Tulia Ackson aache upotoshaji, Kiti cha Naibu Spika kiko wazi kikatiba

.......Sheria iliyotungwa na bunge....
haya maneno mbona Unayaruka!!??? Tulia yupo sahihi usikitazame hichi kifungu kwa mrengo wa kichama Hakuna Sheria inayomzuia naibu spika kugombea kiti cha uspika
Ahsante sana...

Nimeshangaa sana watu wanashindwa kuona hiyo phrase... wanadhani imewekwa kwa bahati mbaya!

The problem watu wameweka akili yao YOOOOTE kwenye katiba huku wakisahau almost kila Ibara, inatungiwa sheria zake na ndo maana kila ibara kwenye katiba kushito wanataja sheria inayo-govern ibara husika!!
 
Kwa kuchukua fomu ya uspika maana yake ameshajiuzulu nafasi yake ya unaibu spika au?
 
sukuma gang mnahali mbaya sana aisee
 
Katibu wa bunge halioni hilo? au na yeye ni pangu pakavu kwenye Sheria na katiba?
Hako kadada ni karoho na kalafi sana,kanaweza kutemea mate chakula ili wengine wasile
 
Kwa kuchukua fomu ya uspika maana yake ameshajiuzulu nafasi yake ya unaibu spika au?
Naona hujajibiwa...

In short, Tulia hajavunja Ibara yoyote ya katiba wala sheria yoyote!

Ipo hivi...

Ibara karibu zote huwa zinatungiwa sheria! Sasa hiyo Ibara aliyoiweka Yericko, moja kwa moja inamkataza Waziri na Naibu Waziri kugombea Uspika! Hata hivyo, ibara husika haijasema chochote kuhusu Naibu Spika kukatazwa au kuruhusiwa!

Lakini kama nilivyosema hapo awali, karibu kila ibara hutungiwa sheria na ndo maana ibara husika inasema:-
Waziri, Naibu Waziri au mtu mwenye madaraka ya aina nyingine yoyote itakayotajwa na Sheria iliyotungwa na Bunge kwa madhumuni ya ibdara hii, hataweza kuchaguliwa kuwa Spika.
Hapo maana yake ni kwamba, Waziri na Naibu Waziri, kwa mujibu wa katiba HAWEZI kuchaguliwa kuwa Spika!! Wengine waliozuiliwa KAMA WAPO, basi watakuwa wametajwa na na sio Katiba. Kwahiyo mtu akitaka kusema fulani na fulani ambao sio mawaziri/manaibu waziri hawaruhusiwi kuchaguliwa kuwa spika, wanatakiwa kuonesha Sheria #12 ya mwaka 1995 Ibara ya 15, na sio katiba tena kwa sababu katiba, hususani kwa kifungu husika, kinamkataza Waziri na Naibu Waziri TU!
 
Unaharaka na papara sana
Dr. Tulia anagombea Uspika wapi?
 
Haiwezekani mtu anavunja katiba na anaachwa tu na wanasheria wapo na chama chao kimekaa kimya.

Tabia hii ya kuwaacha hawa waarifu wa kikatiba ndio inafanya tuwe laugh stock of East Africa,mko wapi wanasheria?

Pelekeni hii kesi mahakamani ASAP!
Tumia akili kidogo ndugu yangu na uuache mihemuko- Tulia anagombea Uspika wapi? au ameomba kuteuliwa ili akagombee Uspika- Una fail wapi?
 
Tumia akili kidogo ndugu yangu na uuache mihemuko- Tulia anagombea Uspika wapi? au ameomba kuteuliwa ili akagombee Uspika- Una fail wapi?
Hiyo process tu ya kupitia kwenye chama inamuweka kwenye orodha ya wagombea.

Ina maana akiingia bungeni tayari anakuwa ni mgombea,kaimu na naibu spika! Na katiba hairuhusu ata kwa dakika moja mtu mmoja kuwa ivyo,maana najua wajinga wengi wanatetea eti atajihudhuru ndani ya bunge,tayari ni kosa!

Ungelijua hili usingeandika tu km headless chicken
 
Unahaki na maoni yako- ukweli unabaki pale pale Tulia hagombei Uspika bali anaomba kuteuliwa kugombea Uspika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…