Tukuyu, Rungwe Mbeya wilaya ya kipekee sijaona Tanzania

Umenena vyema nimeishi Tukuyu miaka 14 ni sehemu ambayo naipenda mpaka kesho japo mimi ni mchagga

Kwa upande wa mkeka(lami) barabara ni nadhifu sikuwahi kuona lami ikiwa imetoboka kuna shimo kama nayoyaona kwenye lami za Dar😁

Hali ya hewa ni nzuri sana,wilaya imepangwa ikapangika
 
Hiyo elfu 5000 ya Mkugnu ni nyepesi kwa Wewe unaye safiri Tour huku umejiandaa Wallet iko safi.

Kwa wakazi wa hapo maisha yao hapo hiyo elfu tano kuipata ni mbinde.

Hata wewe tukikwambia ukae hapo Mwaka mmoja, wiki ya kwanza utakula Kitimoto na Mindizi ya kwenda.

Wiki ya pili hadi mwezi unaanza kula nyama ya ng'ombe baada ya Miezi sita utaanza kumiss dagaa na maharage kumbe Walet imeanza kusinyaa
 
Unachosema ni sahihi. Hali ya Lushoto na ya Tukuyu vinafanana Sana, na hata mazao, yanafanana...
 
Hatujakimbia, pamoja na kiwa niko Seattle Washington, home ni Mwakaleli Tukuyu. Last time nilikuwa huko June 2022. Tumetoka ili Kuja kutafuta then tunarudi home kuwekeza...
Home sweet home..
 
Sawa
 
Sasa hivi nchi inahitaji wawekezaji, msikilize Dr.Mahenge wa TIC, wawekezaji sio lazima wawe wazungu, ukiwa na idea ipeleke, au tafuta watu wenye pesa share idea yako, waeleze ni vipi uwekezaji utaleta pesa,mkielewana sawa ukiona hawaelewi Tafuta watu andika proposal peleka TIC wawekezaji wanakuja kibao, wanaweza kuiuza idea yako na ikaleta manufaa, kwa taifa na kwako labda.
Usilaumu tu, labda hawaelewi cable cars ni nini.
 
Umeua ule mji ni wa kipekee kuna miti fulani imeteshwa mle karibu na chuo cha ualimu na maeneo mengine pia ipo madhari yake ni ya kuvutia sana, ukija mashamba ya chai pia yana madhari nzuri mno, wapiga picha, wacheza muvi na watafuta location wengine kuna kitu Tukuyu, watu wakule ni wakarimu sana, mvua zinanyesha kila mda, radi za nguvu Ndo usiseme, kipimo cha mche ni bakuli fulani(ndonya[emoji847]), nyumba za ibada kila kona watu wanasali sana Mungu awabariki Tukuyu Nitarudi tena[emoji1544]
 
Okay mkuu,nchi kwa sasa HAINA PESA, ila tuna mapesa ya kununua V8s kwa CEOs kwa well connected guy's, nani owner wa UDA na Nyati cross border transporters?
 
Hakuna wilaya isiyokuwa ya kipekee Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…