Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Mwaka 2010, nyumbani tulikuwa wawili tu, mimi na mama watoto,tu na wakati huo tulikuwa hatujaanzisha familia bado.

Nilirudi nyumbani mapema Sana siku hiyo mida ya saa 12 jioni tu, baada ya kula mapema pia nikaenda kujipumzisha mapema pia, saa nane usiku nikasikia milio ya bunduki, nikahisi hapa tushavamiwa, Jana yake tu nilikuwa nimetoka kuchukua kagari Ka kutembelea( T blj), nikajua pengine ndo wanafata Hilo Gari, kwa hiyo si kuwa na idea kama wangeweza kunidhuru kwa kuiba Gari ambalo lipo nje na wangeweza kuwasha tu hata kwa funguo Malaya na kuondoka. Nyumba haikuwa na fensi

Kulikuwa na ukimya wa kama dakika moja, nikasikia tena milio mkubwa Sana maeneo mlango wa sebuleni na wa jikoni kwa pamoja! Sekunde kadhaa tu wakawa tayari wanavunja mlango wa chumba changu!

Muda wote huo wife anahangaika kujificha chini ya uvungu bila mafanikio, ni kibonge flan, so zoezi Zima la yeye kuingia huko halikuwezekana,mpaka jamaa wameingia nilikuwa Sina clue, yaan wakanza straight na mapanga mwilini,, toa pesa!toa pesa! Tunajua umezificha, chumbani walingia kama watu watano,wawili ni heavy kiasi kwamba nikahisi hapa nikijaribu kufurukuta napotea, watatu wa kawaida tu ningeweza kupambana nao kama wasingeambatana na Hao heavy duty, nikaona ni comply tu yaishe!

Mapanga yalitembea takriban dk 5 mfululizo, wife ndo alikua mtetezi wangu analia kwa kuwaambia kuwa Leo huyo baba hajaja na hela, an gekuwa nazo angewapa, kiukweli Nina kawaida ya kumkabidhi wife kila siku kile nilichokuja nacho nyumbani, na siku hiyo kweli si kuwa na pesa niliyokuja nayo nyumbani, kulikuwa na laki mbili tuu kabatini ambayo ilikuwa kama balance ya dharula wakaichukua

Momment ambayo Hua inaniumiza hadi Leo, ni kuna mmoja alikuwa amepania kuniua kabisa alipiga panga mbili Moja ikaingia haswa, ya pili nikasema ngoja nikinge, ikaondoka na kidole kimoja, baadaye akanitupia taulo huku akisema jifunike sasa nakata shingo hapo nadhan ufahamu wangu ndo ulifika mwisho,

Wife alikuwa anaona kila kitu anasema baada ya tukio la kunitupia taulo alipiga panga mbili ambazo alikosa zote, ikawa wenzake wanamuita kwa code ndo pona yangu, nililala hapo chini huku nikiwa Sina fahamu, hadi nilipokuwa kusikia sauti ya wife aliniambia mume wangu kama upo hai amka wamesha ondoka,!! Ni sauti ya huzuni kabisa kuwa hi kusikia Kutoka kwa mke wangu, anasema alijaribu mara kadhaa Kuniambia hivyo, Lakin si ku respond akajua nshapotea. nadhan mungu tu alikuwa upande wangu siku hiyo.

Hawakuchukua Gari ambalo nilidhani ndo liliwaleta, kilichofata nilikimbia nyumba na kwenda kupanga Tena mana niliona haikuwa bahati yangu kujenga, ila Nilirudi baada ya kupata Familia, na nipo hadi sasa ila nina makovu kichwani na kidole kimoja Sina, plus mimi. Na wife kila ikifika saa nane usiku automatically tunakua macho, hii nadhan ni physiological toucher ambayo tutakufa nayo

User name yangu inareflect namba za Gari ambazo nadhan lilichangia pia kuniletea majanga. siku ya tukio tulivamiwa nyumba tatu mitaani, sisi tulikuwa wa mwisho kuvamiwa na Kutoka na maisha. nyumba moja walimuua baba na ya pili wakaumuua mlinzi, kwa maelezo ya wenzetu muuaji alikuwa yule yule aliyekuwa ananisulubu mie.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi mbona almost wote mliivamiwa mmejenga tu kuhamia unakutana na majambazi?

Kujenga kunaanza kuogopesha sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baba yangu mzazi, mzee isaki alikuwa mlinzi kanisani. Ule ulinzi kwamba siyo mgambo wala askari ni raia tu, miaka ya nyuma uaminifu wako ulikubeba.

kazi hiyo aliifanya zaidi ya miaka arobaini. Akamwambia mchungaji wa lile kanisa, nguvu zimeisha nataka nipumzike, mchungaji hakuona kama serious issue, ikabidi mzee aendelee na kazi huku anangojea aletewe mtu wa kumwachia kazi.

Mwaka 2001, pasaka jtatu kuamkia jnne, waliingia wezi,

Wakamuulia baba yangu, ndani ya kanisa, pale madhabahuni damu yake ilijaa pale hadi tunaenda kwenye ibada ya mazishi iko pale, ilikuwa huzuni kubwa. mzee alikuwa mpole sana.

Walikamatwa vijana ila mama akasema sitaki kesi, mzee wangu wameshamuuwa, waachieni Mungu anajua.

Walikufa vijana wengi pale kwetu wakiweweseka tulimuuwa yule mzee kanisani. Wengine hadi wazazi wao na ndugu zao walikufa.

Wezi hawafai.

So sad.

R.I.P. Paradise Baba na Mama!

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana laana ya Damu ilitembea juu yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuuh pole sana

Mke wako anakupenda sana tena sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Haa, akiona hii mama chanja atatamba balaa,!!! Ni mke na kama rafiki, simfichi kitu na siku Ile ndo aliyabeba maisha yangu haswa, uzuri alikuwa anajua kila kitu, ni kweli siku Ile sikurudi na pesa na alilijua hilo,

Sent from my BKK-AL10 using Tapatalk
 
siri kubwa ya dua yoyote kubwa hasa ya kudhulumiwa au kufanyiwa ubaya basi wakati unaifanya ufanye na watoto hasa watoto yatima wale wadogo kabisa then mwisho uwape sadaka na kwa kusudi kabisa kabla ya kuanza kusoma nao hyo dua waambie kilichotokea mpka wasikitike haswa then piga nao dua hali ya kuwa wanakuonea huruma na huzuni

Sent using Jamii Forums mobile app
Ok mkuu nashukuru sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni uongo tosha
Majambazi hawana muda wa kujibishana na wewe. Eti hela nimepitisha kazini

Majambazi hujawahi kutana nao.

Umesema uliwekwa uvunguni, akaletwa na HG naye uvunguni...
Baadae unasema Mdogo wako aliwekwa chooni na HG

Mkeo hujasema alikuwa wapi

Majambazi hawama sababu ya kurusha risasi kama hakuna kilichotokea nje ya eneo la wizi.

Majambazi sio wajinga una bastola wakuachie wakiwa wanaondoka.



Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, nisamehe. Nataka kujua tu; wewe ni jambazi?

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili la kutoka ni hatari na inabidi mtu uwe makini. Miaka ya nyuma kuna mwanajeshi mmoja aliuawa mitaa ya Tanki bovu. Nadhani huenda kuna members wanaojua hiki kisa. Walivamia sehemu, mjeda akatoka akakuta jambazi mmoja amebana kwenye michongoma. Akamwamrisha ''mikono juu''. Jambazi badala ya kunyoosha akamfyatulia risasi na kumuua palepale. Kwa upande mwingine nao watu wasipokuwa wanatoka majambazi na vibaka ndiyo hufurahi na kuonea huo mtaa.
Kutoka ni salama ikiwa tu nawe utatoka kama jambazi au komando, sio unatoka kilegelege. Hakikisha unajua mbinu za medani na zana za kujilinda unazo in case of anything na backup plan utengeneze kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka kipind niko primary sikumbuk mwaka vzr ila ni 200.., mama anakuja kuniamsha asubuh ananambia tumeibiwa mwanangu baada ya kuona mlango wa nyuma ambao haufunguliwagi upo wazi, namm nakurupuka kitandan namuamsha mjomba, sasa tukaanza kutafuta tumeibiwa kitu gani,pekua nyumba nzima sebuleni had vyumban hatuon tulichoibiwa,tukaenda uani ambapo kuna banda la kuku tukakuta baiskeli ya anko ndio imeibiwa,
Kesho yake usiku tukaita shehe walipiga dua usiku kucha ndimu zinachomekwa sindano na viwembe alafu zinawekwa katika chungu jikoni zinaanza kupikwa had alfajiri, haikupita wiki anko aliikuta baiskeli yake bugurun sheli imekaa tu, akakaa pale hadi usiku aone atakayekuja kuchukua lakin had saa 4 hakuna mtu, akiwauliza watu wa pale kila mtu haijui na hajamuona mtu akiiweka pale, akaichukua akarud nayo home.
Nb:Huyu alikua mwizi sio jambazi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila majambazi watu wabaya sana nina matukio kama matatu hivi.

La kwanza Magomeni mapipa miaka ya 2000
Nakumbuka nilikuwa na brother tunaelekea bakery saa mbili sasa kufika mtaa wa dosi tukagawana pale mimi nikaenda kununua Chips brother kaenda Bakery.
Balaa likaanzia hapo nakumbuka siku inayofata ilikuwa skukuu ya Iddi.
Wazee wa kazi wakaingia walilenga duka kubwa la mpemba jamaa mmoja akakaa kati kati ya njiapanda nne anamkanda kabisa wa risasi jamaa wakaanza kuvunja taa za duka wakaiba milioni 3 muuza chips mmoja sijui aliona sinema akaanza kupayuka sio risasi na kelele za muuza chips baruti hiyooo zikampa mori yule jambazi sitasahau alichokifanya alipiga risasi kwa yule Muuza chips alifariki hapohapo akageuka pande zote nne akawa anafyatua risasi wale wezi walikuja na cresta nyeusi walipomaliza wengine walipanda gari wengine wakatokomea kwa mguu huku wakifyatua risasi wakaenda kuvamia Bar.

Zile taarifa zilienea mda mchache watu wakiona gari nyeusi wanakimbia nakumbuka mimi nakaka yangu tulionana nyumbani cha kusikitisha tukio lilifanyika saa mbili usiku polisi walikuja saa tatu asubuhi kesho yake[emoji1] [emoji1]

Tukio la pili lilitokea 2012
Wezi walivamia sehemu tunayoishi nilikuwa na milioni 3 ndani harakati za vyumba za kupanga chumba changu kilikuwa mbele kabisa kinachofata kulikuwa cha mdada sasa wale wezi walimjia yule dada tu wakati nyumba ina vyumba sita zote master chumba cha tatu kilikuwa cha mwanajeshi walimtilia kufuli nje nilishtuka usingizini nilisikia kishindo nikaamka nikafungua pazia nikaona jamaa mmoja yuko nje mwengine anafanya uvamizi nikachukua simu nikawapigia wapangaji wenzangu wengine wakatoka madirisha ya aliminium yule dada aliumizwa vibaya ila vitu waliviacha badaa ya kuwahi kutoka nje majirani wenzangu baada ya upelelezi ikaonekana mwenye nyumba ndie aliefanya mchongo.

Tukio la tatu:
Nilivamiwa na wezi wakati natoka ATM karibu kabisa namaeneo ninayo ishi ilikuwa mapema tu saa tatu usiku jamaa walinisimamisha wakaniomba pesa walikuwa kama watatu hivi walinivamia nikapambana nao wakanishinda nakumbuka ilikuwa kwa lami kabisa boda zinasimama wananiuliza vipi wale jamaa wanasema tunamdai huyu mwisho ikaja daladala nikapanda nilipigwa sana na bisibisi na mabapa za panga wakafanikiwa kuniibia 400,000 nilizotoa Atm kurudi geto nikaawambia kilichonikuta kwa msaada wa rafiki yangu tukaanza kuzunguka Bar zote za karibu nikaja kuwakamata Bar maana nilimshika sura mmoja nikawapeleka staki shari ila kilichotokea polisi walikuwa wanachukua pesa kwangu na kwa wale wezi nikaamua kupotezea.

Naongezea tukio la mwisho magomeni
Wazee wakuvunja kwa jiwe wakafanya yao saa nane usiku walianza kuvunja chumba cha mzee walimtoa nje nakumsihi atoe pesa alikuwa mbishi walimpiga sana panga za kichwa mpaka akapoteza fahamu wakati wako namzee baadhi wachache wakataka kuingia chumba cha brother kilichomukoa ni kioo mlango ulikuwa wazi alijibanza pembezoni ya mlango akishika panga wezi wakamuona brother kupitia kioo kashika panga wakaamua kuondoka ikaskika jamaa anasema nimuona kashika panga kwenye kioo walifanikiwa kuchukua vitu vya sebleni walipoondoka usiku huohuo tukampeleka mzee hospital.
Mpaka leo brother anaitwa ** kioo.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha utani hamna kituo cha polisi kinafungwa.
Mecco sasa hivi wapo vibaka tu uhalifu wa namma hiyo haupo tena.
.
Huwezi kupiga risasi kiholela holela au kuvamia Mecco, Igoma, National kwa kifupi katikati ya mji ukatoka salama ninaandika nikiwa nauhakika wa 100% sehemu zote zilizokuwa na matukio ya kuvamiwa na majambazi zimedhibitiwa ukija hutoki Mecco, Kishiri, Katoro, Tarime, Kahama, Lunzewe na Geita
Kukiwa n Pesa wanaingia wanapora n kutoka kk.... Acha ubishi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hiyo mitaa ya buzuruga, memo, had I national vijana wezi sana. Mimi mwaka Jana mitaa niliyokuwa naishi national nyuma ya comfort hotel walinipulizia dawa wakaiba flat screen,jiko, nguo na via zangu kwenye nlishtuka SAA 3 asubuhi. Hata job nilishindwa kwenda sumu Kali sana ile.
Pole mkuu kumbe we Ni jirani yng

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu wana roho mbaya sana ,natumai nae alilipwa kwa upanga.
Mwaka 2010, nyumbani tulikuwa wawili tu, mimi na mama watoto,tu na wakati huo tulikuwa hatujaanzisha familia bado.

Nilirudi nyumbani mapema Sana siku hiyo mida ya saa 12 jioni tu, baada ya kula mapema pia nikaenda kujipumzisha mapema pia, saa nane usiku nikasikia milio ya bunduki, nikahisi hapa tushavamiwa, Jana yake tu nilikuwa nimetoka kuchukua kagari Ka kutembelea( T blj), nikajua pengine ndo wanafata Hilo Gari, kwa hiyo si kuwa na idea kama wangeweza kunidhuru kwa kuiba Gari ambalo lipo nje na wangeweza kuwasha tu hata kwa funguo Malaya na kuondoka. Nyumba haikuwa na fensi

Kulikuwa na ukimya wa kama dakika moja, nikasikia tena milio mkubwa Sana maeneo mlango wa sebuleni na wa jikoni kwa pamoja! Sekunde kadhaa tu wakawa tayari wanavunja mlango wa chumba changu!

Muda wote huo wife anahangaika kujificha chini ya uvungu bila mafanikio, ni kibonge flan, so zoezi Zima la yeye kuingia huko halikuwezekana,mpaka jamaa wameingia nilikuwa Sina clue, yaan wakanza straight na mapanga mwilini,, toa pesa!toa pesa! Tunajua umezificha, chumbani walingia kama watu watano,wawili ni heavy kiasi kwamba nikahisi hapa nikijaribu kufurukuta napotea, watatu wa kawaida tu ningeweza kupambana nao kama wasingeambatana na Hao heavy duty, nikaona ni comply tu yaishe!

Mapanga yalitembea takriban dk 5 mfululizo, wife ndo alikua mtetezi wangu analia kwa kuwaambia kuwa Leo huyo baba hajaja na hela, an gekuwa nazo angewapa, kiukweli Nina kawaida ya kumkabidhi wife kila siku kile nilichokuja nacho nyumbani, na siku hiyo kweli si kuwa na pesa niliyokuja nayo nyumbani, kulikuwa na laki mbili tuu kabatini ambayo ilikuwa kama balance ya dharula wakaichukua

Momment ambayo Hua inaniumiza hadi Leo, ni kuna mmoja alikuwa amepania kuniua kabisa alipiga panga mbili Moja ikaingia haswa, ya pili nikasema ngoja nikinge, ikaondoka na kidole kimoja, baadaye akanitupia taulo huku akisema jifunike sasa nakata shingo hapo nadhan ufahamu wangu ndo ulifika mwisho,

Wife alikuwa anaona kila kitu anasema baada ya tukio la kunitupia taulo alipiga panga mbili ambazo alikosa zote, ikawa wenzake wanamuita kwa code ndo pona yangu, nililala hapo chini huku nikiwa Sina fahamu, hadi nilipokuwa kusikia sauti ya wife aliniambia mume wangu kama upo hai amka wamesha ondoka,!! Ni sauti ya huzuni kabisa kuwa hi kusikia Kutoka kwa mke wangu, anasema alijaribu mara kadhaa Kuniambia hivyo, Lakin si ku respond akajua nshapotea. nadhan mungu tu alikuwa upande wangu siku hiyo.

Hawakuchukua Gari ambalo nilidhani ndo liliwaleta, kilichofata nilikimbia nyumba na kwenda kupanga Tena mana niliona haikuwa bahati yangu kujenga, ila Nilirudi baada ya kupata Familia, na nipo hadi sasa ila nina makovu kichwani na kidole kimoja Sina, plus mimi. Na wife kila ikifika saa nane usiku automatically tunakua macho, hii nadhan ni physiological toucher ambayo tutakufa nayo

User name yangu inareflect namba za Gari ambazo nadhan lilichangia pia kuniletea majanga. siku ya tukio tulivamiwa nyumba tatu mitaani, sisi tulikuwa wa mwisho kuvamiwa na Kutoka na maisha. nyumba moja walimuua baba na ya pili wakaumuua mlinzi, kwa maelezo ya wenzetu muuaji alikuwa yule yule aliyekuwa ananisulubu mie.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa hapo kwake Buzuruga kwa nje ndipo ulikuwepo uwanja wetu machalii wa kucheza mpira miaka hiyo mtaani.

Ninamfahamu yeye na familia yake vizuri.
Dahhh....
Nimemkumbuka marehemu Rasta flani pale alikuwa anavuta bange na kuiuza aiseeeee....
Nakumbuka mdogo wake Rasta pia aliitwa Paul alifariki mkuu...
Dahh, yule mama mwenye iliyokuwa Baxtan alijikuta anapoteza wanawe wote wakiume

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baba yangu mzazi, mzee isaki alikuwa mlinzi kanisani. Ule ulinzi kwamba siyo mgambo wala askari ni raia tu, miaka ya nyuma uaminifu wako ulikubeba.

kazi hiyo aliifanya zaidi ya miaka arobaini. Akamwambia mchungaji wa lile kanisa, nguvu zimeisha nataka nipumzike, mchungaji hakuona kama serious issue, ikabidi mzee aendelee na kazi huku anangojea aletewe mtu wa kumwachia kazi.

Mwaka 2001, pasaka jtatu kuamkia jnne, waliingia wezi,

Wakamuulia baba yangu, ndani ya kanisa, pale madhabahuni damu yake ilijaa pale hadi tunaenda kwenye ibada ya mazishi iko pale, ilikuwa huzuni kubwa. mzee alikuwa mpole sana.

Walikamatwa vijana ila mama akasema sitaki kesi, mzee wangu wameshamuuwa, waachieni Mungu anajua.

Walikufa vijana wengi pale kwetu wakiweweseka tulimuuwa yule mzee kanisani. Wengine hadi wazazi wao na ndugu zao walikufa.

Wezi hawafai.

So sad.

R.I.P. Paradise Baba na Mama!

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana mkuu.
 
Back
Top Bottom