Tukutane hapa watumishi ambao hawategemei mishahara, tuelezane changamoto na mbinu

hapa mtumishi nina buku tatu mfukoni,nikienda leo home ,kesho nguvu ya kuamka ni kudura za muumba,bahati nzuri home mazaga yapo watoto watakula.
Biashara zimekuwa ngumu sana,kiufupi kuna upepo flani mgumu
Upo mjini au kijijini

Sema nikupe formula
 
P
Pesa haziwatoshi watumishi wengi kwasababu wanatumia matumizi makubwa kuliko vipato vyao, mimi nimewashuhudia wengi, take home yako laki sita, unataka unywe pombe na genge lako, unataka ubadilishe pisi kali kama matoleo ya simu mapya yanavyokuja, unataka usomeshe watoto wa shangazi, mjomba, bamkubwa, bamdogo.

Na ndugu nao hawaangalii kuwa una majukumu na mishahara ni midogo, wakijua tu umeajiriwa basi umeumia, kila mwezi lazima wakupige vizinga kila mtu kivyake, hajui kuwa mpo wengi.
 
Lakini umeleta Uzi mzuri kwakweli.
 
Mtu akiajiriwa akae miaka mitano ndo aoe dah, je kama kaajiriwa akiwa na miaka 35, akae miaka mitano?
 
3. Uwizi kazini
Kwa Kazi za serikali bila hili HUWEZI KUTOBOA.

4. Kuridhika na mshahara
Ukiridhika ndio unaukaribisha UMASIKINI.

#YNWA
Nyie ibeni tu, kumbuka kuna kufungwa na kufukuzwa kazi.
 
Hicho ndo tulitaka kukisikia, ahsante. Then hizo bidhaa wewe ndo unaenda kuziuza? Na biashara hiyo inafanyika kila mkoa hapa Tz au ipo limited na baadhi ya mikoa?
 
Kijana umetoa ushauri mzuri sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…