Mimi binafsi sio mtumishi serikalini ila ntachangia machache ninayoweza wakuu
Kwanza, ukiajitiwa iwe serikalini au sekta binafsi usikimbile kuoa au kuolewa, au kuzaa mtoto au watoto. Wekeza kwanza kwenye uchumi angalau miaka 5 nipo uanze hayo mengine.
Pili, ukiajiriwa popote ple usibadili mfumo wako wa maisha kwa zaidi ya 40%,ni kweli ulikwa umechakaa sasa unatakiwa upendeze kiasi na ule vizuri ila sasa unapoanza kutoka usiku kwenda club au bar kisa una uhakika wa mshahara ndipo unapoanza kuharibu uchumi wako.
Tatu, unapoajiriwa popote pale jitahidi sana kuona fursa za kiuchumi nje ya ajira zichambue kisha kusanya mtaji wako baada ya miaka miwili anza kuifanya fursa moja wapo.
Nne, kamwe sinunue gari la mkopo hata kama utashawishiwa vipi hapo kazini kwenu. Ukiona unanunua kwa mkopo jua huwezi kulimliki hilo gari fuata kanuni ya nunua kitu unachoweza kukinunua mara mbili.
Mwisho kabisa, uisubiri ukastaafu ndipo ukaanza biashara yoyote, hautaiweza. Kama umeshastaafu au unaelekea kustaafu na una vijana wakubwa fanya utaratibu wa kufungua biashara ya familia wewe usimamie fedha wao waifanye hiyo biashara na muheshimianekama wafanyabiashara sio baba/mama na wanawe maana mtafeli.
Vikubwa vya kuepuka ni;
1. Starehe
2. Kuiga maisha ya watu
3. Uwizi kazini
4. Kuridhika na mshahara