Nikiwa mwaka wa kwanza UDSM kwenye uwanja wa mazoezi kampasi ya mlimani yalinikuta mazito.Nikiwa nafanya mazoezi ya kukimbia na kuruka kama chura kuzunguka uwanja akanijia mrembo.Wajihi wake ulipendeza.Mfupi hivi,kiswahili chake cha daresalama,rangiye maji ya kunde.Akanisabahi huku makalio yake makubwa yakitetema...haraka maungo yangu yakatetema!kijana wa kinyakyusa matatani!Nikajiwazia hawa sio wakina Atuganile niliowazoea!Kavaa suruali njiwa ya Mpira ibanayo...ikayanasa vema makalio yake!Basi bwana tukaanza kupasha,jinale Anna akinijuza na kuwa anachukua shahada ya kwanza ya uhasibu mwaka wa pili!Soga likanoga huku tukipasha,mie nikimwacha atangulie mbele kwa spidi ndogo huku nikiifaidi rasilimali makalio!.Bwana wee akadai eti Mimi nikitoka mazoezini na baba huwa ananinunulia aishi kirimu....wakati huo namwona muuzaji wa bidhaa hizo akirandaranda na kibaiskeli chake....hohooo!nikamwambia nawahisha funguo rumu nikakimbua haswaa....sikuwa na fwedha za mzahamzaha.