Tulia Ackson atoa msimamo wa Bunge, asema Rais ni Mkuu wa Nchi na ana mambo yote!

Na huyu ndio huenda akawa Spika mtu mwenye mtizamo wa hivyo ?

Ndio hata kama asipokuwa na mambo yote hata ki-umri yeye na huyu inabidi apewe heshima..., ila kupewa heshima haimaanishi hakuna kuhojiwa
 
Bunge halina maana tena, inashangaza Naibu Spika anapotamka kuwa sio lazima serikali ichukue ushauri wa bunge, sasa nini maana ya uwepo wa bunge kama taasisi inayoisimamia serikali?

Huyu Tulia anadhani hii ni nchi ya kidikteta, kwa hii kauli yake nae anatakiwa kujiuzulu, anaonekana bado ana "mindset" ya kitumwa licha ya kuwa mwanasheria.

Zaidi hafai kuendelea kuwa NS kwa huu mtazamo wake, sasa kama ushauri/ kuhoji wanavyofanya kwa serikali sio lazima kuna haja gani ya kuwa na bunge?
 
CCM backbenchers tayari wanajutia hiyo katiba.
 
Hata usome vipi, ukiamua kuutumikia unafiki, unakuwa mwendawazimu. Uwendawazimu ukimpata msomi na ambaye hajasoma, huwa hakuna tofauti. Kama kutakuwa na utofauti, mwendawazimu ambaye hakusoma atatukana kwa Kiswahili, ambaye amesoma atatukana kwa Kiingereza.
 
Dola ni nini ?

Nani mkuu wa Dola ?

Jamani semeni mambo yote lakini acheni kukwepa UHALISIA kwasababu ya MIHEMKO.

Rais ndio mkuu wa kila kitu, kinacholeta tofauti ni kuheshimu taratibu tu.

Fanya ufanyavyo, tengeneza Katiba uwezavyo ila mwisho wa siku yule ambaye JESHI LINAMTII na anakaa na HAZINA akitakaa kuwasumbua, atawasumbua tu na hakuna kitu mtafanya.
 
Binafsi naamini iko wazi kuwa CCM ni Mwenyekiti (Rais) tu na huyu pekee ndo kila Kitu, aweza fanya lolote hata kama nila kipuuzi na akaungwa Mkono na kila mtu ndani ya CCM.

Jaji Mkuu na Spika wa Bunge kwa Nchi hii ni vyeo tu vyenye Nguvu na heshima ndani ya mihimili yao tu.
 
Usilete vitu vya kufikirika Kwa kuwa kasema, Mimi nimesema msomu kma yeye angeleta kitu kilichopo kwenye katiba yetu hiyo mbovu, SASA wewe tutajie Kifungu gani kinasema hicho alichokisema kma mwanasheria?
 
Usilete vitu vya kufikirika Kwa kuwa kasema, Mimi nimesema msomu kma yeye angeleta kitu kilichopo kwenye katiba yetu hiyo mbovu, SASA wewe tutajie Kifungu gani kinasema hicho alichokisema kma mwanasheria?
Sawa kamandaaaaa pipoooooooooooooooosssssssss
 
Hili sio taifa la kidikteta.
 
Rais yupo kwa sababu Kuna watu/wananchi hivyo asili ya mamlaka yake ni wananchi. Wananchi wanawasiliana na Rais kupitia wawakilishi wao ambao ni wabunge. Ukisema sababu ya ukuu wa Rais uamiri jeshi mkuu si sawa. Hakuwekwa Hapo na jeshi. Jeshi linalinda matakwa ya wananchi.
 
Ulishawahi kumuona mtu anayejilengesha abakwe tana anaandaa na mafuta kabisa??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…