Tukutane hapa watumishi ambao hawategemei mishahara, tuelezane changamoto na mbinu

Hebu fafanua kidogo kuhusu hiyo Kampuni kama haina longolongo. Ofisi zao kwa Tanzania zinapatikana wapi?

Na hizo bidhaa ni used, au ni brand new?
 
Ahsante ingawa Ww mkuu unaongea theory sana kuliko mtoa mada, Yeye kaonyesha vitu vinawezekana. Vyako ni vigumu kutekelezeka cause sometimes family inakuja automatically hata kabla ya kazi so tell us what we can do after.....
 
Mimi sio mtumishi mkuu, ni wapi huko kuna mabonde hawategemei mvua ili tukalime...
 
Mkuu hizo Habari unaingia hapo unawauliza Kuna namba ya simu ya Japan na Tanzania

Misiwezi kuwaelekeza watumishi wenzangu sehemu ambayo sio sahihi
Hapa sasa ndiyo umenipa walau mwanga wa kitu cha kufanya.
 
Nami nasubir ukianza kutoa Elimu ya hiyo company
Hapo kuna platforms ambazo wauzaji wa bidhaa wakikwa sehemu mbalimbali ikiwepo Japan South Africa Dubai Tanzania wamejisajili pale kwenye online platform wengi ni Watanzania wanaushi nje ya nchi na wanatangaza na kuuza bidhaa zao kupitia pale.

Unaweza kumtafuta seller moja ukamwambia unataka nini akakutafutia kuweka order Kisha ulalipa kwa njia za kawaida bank kama CRDB NMB au kwenye simu unaingia kwenye menu unachugua kampuni unalipa

Ukifanya malipo weka kumbukumbu namba ya Jina unalotumia kwenye website yao.

Mizigo ikijaa wanapakia kwenye container wasafirisha na kule huku Kisha wanalipoa ushuru wa custom wanakupigia unawapa maelekezo mzigo wako utafikaje
 
Safi sana mkuu!

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Hili tangazo
Hili ni Tangazo tu kama matangazo mengine..
 
Mimi sio mtumishi mkuu, ni wapi huko kuna mabonde hawategemei mvua ili tukalime...
Inategemea na ulipo mkuu ufanye survey, Mimi nipo kigoma kusini Kuna sehemu wanapaita njia za maji..mwambao wa ziwa Tanganyika.
 
Vijana subilia niwambie msiishi katika nadharia suala la kujikwamua kiuchumi ni wazo zuri Ila mtambue mafanikio si kwa wote Kwenye kila jambo iwe siasa, biashara, elimu nk hapa tuambiane ukweli watumishi wengi wa umma huingia katika huu mtego wa kuamini wakikopa wakiwekeza kwenye biashara ndio njia sahihi ya matumizi ya mkopo Ila akikopa akinunua kiwanja au akijenga si njia sahihi, anasahau yeye kashapoteza umri kwenye kusoma nk

Kipindi wewe upo shule wenzako wapo mtaani Wana pitia uzoefu na changamoto za biashara so wanaheshimu kipato Cha biashara sababu ndio ajira zao ndio elimu zao Kama wewe unavyotamba na ujuzi wako so nachotaka kusema nini

Vijana wa Sasa mnao ajiliwa mnaharaka na maisha hizo haraka haraka zenu ndio unajikuta unakosa vyote na kuona ajira haina maana bora biashara kwanini unataka biashara sababu uijui unataka kilimo kwa sababu ukijui kuwa uko napo Kuna changamoto zake hivyo basi Kama wewe mtumishi wa umma usikope ukabeti pesa ya mkopo kwenye biashara narudia usikope ukaenda kubeti kwenye biashara utalia nachokushauri

Kopa mapema pesa kidogo kwa mda mdogo nunua kiwanja, samani za ndani tulia utachekwa Ila tulia ishi usiwe na haraka na maisha kikubwa uhai sawa, tulia mkopo ukiisha huo wa miaka miwili, kopa tena miaka mitatu endeleza kiwanja chako inua boma lako mpaka usawa wa kupaua, tulia ishi, kula vizuri vaa vizuri achana na story za ujenzi hiyo miaka mitatu ipite, sawa miaka mitatu ikipita mkopo wako ukiisha nenda sasa kakope ule mkopo wa kinua mgongo yani mkopo wa miaka nane vuta mzigo wote Kisha nenda kapaue nyumba yako weka milango madilisha piga ripu, weka umeme, maji Kisha hamia kwako, ukishamia kwako hapo Sasa ndio anza kamali na pesa zile za top up million tatu nne unapeleka uku ikipotea unatulia unatafuta nyingine tena sijui kwenye kilimo nk yani unabeti upo kwako kumbuka hapo upo kwako ndani ya miaka mitano ya ajira ujaishi kwa shida ulikua unafurahia maisha na una mipngo yako na upo kwako so ndani ya miaka kumi utaishi katika ndoto zako cause una mji wako pia una deal zako zinazokupa pesa ya kusukuma maisha

Sasa wewe chukua mkopo wa kinua mgongo yani mkopo wa miaka nane kabeti kwenye biashara au kilimo hiyo pesa kikipotea uko majanga unatulia miaka Saba unakopa tena inaanza plan zako kumbuka hapo yule mwenzako aliyekopa kidogo akaanza na ununuzi was kiwanja ndani ya hiyo miaka Saba ambayo wewe ulibeti yeye yupo kwake na anafanya ambacho wewe ukitaka awali kikaferi, na hiyo miaka Saba mwenzako aliishi vizuri bila stress maana anajua pesa ilienda wapi Ila wewe una stress maisha pesa huna maisha huna

Asikwambie mtu maisha ya kibongo makazi Yani nyumba kwanza ambao hawamini nyumba kwanza wanazo nyumba za urithi za baba zao na mama zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…