Tulia Ackson atoa msimamo wa Bunge, asema Rais ni Mkuu wa Nchi na ana mambo yote!

Tulia Ackson atoa msimamo wa Bunge, asema Rais ni Mkuu wa Nchi na ana mambo yote!

Naibu Spika akiongea katika hafla ya kuwaapisha mawaziri, manaibu na viongozi wengine, amewapongeza wote walioteuliwa na kuwashauri wameteuliwa kufanya kazi za Rais nao wao wanamsaidia hivyo wazifanye kama wasaidizi wa Rais wa Jamhuri wa Muungano na si vinginevyo. Kuhusu Bunge, amesema kuna watu wanahisi kazi ya Bunge kila wakati ni kukosoa pekee. Amesema uko wakati Bunge linaishauri Serikali, kuna wakati linatunga sheria pia uko wakati Bunge linaisimamia Serikali.

Tulia amesema katika kipindi cha awamu ya sita imekuwa ikiwasikiliza ushauri wa wabunge na imekuwa ikizifanyia kazi.

Kwa muktadha huo, Tulia amesema Bunge liko tayari kushirikiana na awamu ya sita kwa mambo yote ambayo itayaleta bungeni ili wasimamie Serikali.

Naibu Spika amesema pale ambapo wanahitaji kukosoa Serikali wataikosoa kwa heshma na kwa muktadha ambao katiba inaruhusu kufanya hivyo, kwenye kushauri watashauri na si lazima Serikali kufata ushauri wa Bunge lakini katiba imetoa nafasi ya Bunge kuisimamia Serikali na kupata fursa ya kuiuliza Serikali walifanyia ushauri gani.

''Mihimili yote ina kazi zake na hapo mheshimiwa Rais nisisitize jambo moja maana kunakuwa na upotoshaji, Rais ni mkuu wa nchi, wapo watu wanachukua hiyo sehemu inayosema Rais ni kiongozi wa Serikali lakini Rais ana mambo yote, ni mkuu wa nchi, ni kiongozi wa Serikali, ni amiri Jeshi mkuu wa nchi hii.

Naamini kwa ufafanuzi huu watu watafahamu kwamba Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania, mheshimiwa Samia Suluhu Hassan sio tu kiongozi wa Serikali lakini ni mkuu wa nchi kwa hiyo yeye uongozi wake hauko sawasawa yeyote wa mhimili wowote ulioko hapa nchini"

Alisema Naibu spika, Tulia Ackson
Na huo ndio ukweli wenyewe.Tulia awe Spika anatosha kabisa.
 
Hotuba yake ilikuwa sehemu ya kuombea kura.

#KatibaMpya
 
Hata mimi nimemsikia. Kwa kifupi, huyu hata Ndugai atakuwa na nafuu!!

Kaongea alichongea ili kumfurahisha Mama ampe uspika, na akiupata, atakuwa ni bora Ndugai.

Wabunge kama mko makini, huyu msimpe uspika ingawa sioni uwezekano wa nyinyi kupinga chaguo la Raisi ni nani awe spika.

Kwa sasa Mama anaweka Spika wake(atakaeilinda serikali yake Bungeni) na baadae ataweka Waziri Mkuu wake.

Tukio la Ndugai kushinikizwa kujiuzulu ni ushahidi tosha wa hii katiba mbovu tulioanayo(Mungu ana makusudi kwa kila jambo).

Hata hivyo, nafurahi Ndugai kaonja machungu ya hii katiba mbovu, na ipo siku CCM kama chaka watakuja kujutia hii katiba.
Nani huwa anaweka spika wa wengine? Uliwahi sikia au kuona Nchi gani chama na Serikali inaweka Spika wa kuwapinga ?
 
Sawa alivosema lakini hii haifuti majukumu ya mihimili mingine. Hata ya kuiwajibisha seriaka.
Hekima, harmonidation kati ya mihimili yote ndo jambo muhimu na si kuwaambia raia kuwa muhimili mmoja umejichimbia zaidi
Ndio kwani yeye kafuta jukumu? Amesema watakosoa inavyotakiwa ila kwa staha,si unajua kuna kitu kinaitwa lugha ya kuudhi? Ndicho alifanya Ndugai tena nje ya Bunge.
 
Bunge halina maana tena, inashangaza Naibu Spika anapotamka kuwa sio lazima serikali ichukue ushauri wa bunge, sasa nini maana ya uwepo wa bunge kama taasisi inayoisimamia serikali?

Huyu Tulia anadhani hii ni nchi ya kidikteta, kwa hii kauli yake nae anatakiwa kujiuzulu, anaonekana bado ana "mindset" ya kitumwa licha ya kuwa mwanasheria.

Zaidi hafai kuendelea kuwa NS kwa huu mtazamo wake, sasa kama ushauri/ kuhoji wanavyofanya kwa serikali sio lazima kuna haja gani ya kuwa na bunge?
Kwani kaongea uongo? Kazi ya Bunge ni kushauri ila huilazimishi serikali kufuata ushauri tena kwa mujibu wa Katiba.
 
Rais yupo kwa sababu Kuna watu/wananchi hivyo asili ya mamlaka yake ni wananchi. Wananchi wanawasiliana na Rais kupitia wawakilishi wao ambao ni wabunge. Ukisema sababu ya ukuu wa Rais uamiri jeshi mkuu si sawa. Hakuwekwa Hapo na jeshi. Jeshi linalinda matakwa ya wananchi.
Wananchi wanaomfanya Rais ndio hao wanampa mamlaka ya kuwa mkuu wa vyombo vyote vya Dola kwa mujibu wa Katiba.

Na Katiba ipo kuweka uwiano na mahusiano baina ya mihimili.

Harafu nani aliwaambia kwamba Kazi ya mihimili ni kuleta mtafaruku au kufanya ligi za kukomoana na kuona nani zaidi?
 
Wapi katiba ilisema RAIS, SPIKA NA JAJI MKUU NI LEVEL MOJA??

ACHA KUJITOA UFAHAMU.
Kama tunataka nchi yetu iwe mahali bora kwetu sote fikra kwamba kuna muhimili mkubwa zaidi ni ujinga sana.
Yaani tumfanye mtu atembe akijigamba kuwa yeye ndo mwamba asiyetikiswa. Kama si kupalilia udikteta nini.
Ni lazima fike mahali muimili wowote ujue na uamini kwamba unaweza kutikiswa kama hauendi vizuri. Hiyo ndiyo afya ya taifa
 
Haya unayosema huwa yanafanyika katika nchi zenye demokrasia uchwara, mataifa yenye demokrasia imara kama US serikali imewahi kufungwa mara nyingi tu baada ya bunge kuikataa bajeti ya serikali, pia mkuu wa jeshi la Marekani amewahi kutangaza mbele ya vyombo vya habari kiapo chao ni kwa katiba ya nchi na sio mtu binafsi hivyo hawatatekeleza amri yoyote batili isiyofuata utaratibu wa sheria na kuingilia uhuru wa demokrasia.
Kutamka ni suala moja ila kwenye practical ni ishu tofauti,ndio maana Trump alikuwa anawatimua na hakuna sehemu alivunja Katiba licha ya kuapa kwao huko ulikosema lakini walikuwa wateule wa Rais.
 
Hawa wanamharibu huyu maza
Hakuna namna tutatoka kwenye hiyo tragedy bila kupata Katiba Mpya.

Katiba ya ccm inatumika kutuharibia taifa!

Kumbukeni kuwa ndani ya CCM SSH ni kila kitu kwao. Kwa hali ilivyo sasa wakitofautiana na mwenyekiti wa chama chao hakuna rangi wataacha kuona!
 
mwaka 2017 nakumbuka kwenye saga la makinikia kuna event ilifanyika ikulu , katka waongeaji mle alikuepo Ndugai jamaa akalopoka kuwa ile kamati iliyokuwa inawasilisha taarifa siku ile spika alimpigia simu rais ili ndo aiteue . 😀😀😀😀 yaani kamati ya bunge speaker anampigia rais ndo aiteue.
 
Bunge halina maana tena, inashangaza Naibu Spika anapotamka kuwa sio lazima serikali ichukue ushauri wa bunge, sasa nini maana ya uwepo wa bunge kama taasisi inayoisimamia serikali?

Huyu Tulia anadhani hii ni nchi ya kidikteta, kwa hii kauli yake nae anatakiwa kujiuzulu, anaonekana bado ana "mindset" ya kitumwa licha ya kuwa mwanasheria.

Zaidi hafai kuendelea kuwa NS kwa huu mtazamo wake, sasa kama ushauri/ kuhoji wanavyofanya kwa serikali sio lazima kuna haja gani ya kuwa na bunge?
Ni kademu ka nani kale kwani?
 
Anajisogeza karibu na kiti, ashajua mama yupo kama mtangulizi hataki uende tofauti hapo uhakika kamati kuu kupitisha jina lake
 
Kumbukeni Huyu mama ni mwanasheria kabisa, pale Leo anapokuja na kusema kuwa Rais wa Tanzania ndo Muhimili mkubwa wa mihimili yote iliyoopo, hiyo ipo kwenye ibara gani ya katiba yetu au ni kujipendekeza kumezidi? Hebu wanasheria twambieni kama kuna Kifungu kama hicho kwenye katiba yetu
Mie nimeelewa hivi;
Sisi watatu tunaishi nyumba moja.
House girl ni muhimili,
Mlinzi, ni muhimili pia,
Mtoto/Watoto ni muhimili. ila Mzazi/ Wazazi ndio MUHIMILI MKUU.
Hahuna cha spika wala mahakama. Rais ndie Muhimili wa mkubwa wa mihimili yote.
 
Back
Top Bottom