Tukutane hapa wapenda ujasiriamali

Tukutane hapa wapenda ujasiriamali

Kumbe yanapatikana ya mtumba pia?
Mimi niko mkoani naweza pata mawasiliano ya muhusika yeyote unayemfahamu hapo tafadhali?

Vizuri zaidi ukamtuma mtu wako wa karibu akaenda kuangalia na kufanya mawasiliano

Yapo ya mtumba na kuna mafundi humo humo wakurepair

Pia unaweza ukashona
 
Hivi vitambaa vya mapazia ili ushoneshe vinapatikana mitaa gani dada
 
Kwa hiyo Pisikali naweza kuchukua kitambaa cha Mapazia na nikashona kwa mitindo kama Hiyo kwenye picha zako na je vitambaa vinapatikana maduka mitaa ipi
 
Ilala sokoni saa 10 hadi saa12 alfajiri kila siku wanafungua mabalo ya nguo (jeans magauni nguo mchanganyiko) nguo hadi 1,000/500 nzuri tu

Nguo zinazouzika sana it depends na wateja wako kama watu wa makazini basi magauni sana, jeans pia zinauzika ziwe tu nzuri na bei inayoendana na hali ya nchi[emoji1][emoji1] affordable

Blouse pia, shifon nzuri nzuri ukiwahi asubuhi sana unakuta nguo nzuriii blouse unanunua hata jero na nzuri hatari wewe usiuzie tamaa, uza 5,000 au 3,000 tu
2,500 ni faida kubwa sana hapo ukiuza blouse kumi unafaida ya 25,000 per day (sio kila siku)

Mapochi pia
Blouse ndio mashati ya kike hivi mkuu yanapendwa haya
 
Hivi vitambaa vya mapazia ili ushoneshe vinapatikana mitaa gani dada

Mitaa ya kkoo inanichanganya majina ila mtaa wa mapazia ni aggrey na swahili utaona tu nje mtaa huo umejaa mapazia ingia ndani waambie nionesheni sampo za vitambaa vya mapazia unachagua unanunua (zunguka maduka hata matatu angalau) nunua urembo mwenyewe fundi kazi yake kutoboa kuweka urembo na kuyapinda basi (2,000 tu) kwa pazia moja

Wengi wanashona nzito mita 1 na nusu (2)nyepesi mita mbili, wengine mita 2 kwa madirisha makubwa

Ila madirisha ya futi 6, yani pazia la 3/4x6 unakata hata 1 na robo mara 3
 
Kwa hiyo Pisikali naweza kuchukua kitambaa cha Mapazia na nikashona kwa mitindo kama Hiyo kwenye picha zako na je vitambaa vinapatikana maduka mitaa ipi

Curtains?? Ni tofauti unachagua urembo na dizaini unayotaka kama simple au yenye manjonjo mengi pia mshirikishe fundi atakushauri maana ndio kazi zao
 
Nasubir hili jibu + vitambaa za mito kama aliyopost

Kingsmann

Mito, kuna vitambaa vya mapazia vya maneno such as gucci, i love you unakata unashona au plain

Vya maneno mengi vinapatikana kwa habby kkoo ukifika sokoni tahfif mtaa unaofatia ulizia kwa habby au wanapouza foronya hapo hapo mwambie nataka kitambaa unachagua unachotaka, ukitaka kushona hapo hapo au kwingine

Foronya kushona ni 1,000 zipu kuna za 2,00 kwa 5,00

Nb: wanakuangalia wakikuona wakuja UNAPIGWA!
 
Shukrani sana mkuu

Kingsmann
 
Back
Top Bottom