Mwaka 2010, nyumbani tulikuwa wawili tu, mimi na mama watoto,tu na wakati huo tulikuwa hatujaanzisha familia bado.
Nilirudi nyumbani mapema Sana siku hiyo mida ya saa 12 jioni tu, baada ya kula mapema pia nikaenda kujipumzisha mapema pia, saa nane usiku nikasikia milio ya bunduki, nikahisi hapa tushavamiwa, Jana yake tu nilikuwa nimetoka kuchukua kagari Ka kutembelea( T blj), nikajua pengine ndo wanafata Hilo Gari, kwa hiyo si kuwa na idea kama wangeweza kunidhuru kwa kuiba Gari ambalo lipo nje na wangeweza kuwasha tu hata kwa funguo Malaya na kuondoka. Nyumba haikuwa na fensi
Kulikuwa na ukimya wa kama dakika moja, nikasikia tena milio mkubwa Sana maeneo mlango wa sebuleni na wa jikoni kwa pamoja! Sekunde kadhaa tu wakawa tayari wanavunja mlango wa chumba changu!
Muda wote huo wife anahangaika kujificha chini ya uvungu bila mafanikio, ni kibonge flan, so zoezi Zima la yeye kuingia huko halikuwezekana,mpaka jamaa wameingia nilikuwa Sina clue, yaan wakanza straight na mapanga mwilini,, toa pesa!toa pesa! Tunajua umezificha, chumbani walingia kama watu watano,wawili ni heavy kiasi kwamba nikahisi hapa nikijaribu kufurukuta napotea, watatu wa kawaida tu ningeweza kupambana nao kama wasingeambatana na Hao heavy duty, nikaona ni comply tu yaishe!
Mapanga yalitembea takriban dk 5 mfululizo, wife ndo alikua mtetezi wangu analia kwa kuwaambia kuwa Leo huyo baba hajaja na hela, an gekuwa nazo angewapa, kiukweli Nina kawaida ya kumkabidhi wife kila siku kile nilichokuja nacho nyumbani, na siku hiyo kweli si kuwa na pesa niliyokuja nayo nyumbani, ila kulikuwa na laki mbili tu kabatini ambayo nayo ilikuwa kama balance ya dharula, wakaichukua!
Moment ambayo Hua inaniumiza hadi Leo, ni kuna mmoja alikuwa amepania kuniua kabisa alipiga panga mbili Moja ikaingia haswa, ya pili nikasema hapana, ngoja nikinge, ikaondoka na kidole kimoja, baadaye akanitupia taulo huku akisema jifunike sasa nakata shingo hapo nadhan ufahamu wangu ndo ulifika mwisho,
Wife alikuwa anaona kila kitu, anasema baada ya tukio la kunitupia taulo alipiga panga mbili ambazo alikosa zote, ikawa wenzake wanamuita kwa code ndo ikawa pona yangu, nililala hapo chini huku nikiwa Sina fahamu, hadi nilipokuja kusikia sauti ya wife aliniambia mume wangu, kama upo hai amka wamesha ondoka,!! Ni sauti ya huzuni kabisa kuwa hi kusikia Kutoka kwa mke wangu, anasema alijaribu mara kadhaa Kuniambia hivyo, Lakin si ku respond akajua nshapotea. nadhan mungu tu alikuwa upande wangu siku hiyo.
Hawakuchukua Gari ambalo nilidhani ndo liliwaleta, kilichofata nilikimbia nyumba na kwenda kupanga Tena mana niliona haikuwa bahati yangu kujenga, ila Nilirudi baada ya kupata Familia, na nipo hadi sasa ila nina makovu kichwani na kidole kimoja Sina, plus mimi. Na wife kila ikifika saa nane usiku automatically tunakua macho, hii nadhan ni physiological toucher ambayo tutakufa nayo
User name yangu inareflect namba za Gari ambazo nadhan lilichangia pia kuniletea majanga. siku ya tukio tulivamiwa nyumba tatu mitaani, sisi tulikuwa wa mwisho kuvamiwa na Kutoka na maisha. nyumba moja walimuua baba na ya pili wakaumuua mlinzi, kwa maelezo ya wenzetu muuaji alikuwa yule yule aliyekuwa ananisulubu mie.
Sent using
Jamii Forums mobile app