Tukuyu, Rungwe Mbeya wilaya ya kipekee sijaona Tanzania

Tukuyu, Rungwe Mbeya wilaya ya kipekee sijaona Tanzania

Huu mji sikuamini nilinunua ndizi za buku nikapewa fuko zima.! Nikamwambia muuzaji nataka ndizi za buku sio za elfu saba ! Abiria wakanicheka sana wakasema hizo mbona kakupunja amaekuona mtu WA dar
Hivi zile ndizi zenye rangi ya purple bado zipo hapo Tukuyu?,ni muda mrefu sijaziona hizi ndizi ,ni ndizi nene hivi na zinaliwa zikiwa mbivu
 
Nilibahatika kufika Tukuyu Mbeya ule mji Ni moja ya wilaya zilizobarikiwa kwa kuwa na mandhari ya kipekee Sana, Hali ya hewa ya kule uko cool mda wote. Vyakula Sasa ushindwe wewe na tumbo lako.

Zaidi maji Safi ya mito na bomba yasiyo na Mita. Lita ya maziwa 600, wapenzi wa kitimoto, kilo 6000, mkungu wa ndizi 5000. Sijui wanyakyusa wanaokimbia kwao wanashida gani???????? Wanyakyusa majibu tafadhali.........................

Wewe kwenu kukoje? Usiogope nyumbani ni nyumbani.
Picha mkuu muhimu sanaaaa
 
Tukuyu pako poa sana nilienda huko uakweni japo wako town kabisa karibu nyuma ya stend ya tukuyu ila nimetembea sana maeneo mengi ya tukuyu kule maisha ni rahisi sana hasa swala la chakula ila nilichogundua mzunguko wa pesa sio mkubwa kivile ila km umewekeza sehem na unataka sehem ya kukaa ule uzee vizuri tukuyu ni safi kabisa sema likianza baridi dah...km uko Russia
 
Tukuyu ni green mwaka mzima hawajui vumbi,maji utiririka mwaka mzima.
Wanyakyusa wao na dini tu wamestaaraabika hawana mambo ya kishenzi.
Kuna muda vumbi linakuwepo vizuri tu,enzi hizo tunatoroka rungwe boys tunaenda mnadan kiwila,halafu Kuna utofauti mkubwa sana wa wanyakyusa wa tukuyu na kyela

Sent from my Infinix X693 using JamiiForums mobile app
 
Aerial view photography.....hapo ni landmark..... round about ( kipreft[emoji1])

huo mkeka mweusi ni road mpya inayoenda kuunganisha na busokelo.....lwangwa
IMG-20230425-WA0003.jpg


Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom