Da nakumbuka mwaka 1999 ....nikiwa na mama wadogo zangu wawili walisafiri kwenda kijijini mi niligoma nikabaki na mama
Mama alikuwa kaajiriwa duka moja la tajiri kuuza sement....!! Katika biashara siku moja aliuza sement kama za Milion 9 ...kutokama na MEM ilikuwa imepamba moto
Wakati akitoka dukani kuna watu walikuwa wanamfatilia kwa nyuma bila kujua alipofika zile hela akanipa mimi zikiwa kwenye jagi ...la maji likuwa tupu nikachukua kama natoka kwenda kununua kitu dukani nikazipeleka zile hela mpk kwa tajiri yake mama ...
Maana ilikuwa desturi kunituma mm mida ya saa moja na nusu nilifika akahesabu akaniandikia kitabu cha risiti cha kupeka hela nikarudi
Tukalal mm nikuwa nalala sebleni ...mama alikuwa nalala chumbani. ..mida ya saa saba usiku nikasikia mlango ukipigwa kwa nguvu !! ...aise na nilikuwa bado chali mdogo nikiwa darasa la V
Mlango ulipasuka mbao zikaachia watu kama nane waliingia ndani , ......wakapitiliza mpk chumbani kwa mama !!
Wakaanza kumuomba hela huku wanampiga kichwani ubavuni.......!! Mama alilamika sana akawa anawaambia mbn sina hela nimezipeleka kwa tajiri yangu
Mwingine kwa nje akawa anasema kama hela muueni ...sauti yake niliitambua alikuwa ni polisi ....kabisa tena jirani yetu !! Nyumba km ya tano ..
Nilishikwa na uchungu nikarusha taa ya chemri ilikuwa karibu na kitanda nilipigwa risasi mkono !! Nilianguka chini kutokana na damu nyingi kutoka nilizima kabisa
Yaani walichoambulia ni laki mbili tu !! Ila walimpiga sana mama na walijua wamemuacha wamemua pamoja na mm
Nilikuja kushituka mchana tokea saa sita mchana nipo hospital watu wamenijalia ndugu ...muda huo nilikuwa nimewekewa damu katika mshipa wa mguuni na kwenye mkono wa kushoto
Yaani nilivyoomuona mama alikuwa amevimba mpk nilimsahau .....alipona , japo kuna ukilema walimuachia
Na mm nilipona ila mkono ulibaki na kovu kubwa yaani huwa nikiangalia mkono napata uchungu kabisa na majambazi na vibaka
Yaani nikikamata naua kabisa kama kesi nitaikuta ....mahakamani!!
Yaani nawachukia sana na kamwe siitakuja kusahau tukio lile ...japo majuzi juzi nilivamiwa tena ila niliwazidi nguvu
View attachment 1328397
sent from toyota Allex