Tulia Ackson: CCM haitoachia Dola KAMWE

Tulia anachokisema ndio msimamo wa CCM na ukweli ni kwamba CCM Wana tamaa na madaraka na hawajawahi kufanya uchaguzi wa kweli iwe ndani ya chama chao na hata baada ya mfumo wa vyama vingi. Ndiyo maana hawaipendi na hawatakubali katiba Mpya inayoruhusu mfumo huru wa uchaguzi na katiba ya kumwajibisha Rais aliyeko madarakani.
Samia anazuga ila hebu tuelekee uchaguzi mtajionea rangi halisi ya CCM,wao na magufuli ni kitu komoja.
 
Huu unaweza kuwa ndio mwisho wao
 
Hizi ndizo fikra halisi za madktari wa falsafa waliojazana ndani ya chama tawala kwa njia za uani, ili kutafuta ulaji. Hawawezi kupambana kihoja majukwaani, zaidi ya kutegemea msaada wa dhuluma ya vyombo vya dola dhidi ya vyama upinzani.
 
Hizi ndizo fikra halisi za madktari wa falsafa waliojazana ndani ya chama tawala kwa njia za uani, ili kutafuta ulaji. Hawawezi kupambana kihoja majukwaani, zaidi ya kutegemea msaada wa dhuluma ya vyombo vya dola dhidi ya vyama upinzani.
Safari hii hatutawapa nafasi , Liwalo na Liwe !
 
Ndiomaana huwa siwaamini sana Wanasheria sijuhi kwanini?

Mwanasheria anaweza kumuhoji Polisi mahakamani kuwa WEWE UNASEMA ULIMKAMATA HUYU BWANA AKIWA NA GONGO, polisi-ndio

TUAMBIE ILIKUWA NA RANGI GANI.

polisi-nyeupe.

MWANASHERIA ANALETA MAZIWA..

TUAMBIE HII NI RANGI GANI?

polisi-nyeupe.

UKIONJA UNAHISI LADHA GANI?

polisi-maziwa

HAKIMU-Kesi imeisha Polisi kashindwa kesi.

Yaani ujinga ujinga tu. Ona na huyu ni mwanasheria, Mwalimu wa sharia, mtu mkubwa kabisa katika dola afu anaongea maneno kama Haya???

Wanamuharibia Mhe. Rais watu kama hawa! Sijuhi hawaelewi anapowaambia enzi za haya mambo zimeisha!!!!
 
Ila Tulia hajawahi kushinda kesi yoyote mahakamani , hata ya kuku
 
Mada kama hizi napenda kusoma tu,maana naweza kutoa mawazo yangu nikajikuta matatani!ila huyo mama ajue ipo siku hata kama miaka 1000000 ijayo ccm itaanguka tu.
 
Huyu mama ana hofu Sana na sugu. Anajua uchaguzi wa haki ataangushwa sasa anataka ufanyike uhuni kama wa 2020 ndio maana daima kauli zake ni hizo wasifuate demokrasia kwenye uchaguzi. Hana Amani kabisa na jimbo la mbeya mjini
Na ndiyo mwisho wake umefika. Ukishaona mchezaji anacheza rough uwanjani ujue kaishiwa maarifa.
 
Narudia kuwakumbusha kuwa Mungu amesikia kilio cha Watanzania na sasa mnachokishuhudia ni watawala kunyang'anywa ndimi zao na kizungumza yasiyotamkika yanayowafiti wenyewe.
Haina tofauti na Farao na jeshi lake walipoondolewa magurudumu yao kwenye bahari ya Shamu kabla hawagharikisha.


Kauli ya Tulia ndiyo picha inayoendelea serikalini. Kitu kinachoitwa MUAFAKA ni danganyatoto. Subirini mwaka ukipinduka ndo mtajua hamjui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…