Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

2013 Natokea morogoro tumefika kibamba kuna foleni moja ya maana kuingia jijini, ilikuwa mida ya saa moja usiku hadi tunafika ubungo ni saa saba kasoro usiku (mimi mwenyewe sijawahi kuamini), Kituo changu cha mwisho ni makumbusho, nikashuka zangu ubungo mataa pale nikasogea kushoto kidogo nikakamata hiace (private) ilikuwa inachukua abiria wa mwenge na ilikuwa hiyohiyo tu kituoni, nikashuka mwenge nikakamata nyingine ilikuwa pekee kituoni pia inaenda magomeni kupitia shekilango rd. nikashuka chuo cha ustawi wa jamii, nikasogea mbele kidogo kuna njia huwa inaingia kushoto kabla ya hongera bar.

Mdogomdogo natembea zangu nikiwa makini sana, bahati nzuri sikuwa na mzigo wowote zaidi ya simu ambayo tayari nishaiweka mfukoni pamoja na wallet ikiwa na kama elfu kumi na saba hivi, nyuma ya chuo kuna mtaro mkubwa hivi kushoto kwa mbaaali kwenye kona nikawaona jamaa wamekaa kwenye mtaro wanamulikwa kwa tabu na taa za nyumba zilizoko upande wa kulia mwa barabara, nikajisemea leo ndo leo siku yangu imefika, sikutaka kurudi kwani nilikopita hapakuwa shwari pia.

Kiasi ninawakaribia nikawaona vizuri japo huwezi kuwatambua sura zao, walikuwa kama watano hivi mmoja akasimama akawa kama anavuka barabara kwa hatua za kusubiri sana, mimi niko katikati ya barabara nazidi kumkaribia, bado kama hatua kumi na tano nimfikie upande wa kulia likatokea kundi lingine la watu kama saba hivi baadhi yao wakiwa na vitu kama nyundo au rungu hivi nikajua kumekucha. nazidi kumkaribia jamaa kwa mbele ikawa inakuja coaster inatokea upande wa sayansi, nikasema Alhamdulillahi, namfikia jamaa akamalizia kuvuka na coaster ndo inapita hiyo speed niliyotoka nayo sijawahi kukimbia vile, nafika mbali nishawaacha wote wale nageuka nyuma nawakuta wako barabarani wote wamenigeuka wengine kama wanacheka hivi hadi wanainama.... sikupita chocho tena ikabidi nitokeze tu barabara kubwa sayansi nikamalizia mwendo hadi home mapigo ya moyo yakiwa very high.
 
Sasa mtu bado kala na kunya juu [emoji23]
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hahahahah huyu sasa ndio kidume ndago baba LA baba kama unaye hadi Leo embu MPE mambo matamu usiku wa Leo hahahah

Sent using Jamii Forums mobile app
Msifiee upuuzi tu...usiombee hao jamaa watekaji wakukutee.kuna wenginee wanakulaa kibogaa....unakimbuka story ya mashiftaa kwenye maporii ya utalii..madereva wengi wa utalii waliliwaa viboga sanaa
 
Huo ndo upimbiii dereva gani unatembea root ya mbali bilaa spare Tyree chief
 
[emoji23] [emoji23] kicheche ndege au
 
Wee Ni boyaaa Sanaa.unamkimbia mke wako unamuachaa mtoto wako kwa manyangau.
 
Huo ndo upimbiii dereva gani unatembea root ya mbali bilaa spare Tyree chief
Sikuwa na tairi uchwara so nilijiamini kupita kiasi na nilienda mpaka Dar bila spare tyre uhenga unasaidia dogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…