Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

mimi nikiwa secondary niliona wananchi kadhaa wanamfukuza mwizi na mimi nikaunga tena mimi ndiyo nikawa namkaribia kabisa kumkamata huyo mwizi na hao wananchi wengine wapo nyuma yangu tunamkimbiza mwizi kwa pamoja,

tulivyofika maeneo flani kwenye reli gafla yule mwizi tunayemkimbiza akapiga break kali sana nikawa niko katikati ya huyo mwizi na wale wakimbizaji wengine, kwa haraka sana nikagundua kuwa huo ulikua ni mtego na hao wakimbizaji wengine pia ni vibaka wakawa wameniweka kati,

wakanitazama nimeavaa nguo za shule wakajua sina pesa wakaniambia niondoke haraka sana,
kuanzia hapo nikakoma kukimbiza wezi hovyo labda awe mwizi aliyeniibia mimi.
 
mimi nikiwa secondary niliona wananchi kadhaa wanamfukuza mwizi na mimi nikaunga tena mimi ndiyo nikawa namkaribia kabisa kumkamata huyo mwizi na hao wananchi wengine wapo nyuma yangu tunamkimbiza mwizi kwa pamoja,
tulivyofika maeneo flani kwenye reli gafla yule mwizi tunayemkimbiza akapiga break kali sana nikawa niko katikati ya huyo mwizi na wale wakimbizaji wengine, kwa haraka sana nikagundua kuwa huo ulikua ni mtego na hao wakimbizaji wengine pia ni vibaka wakawa wameniweka kati,
wakanitazama nimeavaa nguo za shule wakajua sina pesa wakaniambia niondokea haraka sana,
kuanzia hapo nikakoma kukimbiza wezi hovyo.
😂😂😂😂
 
Jamaa ulikuwa na mbio zaidi ya akili
 
Mtoa
Nakumbuka ilikua mwaka 2011.

Nikiwa nafanya biashara ya viatu jijini Dar es Salaam, hapo nna miezi sita tu tangu kuingia jiji hilo la kibiashara.

Nikawa naishi na mshkaji wangu maeneo ya Kimara butcher.Siku moja nmetoka Kariakoo kuchukua mzigo nikawa narudi huku natembea mdogomdogo barabarani foleni ilikuwa kubwa sana. Mahesabu yangu nikifika mbele kabisa ambako hakuna foleni sana nipande daladala.

Ghafla kufika maeneo ya Manzese nakutana na kundi kubwa la vijana wakiwa wamebeba mapanga,kuna jamaa yupo njiani ananambia hao ndio wafalme wa Dar es Salaam. Mimi nikasogea nijue kuna nini wakasogea barabarani wakaizingira gari moja ilikuwa imepakia ng'ombe nikamfuata kijana mmoja wao nikamuuliza kwani vipi akasema wale ng'ombe ni wa kwao wameibiwa.

Utingo wa lile gari akawa anajitetea kuwa wao wamepewa kazi tu ya kusafirisha yeye hajui issue yoyote kuhusu hao ng'ombe.

Aisee! Ghafla kijana mmoja akamfuata utingo akampiga panga la mgongo kisha vijana wengine nao wakaanza kumkatakata utingo kama nyama vile nikaona hii kesi ngoja niondoke.

Ghafla mmoja wa wale vijana nae akiwa kabeba panga akaniita,akanambia kaa pembeni hapo.
Alarm ya hatari ikalia kichwani mwangu nikaona hapa soon naibiwa ikabidi nijifanye na mimi mhuni,
nilivyoona haniangalii nikatoa hela mfukoni nikaweka kwenye kiatu kijanja sana halafu nikamuuliza yule kibaka aliyenizuia kuondoka "oya hivi maeneo haya wapi napata geji?(ugoro)"

Jamaa akanishangaa kidogo,akanambia mbona pale maeneo ya kuuza geji yapo kibao twende anipeleke.

Nikamwambia tatizo sijatembea na hela hivyo kama ana ugoro kidogo anisaidie maana nina arosto mpaka mavi yananibana.

Jamaa akasema nisimzingue kwani kwenye begi nimebeba nini.Hapo kawoga kapo kwa mbali nikamfungulia begi nikamwambia kuna viatu tu ndo nataka nikaviuze nipate pesa.

Jamaa akamwaga viatu vyangu vyote hakuona pesa,akaanza kunisachi mifukoni hakukuta pesa, akanambia bahati yangu nina arosto angechukua viatu vile.

Akanitolea ugoro akanambia nichukue kidogo, nami kujifanya mhuni ikabidi nizuge hivyo hivyo nikachukua nikaupachika mdomoni.

Nilikuwa sijawahi na sijui hata kuutumia huo ugoro ila nikazuga jamaa wakanambia niondoke hapo nawatilia kiwingu ikabidi nisepe haraka haraka kufika mbele nilitembea haraka nikapanda daladala.

Tangu siku hiyo nilijifunza kumind my business yaani kushangaa mwizi wa ng'ombe kulitaka kusababisha na mimi niibiwe.

Siku hizi hata nikikuta mtu anaibiwa ilimradi mimi siathiriki chochote basi siingilii.
Kuna siku nilikuta vijana wawili wanamuibia mwanamke karibu na machinga complex nilipita kama sioni vile.

Kila mtu ana njia zake za kuingiza kipato., sihangaiki na ishu za wengine mpaka ziwe zinagusa maslahi yangu
Mtoa mada mbna Kama hapo kwenye ugoro Kuna ukakasi
 
Wanaume wa dar bhana
 
mimi nikiwa secondary niliona wananchi kadhaa wanamfukuza mwizi na mimi nikaunga tena mimi ndiyo nikawa namkaribia kabisa kumkamata huyo mwizi na hao wananchi wengine wapo nyuma yangu tunamkimbiza mwizi kwa pamoja,

tulivyofika maeneo flani kwenye reli gafla yule mwizi tunayemkimbiza akapiga break kali sana nikawa niko katikati ya huyo mwizi na wale wakimbizaji wengine, kwa haraka sana nikagundua kuwa huo ulikua ni mtego na hao wakimbizaji wengine pia ni vibaka wakawa wameniweka kati,

wakanitazama nimeavaa nguo za shule wakajua sina pesa wakaniambia niondokea haraka sana,
kuanzia hapo nikakoma kukimbiza wezi hovyo labda awe mwizi aliyeniibia mimi.
Haa haa haa kula like kwanza mkuu!
Story yako imenifurahisha sana ndugu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom