Tukutane tunaomiliki magofu kwa ajili ya kufarijiana

Hivi sifa ya jengo kuwa gofu nini?
 
Ulianza Dharau kwa kuita Nyumba Kibanda
 
Nikikumbuka nacheka sana.... Nyumba yangu nikajenga hadi kwenye renta nikapumzika mwaka 1 nikarudi tena nikapua nikapumzika miezi 6 nikahamia kibishi...
Kilichokua kina niumiza ni zile safar za kila wiki lazima niende kuangalia tu nilipoishia, nilikuwa napata hasira na kupata pesa huoni hata dalili... Sometimes naenda kwa kujificha maana nilikuwa naona aibu majiran watasema yule jamaa kila mara anakuja kuiona nyumba kama vile ipo hospital au jela...
Nilikutana na maza fulani akaniuliza wewe kijana hio ni nyumba yako? Nikamjibu ndio, nilimuona aneshangaa na kufurahi akaniambia ni vijana wachache wanaweza kufanya ulichofanya na wapo watu wazima wanakaribia hata kustaf hawana hata kiwanja... Akaniambia sasa umeshapaua ukitaka uhamie kibishi wewe uwe unaitembelea nyumba yako kilasiku, yaani fanya kama unakuja nyumban kwako najua itakupa akili ya ziada... Maneno yake yalinitia nguvu Mungu ni mwema nikaokoteza pesa kidogo by that time nikanunua magril nikapiga maturubai, nikanunua malango wa mbele na nyuma temporary ya bei rahisi, nikapiga rafu chini nikahamia kibishi...
The rest is history 😊🙏
 
Kuna uncle wangu alikuwa anafanya biashara ya duka la urembo na bidhaa nyingine nyingi tu biashara ilikuwa bora sana lakini sijui aliwaza nini akaenda kujenga aiseh
1.biashara ili shuka mpaka kuisha kabisa
2.alipata msongo wa mawazo sana
3.alianza kuwa kama chizi mara nyingine
4.Alifariki sikujua nini lakini madaktari walituambia tuzike mapema najua itakuwa alikunywa sumu maana tumbo lake lilianza kuvimba

Naumia sana kukumbuka haya
 
Duuh pole na hongera kwa kumaliza sometimes inakosesha amani kuona boma linakaa miaka nenda rudi kwa wafanyabiashara tunasema tumezika pesa
 
Hongereni jamani kujenga moaka hapo ni hatua kubwa
Mimi mwenzenu nilikimbiza nyumba mpaka Renta ndani ya miezi 4 hiyo mwaka 2012 then nikapiga bati na grill na milango huo huo mwaka. Mpaka leo sijamalizia
Maana kipindi hicho hela ya ufuta ilikubali sana yaani. Nikalima hekari 120 mwaka unaofuata ili nimalizie na kuhamia ila nikavuna gunia 6 tu.
Anyway ndio maisha
 
Mungu ampe pumziko la milele kafa katika ujenzi wa taifa
 
Pole mkuu ni changamoto sio ya kitoto biashara ikiporomoka kila kitu kinaharibika ni kama unaanza upya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…