Bachelor ll
JF-Expert Member
- Dec 15, 2019
- 4,106
- 6,678
Sawa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pole saanamimi alikufaga he was so caring, loving, protector nlimuweka miaka mi4 anasubiri bikra yangu na aliweza bila kubadilika,. tulipanga mengi ya baadae ajali ikamuondoa , kazi ya Mungu haina makosa, endelea kupumzika kwa amani
Ishu sio kupata mzee ishu utayari unapata mke wakat life lako halieleweki kula kwa mdingi mda wowote utaondoka dar kwenda depo mafinga jktWazungu wanasema " you will never miss your water untill your well gets/become dry, yaani umuhimu wa maji huja baada ya kisima kukauka.
Nakumbuka nikiwa mwaka wa kwanza wa masomo yangu katika moja ya chuo kikuu hapa nchini niliwahi bahatika kupata " a well raised woman '' unfortunately, sikutambua thamani yake mpaka nilipopata vibaka wakunipuna na kunivunja moyo wangu.
Siwezi kusahau, upole, utu, upendo, heshima na tabia ya kujali kwa yule dada. Vijana wenzengu wife material huja mara moja kumpata tena nimajaliwa.
Kama uliwahi pata wife material kisha ukaleta usela leo unalia kwa uchungu kupoteza bahati dondosha coment yako hapo chini.
Pole sana mkuuUmenifanya nikamkumbuka Mrembo wangu wa Kisukuma, Mweupe aliyebarikiwa uzuri wa asili, mcheshi, mkarimu, mnyenyekevu, ana moyo wa utoaji, mchapakazi, alikuwa na mapenzi ya kweli. Mungu ampe mafanikio pale alipo. Ni kweli mpaka dakika hii bado sijawahi kubahatika kukutana na almasi kama ile.😔..You're still in my heart Aggy.
Akili yako inakuchezea tu mkuu. Kina Eve na mama mtoto wako wapo wengi mno, tuliza akili, jichanganye sehemu sahihi, furahia maisha then utakutana nao.Baada ya kuachana na mama mtoto wangu ambaye nilifahamiana nae kwa zaidi ya miaka 10+, nilibahatika kupata mpenzi mpya anaitwa Eve, Alinipenda sana huyu dada alijitahidi kunifanyia kila kitu mwanaume anastahili kufanyiwa, Ila deep down I was broken. Nilitumia muda mwingi sana kumfikiria mpenzi wangu wa zamani na sio yeye. Pia kipindi tuko kwenye mahusiano nae nilitumia muda mwingi kuwekeza hisia zangu kwa wanawake wengine, Nilimcheat kitu ambacho sikuwahi fanya kwa mama mtoto wangu. Yani aliona kila rangi yangu mbaya ya kuonyesha kutojali. Baada ya kumfanyia vituko vyote hivi, Kuna siku nikawaza tu umri umeenda nilikuwa nakaribia miaka 30, Pia kipato kilikuwa kinaruhusu basi nikamuingizia swala la ndoa. Lakini kiukweli huyu dada hakuwahi jua kama nilikuwa na mtoto huko nyuma na aliwahi niambia kuwa hawezi olewa na mwanaume mwenye mtoto wa nje kipindi tunaanza mahusiano, sema kwa kuwa lengo langu lilikuwa kupata utelezi sikumwambia kipindi kile. Baada ya vituko vingi sana, na kumwambia na mtoto huyu dada hakutaka kabisa ndoa na mimi, alipomaliza chuo tu akaomba tuachane kwa amani. Toka nimeachana na huyu dada yani kila mahusiano nayoingia hayaeleweki badala tena ya kumuwaza mama mtoto wangu sasa hivi namuwaza Eve, Yani circle imekuwa ile ile. Kauli ya huwezi jua thamani ya ulichonacho mpaka kipotee ni kweli, Natamani ningejua thamani yake mapema.
Kuna muda natamani dunia ingekuwa inarudi nyuma, ila ndio hivyo haiwezekani.
Nimegundua hilo mkuu. Nimepata kazi mkoa mwingine, Kesho nasafiri naamini huko akili itaniruhusu kuanza upya. AhasanteAkili yako inakuchezea tu mkuu. Kina Eve na mama mtoto wako wapo wengi mno, tuliza akili, jichanganye sehemu sahihi, furahia maisha then utakutana nao.