Tukio la Mashabiki wa Simba la kuingia na Jeneza Uwanjani limewakera wanaoitwa Maaskofu na viongozi wa Dini , na tumeshuhudia matamko kadhaa kutoka kwa Askofu wa Kikatoliki Kilaini na Mzee wa Mkono wa Baunsa , Gwajima .
Sijaelewa kilichowatoa mafichoni , kama ni Ushabiki wao kwa Yanga au ni kwa sababu ya Jeneza , na au labda nifahamishwe kama watu hawa wameingia nchini Tanzania Wiki iliyopita , vinginevyo nitawashangaa
Tulia Ackson katika harakati zake za kuusaka Ubunge wa Mbeya Mjini , baada ya kutumwa na Magufuli alibeba Majeneza na misalaba ya kila rangi kama Ishara ya kuizika Chadema , alitembea Mbeya yote bila kificho chochote , Mbona Kilaini na Gwajima walinyamaza ? wakati huyu Tulia akifanya yote haya alikuwa Naibu wa Spika wa Bunge la Tanzania (sasa hivi ni spika kamili) , ni mtu aliyekuwa anajitambua , mbona hawa wacha Mungu hawakuwahi kukemea ? Iweje leo mtu Msela kama Tundaman akifanya aliyoyafanya Tulia wao wanapambana naye , Kulikoni ?