Tulia Ackson awataka viongozi wa magharibi kumheshimu. Ni baada ya kushambuliwa kuhusu kukutana na Vladmir Putin

Tulia Ackson awataka viongozi wa magharibi kumheshimu. Ni baada ya kushambuliwa kuhusu kukutana na Vladmir Putin

Umetoa pongezi za kipuuzi bwana; tukwambie ukweli tu. Yaani umsifie PhD holder tena kasoma Uingereza kwa kuongea Kingereza? Msifie kwa uwezo wa kujenga hoja, kujibu maswali kwa ufasaha na kutokua biased sio kuongea Kingereza. Wazungu huaga wanajiona wao NDIO binadamu na sister kaweza kuwamudu kwenye eneo hilo, kawauliza kuhusu Sudan, DRC, Gaza, Israel, Yemen etc. Yaani aliwasoma kwanza, I mean motive behind the question asked; kaenda nao ki ulalo ulalo. Hapo kaweza sana binti Mwaisa.
Ambacho sikielewi kwake na kwa wataalamu wengine ambao ni pro CCM; why wakiwaga nje ya nchi elimu zao zinaonekana lakini wakiwa Tanzania huwatofautishi na sisi wa elimu za hapa na pale?🤔😏


Mpuuzi labda ni wewe mwenyewe.

Tulia hajawahi kusoma Uingereza.

Maandishi kibao, akili kisoda.
 
Dr Tulia ameongea kwa busara sana na waliouliza maswali ni mazwazwa haswa , Mbunge mzima hajui kwamba president wa IPU haombi ruhusa kwa kokote tkutembelea wajumbe? pili mbunge mzima hajui kwamba president wa IPU alishatembelea Israel na Gaza kabla ? Ningekuwa mimi ningemtukana kidogo huyu beberu kuwa aende library tafute hata magazeti ya siasa halafu aje kuanza kuuliza maswali , Mwisho kawachana kidogo japo sikupenda alivyosema i came from such countries ? yaani Africa poor countries sisi ni matajiri sana tulioibiwa tu na kutokiongoza vizuri
Hakuna point aliyoongea huyo ajuza
 
Mpuuzi labda ni wewe mwenyewe.

Tulia hajawahi kusoma Uingereza.

Maandishi kibao, akili kisoda.
Sawa but huwezi kumsifia PhD holder tena wa sheria eti anaongea Kingereza kizuri; haiwezi kua sawa kwa vigezo vyovyote; tumsifie kwa ujengaji wa hoja alio onesha, ujasiri wake na consistency yake bila kuwaogopa hao wazungu. Lugha, hapana
 
watanzania acheni chuki zenu mbona kajieleza vizuri sana huyu dada yuko vizuri sana aisee
Hao wanomlaumu washazowe kupelekeshwa huwezi kuwafundisha namna ya Kujieleza hlf hao Mashabiki wa Simba na Yanga ndio walivo
 
Vipi hakuita polisi wawatoe wabunge hao nje?k
Katibu uchwara!! She is not diplomatic and lack necessary attributes to be a top global diplomat
Hivi walimchguaje? Wazungu nao sio
Kichwani yupo smart sema ana roho mbaya na sura sasa kayatimba
 
1729215529606.png
... PERFECT!
 
Vipi hakuita polisi wawatoe wabunge hao nje?k
Katibu uchwara!! She is not diplomatic and lack necessary attributes to be a top global diplomat

Kichwani yupo smart sema ana roho mbaya na sura sasa kayatimba
smartness yake unaipima na nini?
 
A
Hali imekuwa si Hali huko IPU wakati Rais wake Dk Tulia alipokutana na maswali magumu ikiwepo nani alimpa ruhusa ya kwenda Russia kabla ya kwenda Ukraine.

Maswali mengine ni Kwa nini hajaenda Gaza badala yake akaenda Israel?

Akijibu maswali hayo ameonesha kuwashangaa Wabunge wake vilaza Wazungu ambao hawajui dhima ya IPU na hawafuatilii ziara za Rais wao.


My Take
Kuwa tempared na Unaongea kizungu hakuleti ukakasi kama kwa Kiswahili .

Hongera Kwa majibu Mazuri na kuwapa makavu Wazungu.

Ushauri: Dk.Tulia ajifunze kuzuia hasira zake vinginevyo atakuja kutoa kubwa kuliko maana Wazungu lazima waweke fitina Kwa sababu za mambo Yao.🤣🤣🤣🤣👇👇

Akaheshimiwe Mwanjejwa kwao!
 
Aheshimiwe
Rais wa Muungano wa Mabunge Duniani (IPU), Tulia Ackson, amewataka wajumbe kumheshimu wakati wa mkutano wa Bunge uliofanyika Geneva siku ya Jumatatu Oktoba 14, 2024.

Mvutano ulianza baada ya Artur Gerasimov, mwakilishi wa Ukraine, kuomba "ripoti kamili ya mchakato" wa mkutano wake na kiongozi wa Urusi, Vladimir Putin, na aliuliza ikiwa maazimio ya IPU kuhusu "uchokozi wa Urusi" yalijadiliwa.

"Nataka sote tukumbuke kuwa hili lilitokea siku chache tu baada ya makombora ya Urusi kuharibu hospitali maarufu ya watoto huko Kiev," alisema Gerasimov, huku mwakilishi wa Canada pia akiunga mkono wito wa majibu.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, Gerasimov alijaribu mara kadhaa kumkatiza na kuchukua tena nafasi ya kuzungumza, kabla ya Tulia kumwambia: "Umeshazungumza, ulipata nafasi ya kuzungumza hapa. Nipe, niachie muda kwanza kulihutubia baraza kuu, nijibu masuala yaliyotolewa kisha turudi kwenye ajenda."

Ziara hiyo, aliendelea kusema, ilipaswa kuanza na Ukraine. "Ukraine ilijibu siku tuliyokuwa tayari kuwatembelea, [kwamba] Bw. Zelensky na Spika wangekuwa New York kwa ajili ya mkutano wa NATO. Ningewazuia? Hapana, isingekuwa busara, na kwa hali yoyote sina mamlaka hayo," Dkt. Tulia aliendelea kusema.

Pia Dkt. Tulia aliongeza kuwa hakuna atakayemzuia kuhudhuria Mkutano wa BRICS wiki ijayo huko Urusi.



Pia, soma:
Ana nini? Yeye anayo heshima? Aj8heshimu kwanza kabla ya kuheshimiwa.
 
Hali imekuwa si Hali huko IPU wakati Rais wake Dk Tulia alipokutana na maswali magumu ikiwepo nani alimpa ruhusa ya kwenda Russia kabla ya kwenda Ukraine.

Maswali mengine ni Kwa nini hajaenda Gaza badala yake akaenda Israel?

Akijibu maswali hayo ameonesha kuwashangaa Wabunge wake vilaza Wazungu ambao hawajui dhima ya IPU na hawafuatilii ziara za Rais wao.


My Take
Kuwa tempared na Unaongea kizungu hakuleti ukakasi kama kwa Kiswahili .

Hongera Kwa majibu Mazuri na kuwapa makavu Wazungu.

Ushauri: Dk.Tulia ajifunze kuzuia hasira zake vinginevyo atakuja kutoa kubwa kuliko maana Wazungu lazima waweke fitina Kwa sababu za mambo Yao.🤣🤣🤣🤣👇👇

Imenibidi nimsikilize Mh Tulia ili kutumia haki yangu ya kufikiri.Namuunga mkono!
Hata kama wazungu wanafiki watamtoa pale,ameipa nchi yangu heshima kubwa.
.
 
hongera kuiambia dunia ukweli, zelensky analeta comedy kwenye maisha ya wananchi wake, na huo ndio ukweli, Putin ni mtu humble na ni mnyenyekevu na anaheshimu kila mtu, pamoja na kuwa kwenye majukumu ya brics alitenga muda jalo kidogo kuongea na Tulia, alichokifanya zelensky Tulia kaiambia dunia ukweli na dunia imemuelewa
 
Wanawake watabaki kuwa wanawake sasa si angeongea taratibu na kujieleza vizur kuliko kuwafokea watu wazima??ata apa Tanzania kuna mmoja alishindwa kuvumilia akawatukana wazungu sasa sijuhi ataenda wapi kula pizza.??jamani kuelimika ni kukubali challenge na kuruhusu kukosolewa.tuache udikiteta wa kiafrika.huyu mama Mimi nampa 0% ametuaibisha saana.
 
Amejitahidi kuongea kiingereza vizuri

INgawa hiyo kupanic na kujisifia imeonyesha Kuna kitu hakiko sawa
Na wabunge wenzake wamemshutukia
Na hiyo ndio point wamechukua, wameshajua hawezi kujibu kwa staha
Watakuwa wanamcharua kila vikao ili ateme shombo
 
Back
Top Bottom