Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Dah kwakwel me haijanitokea lakin mvua inyeeshapo usiku hua siwez kulala maana wanatumiaga huo mwanya kuiba
 
Huu ni uongo tosha
Majambazi hawana muda wa kujibishana na wewe. Eti hela nimepitisha kazini

Majambazi hujawahi kutana nao.

Umesema uliwekwa uvunguni, akaletwa na HG naye uvunguni...
Baadae unasema Mdogo wako aliwekwa chooni na HG

Mkeo hujasema alikuwa wapi

Majambazi hawama sababu ya kurusha risasi kama hakuna kilichotokea nje ya eneo la wizi.

Majambazi sio wajinga una bastola wakuachie wakiwa wanaondoka.



Sent using Jamii Forums mobile app
unambishia mwenye story yake upo timamu kweli?! hebu tupe huo ukweli basi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mwaka 2013 niko zangu chuo,nilikuwa nasoma night maana kuna kikazi nlikuwa nakifanya mchana,
Nmetoka zangu chuo saa 3 usiku niko hoi,ni mmoja ya wale vijana ambao si maskini sana lakini mpenzi sana wa kubadilisha mavazi na kujipenda nisiyependa kujichanganya.
Basi nmerudi zangu nmechoka hatari na siku hyo dada yangu mtoto wa baba yangu mkubwa alikuwa ndo ameetoka kupewa mkopo wake wa almost 30m sema alichukua kama 2m nyingne akaiacha kwenye a/c yake.Basi mi sku hyo mapema tu kwenye saa 5 nkalala zangu,sasa majira ya kama saa 8 nkasikia mlio mkubwa mno akili yangu ikanambia hapa itakuwa ni transformer ya mtaani imebutuka ghafla kidogo tena naskia buuu na kishndo cha mlango kuanguka hapo sasa ndo nkashtuka na kujua sasa tumeingiliwa.Waliingia ndani kama 10 wengine wanaweza kufika hata 20 walikuwa nje na silaha na wengine na mapanga,walivyoingia kituo cha kwanza ni chumba cha wanawake,wakavunja mlango ote wakawalaza chini,then ndo wakaja na kwetu sasa ote tukawekwa barazani,dah nakumbuka walisafisha nyumba maana walibeba mpka raba zangu,lakini cha ajabu hawakutupiga hata kofi,na walivyoingia walikuwa wanajua taa zinawashwa wapi na kila chumba anakaa nani,basi majirani wakataka kutoka wakaambia atakayetoka tu anakula shaba ya kichwa,basi mwisho wa siku wakaiba mikufu ya dhahabu,pesa then wakaondoka dah hakuna siku niliyojiona mjinga kama siku hyo,mwenye nyumba alikasirika mno maana mpka alikuwa analia basi,majirani ndo wakatoka wakawa wanatupa pole pale,kuna baadhi ya vitu walishindwa kubeba hvyo waliviharibu tu kama Tv kubwa ya chogo na hata vioo vya gari walivunja kama kukomoa tu na tv walilibamiza chini.Ilivyofika asubuhi saa 12 tukaenda polisi kitunda tukakuta kituo bado hakijafunguliwa wakati tunasubiria tunaona wanakuja watu wngine wamekatwa na mapanga wanavuja damu,kumbe kila walivyoondoka kwetu kila waliyekutana nae njiani alikuwa anaporwa vitu vyake na kuchezea mapanga,pale polisi tulikaa mpka saa 1 ndo wakaja polisi cha ajabu hawakutupa hata uzito wa kusema waje eneo la tukio kukagua na mengineyo mengi yalitokea nisingependa kuyaandika basi mzee kwa hasira akaamua kuipotezea kesi but siku ile ile tukawapigia ndugu simu na kuwaelezea kilichotokea walikasirika mno,akapigiwa simu marehemu babu yetu mzaa mama akaja alivyoambiwa alikasirika mno.Kikafanyika kikao kidogo nakumbuka kulikuwa na ndugu walokuja kutuona tu sku hiyo si chini ya 30,na kilikuwa kipindi mvua inanyesha.Basi mzee akawaambia wale ndugu mpka saa 8 mchana kila mwenye mtoto kati ya wale waliokuwa pale na yupo dar basi anahitajika amlete pale kabla ya hiyo saa 8,na kweli kwenye saa 8 ote walikusanywa then ikaanza kusomwa dua ndani ya nusu saa kwanza mvua ikakata then tukatoka nje ote dua ikaendele dua inasomwa watoto wanaitikia,dua inasomwa watoto wanaitikia lakini kadri dua ilivyokuwa inasomwa ndivyo radi zikawa zinazidi haliyakuwa mvua imekata na jua limechomoza majirani wakawa wanatuangalia tu tunachofanya maana ilikuwa tunafanyia barabarani kabisa ya nyumbani,akaletwa mbuzi akachinjwa alafu akaachwa bila kichwa kumalizwa,unaambiwa mbuzi alikuwa anaruka zaidi ya nusu saa mwsho kabisa akafa akifa amesimama yah ndiyo alikufa akiwa amesimama kabisa huku shingo inaninginia baada ya dua tukamwachia mungu atupe majibu yake,lakini tukaambiwa kilichoibiwa kimeibiwa hvyo hata kikirudishwa haturuhusiwi kukipokea.

Kilichofata usiku ule ule majirani zetu wawili ambao siku ya tukio walikuwa mwanza walichomana visu vya moyo nakufa ote,Asubuhi kuna mzee mmoja jirani yetu ambae pia siku ya tukio alikuja kutupa pole alipata maumivu makali ya kichwa na kujipiga kichwa ukutani mpka mauti,inshort mpka siku ya 5 baada ya tukio walikuwa watu 10 ambao nawajua mtaani maana ilikuwa ni aliyeiba,aliyeshiriki,ote mungu awaadhibu naam ilikuwa ni adhabu mpka leo ukisahau simu yako barabarani unaikuta.
Hyo ndo experience yangu ya kuvamiwa na majambazi japo kuna baadhi walikuja kuomba msamaha na kurudisha vitu na hata kutoa fidia lakini hatukuweza kuvichukua au kuweza kusamehe tena japo roho ziliturudi ila ndo hvho vifo viliendelea ndani ya siku 10 mfululizo i hope kama binadamu unaweza kujua tulikuwa katika mtihani gani japo tulifanya kwa hasira ambayo iligeuka huzuni
asante mungu yalipita

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ulirudia tena hii mambo?? Ulisahau ile sikio uliong'atwa mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya kukamatwa kuna jamaa yangu ndio alionekana pesa ilitumwa kwake


Alikua na duka la simu mitaa ya dampo/ngokozi ndio mfadhili wao alikua

Ni jamaa tunaejua fika.
Kwanza pole kwa yaliyokupata. Ulikumbana na mtihani mkubwa sana. Story yako inaonyesha ni tukio la kweli hivyo wapuuze wanaobeza. Ila hayo majambazi ni mazembe kweli kweli. Ukiona jambazi anayekwenda kupora halafu anakimbilia kubaka ujue ana akili ndogo. Siku hizi maendeleao ya technologia yanafanya DNA iwe chanzo kizuri sana cha kukamata mhalifu na pia ushahidi mzuri mahakamani. Hata hizo kadi za benki walizochukuwa ni ujinga mwingine.
 
Wewe story yako ya kweli maana majambazi wakijua una hela afu uwaambie huna hawakuachi hivi hivi
Da nakumbuka mwaka 1999 ....nikiwa na mama wadogo zangu wawili walisafiri kwenda kijijini mi niligoma nikabaki na mama

Mama alikuwa kaajiriwa duka moja la tajiri kuuza sement....!! Katika biashara siku moja aliuza sement kama za Milion 9 ...kutokama na MEM ilikuwa imepamba moto

Wakati akitoka dukani kuna watu walikuwa wanamfatilia kwa nyuma bila kujua alipofika zile hela akanipa mimi zikiwa kwenye jagi ...la maji likuwa tupu nikachukua kama natoka kwenda kununua kitu dukani nikazipeleka zile hela mpk kwa tajiri yake mama ...

Maana ilikuwa desturi kunituma mm mida ya saa moja na nusu nilifika akahesabu akaniandikia kitabu cha risiti cha kupeka hela nikarudi

Tukalal mm nikuwa nalala sebleni ...mama alikuwa nalala chumbani. ..mida ya saa saba usiku nikasikia mlango ukipigwa kwa nguvu !! ...aise na nilikuwa bado chali mdogo nikiwa darasa la V

Mlango ulipasuka mbao zikaachia watu kama nane waliingia ndani , ......wakapitiliza mpk chumbani kwa mama !!

Wakaanza kumuomba hela huku wanampiga kichwani ubavuni.......!! Mama alilamika sana akawa anawaambia mbn sina hela nimezipeleka kwa tajiri yangu

Mwingine kwa nje akawa anasema kama hela muueni ...sauti yake niliitambua alikuwa ni polisi ....kabisa tena jirani yetu !! Nyumba km ya tano ..


Nilishikwa na uchungu nikarusha taa ya chemri ilikuwa karibu na kitanda nilipigwa risasi mkono !! Nilianguka chini kutokana na damu nyingi kutoka nilizima kabisa

Yaani walichoambulia ni laki mbili tu !! Ila walimpiga sana mama na walijua wamemuacha wamemua pamoja na mm

Nilikuja kushituka mchana tokea saa sita mchana nipo hospital watu wamenijalia ndugu ...muda huo nilikuwa nimewekewa damu katika mshipa wa mguuni na kwenye mkono wa kushoto

Yaani nilivyoomuona mama alikuwa amevimba mpk nilimsahau .....alipona , japo kuna ukilema walimuachia

Na mm nilipona ila mkono ulibaki na kovu kubwa yaani huwa nikiangalia mkono napata uchungu kabisa na majambazi na vibaka

Yaani nikikamata naua kabisa kama kesi nitaikuta ....mahakamani!!
Yaani nawachukia sana na kamwe siitakuja kusahau tukio lile ...japo majuzi juzi nilivamiwa tena ila niliwazidi nguvu




View attachment 1328397

sent from toyota Allex

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duhhh...
Pole sana mkuu.
Pale Mecco, vijana wengi wazee wao walijiweza miaka ya nyuma na wakajenga majumba makubwa na mazuri miaka ile kabla ya ule mtaro kujazwa na taka na kuiunganisha Kangae.
Mbaya zaidi, vijana wengi wa maeneo yale wali acha kusoma na kuendekeza urahabu kwa jeuri ya pesa za baba zao hadi wakajisahau kwamba wazee wao wamesha choka na pesa zimewaishia na nyumba zao zilisha kuwa chakavu.
Mwisho wa siku vijana wamebaki kuwa wezi, vibaka na wakabaji tupu.
Nakumbuka marehem Masubo aliwahi kuwacharanga vijana flani na beto pale Cheers

Sent using Jamii Forums mobile app
Mzee baba, Yaani unavyoandika ni kama vile movie la Mecco.
Linaanzia Tekila Bar jirani na kwa Ali Mwehu.
mbele kidogo kuna Jump around, ukija kwa chini kuna May Day Bar.
Mashineni kwa Peter. (Tajiri miaka hiyo ni Asante Polepole mmiliki wa Kosa sura)
Inzilankoma Kwao Bena (kwa kina shadu)
Bila kumsahau Mzee Mzalendo Baba yao Kapteni na Warioba.
Mzee holela a.k.a TUPWISA

hapo kila jina lina Historia Yake na kituko chake.


Kabla masubo hajaama pale jirani na kwa Madaki, alikuwa na kiwanda cha kutengeneza senyenge.

Last year I was there. Nimepa miss Sana.
 
Kwanza pole kwa yaliyokupata. Ulikumbana na mtihani mkubwa sana. Story yako inaonyesha ni tukio la kweli hivyo wapuuze wanaobeza. Ila hayo majambazi ni mazembe kweli kweli. Ukiona jambazi anayekwenda kupora halafu anakimbilia kubaka ujue ana akili ndogo. Siku hizi maendeleao ya technologia yanafanya DNA iwe chanzo kizuri sana cha kukamata mhalifu na pia ushahidi mzuri mahakamani. Hata hizo kadi za benki walizochukuwa ni ujinga mwingine.

Sahihi mkuu
 
Masubo alianza na biashara na uaafiri enzi za chai maharage, kisha akaja kwenye biashara ya mabondo, na wakati huo alikuwa kijana aliye tazamwa kwa jicho la wasiwasi, kisha akaja kwenye biashara ya kuuza soli za viatu toka Kenya na kabla hajafariki na kinacho semekana (kwenye mabano) alianzisha biashara ya kuuza simu na vifaa vyake

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna zile gari mbili za Masubo moja ilikuwa imeandikwa Redemption. Kisha akanunua Basi Moja yenye rangi ya Zambarau ilokuwa na mziki mkubwa.
 
Huyo huyo Masubo Mkuu!

Alikuwa na Toyota Surf au Nissan Patrol (sikumbuki vizuri) pia miaka ya 200... ina mziki mkubwa utafikiri gari la matangazo ila vijana wake ndo walikuwa wanaitumia zaidi.
Ilikuwa Land Cruiser Amazon (Like) Nyekundu Miaka hiyo ndiyo yupo kwenye harakati za kuhamia Buzuruga karibu na Kisima cha Kwa bibi Lena.
 
Mwaka 2010, nyumbani tulikuwa wawili tu, mimi na mama watoto,tu na wakati huo tulikuwa hatujaanzisha familia bado.

Nilirudi nyumbani mapema Sana siku hiyo mida ya saa 12 jioni tu, baada ya kula mapema pia nikaenda kujipumzisha mapema pia, saa nane usiku nikasikia milio ya bunduki, nikahisi hapa tushavamiwa, Jana yake tu nilikuwa nimetoka kuchukua kagari Ka kutembelea( T blj), nikajua pengine ndo wanafata Hilo Gari, kwa hiyo si kuwa na idea kama wangeweza kunidhuru kwa kuiba Gari ambalo lipo nje na wangeweza kuwasha tu hata kwa funguo Malaya na kuondoka. Nyumba haikuwa na fensi

Kulikuwa na ukimya wa kama dakika moja, nikasikia tena milio mkubwa Sana maeneo mlango wa sebuleni na wa jikoni kwa pamoja! Sekunde kadhaa tu wakawa tayari wanavunja mlango wa chumba changu!

Muda wote huo wife anahangaika kujificha chini ya uvungu bila mafanikio, ni kibonge flan, so zoezi Zima la yeye kuingia huko halikuwezekana,mpaka jamaa wameingia nilikuwa Sina clue, yaan wakanza straight na mapanga mwilini,, toa pesa!toa pesa! Tunajua umezificha, chumbani walingia kama watu watano,wawili ni heavy kiasi kwamba nikahisi hapa nikijaribu kufurukuta napotea, watatu wa kawaida tu ningeweza kupambana nao kama wasingeambatana na Hao heavy duty, nikaona ni comply tu yaishe!

Mapanga yalitembea takriban dk 5 mfululizo, wife ndo alikua mtetezi wangu analia kwa kuwaambia kuwa Leo huyo baba hajaja na hela, an gekuwa nazo angewapa, kiukweli Nina kawaida ya kumkabidhi wife kila siku kile nilichokuja nacho nyumbani, na siku hiyo kweli si kuwa na pesa niliyokuja nayo nyumbani, ila kulikuwa na laki mbili tu kabatini ambayo nayo ilikuwa kama balance ya dharula, wakaichukua!

Moment ambayo Hua inaniumiza hadi Leo, ni kuna mmoja alikuwa amepania kuniua kabisa alipiga panga mbili Moja ikaingia haswa, ya pili nikasema hapana, ngoja nikinge, ikaondoka na kidole kimoja, baadaye akanitupia taulo huku akisema jifunike sasa nakata shingo hapo nadhan ufahamu wangu ndo ulifika mwisho,

Wife alikuwa anaona kila kitu, anasema baada ya tukio la kunitupia taulo alipiga panga mbili ambazo alikosa zote, ikawa wenzake wanamuita kwa code ndo ikawa pona yangu, nililala hapo chini huku nikiwa Sina fahamu, hadi nilipokuja kusikia sauti ya wife aliniambia mume wangu, kama upo hai amka wamesha ondoka,!! Ni sauti ya huzuni kabisa kuwa hi kusikia Kutoka kwa mke wangu, anasema alijaribu mara kadhaa Kuniambia hivyo, Lakin si ku respond akajua nshapotea. nadhan mungu tu alikuwa upande wangu siku hiyo.

Hawakuchukua Gari ambalo nilidhani ndo liliwaleta, kilichofata nilikimbia nyumba na kwenda kupanga Tena mana niliona haikuwa bahati yangu kujenga, ila Nilirudi baada ya kupata Familia, na nipo hadi sasa ila nina makovu kichwani na kidole kimoja Sina, plus mimi. Na wife kila ikifika saa nane usiku automatically tunakua macho, hii nadhan ni physiological toucher ambayo tutakufa nayo

User name yangu inareflect namba za Gari ambazo nadhan lilichangia pia kuniletea majanga. siku ya tukio tulivamiwa nyumba tatu mitaani, sisi tulikuwa wa mwisho kuvamiwa na Kutoka na maisha. nyumba moja walimuua baba na ya pili wakaumuua mlinzi, kwa maelezo ya wenzetu muuaji alikuwa yule yule aliyekuwa ananisulubu mie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom