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni story ndefu lakini usiombe kuvamiwa maana mungu tu ndio atakunusuru.

2017 walinivamia na kufanikiwa kuiba simu smartphone 4, kiasi cha fedha na kumjeruhi kijana mmoja nilikuwa naishi nae, ila walichokipata nao hawatosahau maisha yao huko walipo.

Ila tukio hili lilinipa somo kubwa sana maishani mwangu, lilinipa heshima pia ila lilisababisha nikawa na maadai wengi sana japo walikuwa wakiniogopa tu lakini walikuwa wakinichukia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hebu tuelezee basi tuchukue maexperience

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora wakuogope

Mimi nisingewekwa uvunguni wakati wa kuondoka ningewapiga Shaba maana hawakuiona

Na walikuja bila kujua nina bunduki bahati mbaya haikunisaidia kwa lolote dah hua naumia sana.
Unaumia nini sasa[emoji57][emoji57] badala ushukuru hata hawajaiona?

We unafikiri ni ujinga kutoitumia kumbe Mungu alitaka wasioone labda ingeleta maafa zaidi

Thanks be to God ....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom