Tulia Ackson: CCM haitoachia Dola KAMWE

Tulia Ackson: CCM haitoachia Dola KAMWE

Ex Spy

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2007
Posts
222
Reaction score
1,827
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa hakuna siku itatokea chama hicho kikaruhusu nafasi ya kuachia kuitawala nchi kwakuwa imejiwekea mizizi imara katika kuwatumikia wananchi wake.

Dkt. Tulia ameyasema hayo leo Februari 4, 2023 akiwa Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kichama ambapo alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya sherehe za miaka 46 ya Chama hicho iliyofanyika katika Mkoa wa kusini Unguja.

Amesema kuwa ni wakati sahihi kwa wanachama wa chama hicho hususani vijana kuendelea kukipigania na kuwapigania Viongozi wao wakuu akiwemo Mwenyekiti wa Chama taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuyasemea mazuri anayoyafanya kwa nchi.

“Mwana CCM hupaswi kukaa kinyonge hata siku moja, kote Tanzania bara na visiwani kuna miradi ya ujenzi wa shule kila kona, miundombinu ya barabara, zahanati, vituo vya afya n.k haya yote ni mafanikio ya kujivunia sasa unakaaje kinyonge? tunaposema kwamba chama hiki hakitaachia dola tunamaanisha” Amesisitiza Dkt. Tulia.

Chanzo: Clouds Media

CFD88AF9-BBAF-4989-84E2-50084E014349.jpeg
 
Ni kweli Kwa Katiba iliyopo na tume ya uchaguzi ya ajabu, CCM wataendelea kuwepo tu. A bitter truth ni kwamba kwa sasa Tanzania haina chama cha upinzani kilichopo kwaajili ya umma Bali kwa maslahi ya top Leaders Kama Mbowe, Zitto nk
 
CCM imejipanga sana ,inagusa kote kote na inamgusa kila mtu kiasi Cha kumfikia kila mtu. Nakipongeza sana Chama Cha Mapinduzi kwa usimamizi, utekelezaji ,uendashaji na ufanikishaji wa ahadi zake kwa Wananchi na kufanikiwa kutatua kero na changamoto mbalimbali na kujiweka karibu zaidi na Wananchi.

Na hapa ndio ninakubaliana na Spika Tulia kwamba CCM haitoacha dola kamwe kwa sababu inafanya mambo kwa matokeo na matarajio ya kuendelea kuwepo
 
Spika wa bunge ni mojawapo ya nafasi ambazo ni sensitive sana hapa nchini.

Leo hii huyu mama anadiliki kuyatamka haya maneno kweli hata bila kukumbuka kuwa aliapa kuwatumikia watanzania na kuilinda katiba.

Eti kamwe ccm haiwezi kuwachia madaraka!!!!

Kwanini hii serikali ilikubali kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa?

Tulia anatakiwa awaombe msamaha watanzania kwa kutoa maneno kama haya ya kibaguzi.
Screenshot_20230204-193848_Instagram.jpg
 
Kunawatu wanakula hovyo vya haramu wanavimbiwa wanasahau kuwa yupo Mungu naye ndiye anayeamua nini kiwe na nini kisiwe.

Tuwapuuze maana wamepita shule lakini akili hawana!!!
 
Spika wa bunge ni mojawapo ya nafasi ambazo ni sensitive sana hapa nchini...
Naunga mkono hoja.
Kuna watu tukiwaambia ukweli kuhusu CCM kutawala milele, hawaamini, na kwa vile maneno hayo ameyasema Tulia, bado kuna watu hawataamini hadi maneno hayo ya CCM kutawala milele Tanzania, yatakaposemwa na nanilii!. Sii wengi wanaojua kuwa kauli huumba, ila pia ukitoa kauli mbaya kama kuwatukana wazazi, kauli hiyo inasababisha one to be cursed!. Kauli kama hii ya CCM kutawala milele huko nyuma iliwahi kutolewa na kiongozi fulani who, very unfortunately, he was cursed!. Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!. humo nilisema "Wanabodi,

Kuna wengi wanadhani siasa ni kupiga blah blah tuu, hivyo kwao, kila kinachosemwa na wanasiasa, wanakiona kama ni blah blah!, no!. Siasa sio blah blah tuu, japo blah blah zipo, ila pia kuna ukweli bayana, dhahir, shahir!. Siasa ni sayansi, social science, hivyo sayansi ya siasa ni political science, inafuata kanuni zile zile za kisayansi za Newton's laws of motion, ile kanuni ya "a body in motion" or

" a static body", itaendelea kubaki hivyo hivyo milele, hadi kutokea nguvu nyingine itakayoibadilisha, hivyo kwa hali hii ilivyo sasa, CCM is the body in motion, itaendelea kutawala milele, kwa sababu watu wenye uwezo wa Kimungu, wameishaona kuwa kwa Tanzania, hakuna kabisa uwezekano wa kutokea nguvu nyingine ya kuizuia CCM isitawale milele nchi yetu ya Tanzania, hivyo CCM, itatawala milele!.

Japo kila lenye mwanzo, huwa lina mwisho, na CCM kama chama, ina mwanzo hivyo ni lazima nayo iwe na mwisho, unless CCM ndie Mungu mwenyewe, ambaye Yeye ndiye Pekee Alfa na Omega hivyo CCM hii iliyopo sasa nayo ni CCM Alfa na Omega, haina mwisho, hivyo pia katika utawala wa Tanzania, CCM ndio alfa na omega wa siasa zetu, ndicho chama pekee chenye hati miliki ya kuitawala Tanzania milele!, huu ni ukweli bayana ambao lazima sote, tuupokee, tuukubali na tuutekeleze. Wale wote wasioukubali ukweli huu, ni kweli kabisa watapata taabu sana!.

Jee Umilele wa CCM Kutawala Tanzania Milele, Unatokana na Nini?.

Umilele wa CCM kuitawala Tanzania, unatokana na mungu wa CCM (not Mungu Baba) kuiteua CCM na kuipatia hati miliki ya kuitawala Tanzania milele na milele, ndio maana katika baadhi ya makala zangu za nyuma, niliwahi kushauri tuifute ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, tuifute ruzuku kwa vyama vya siasa, Tanzania turejee kuwa nchi ya chama kimoja cha milele, CCM.

Ruzuku kwa vyama vya Siasa: Mnaonaje tumshauri Rais Magufuli aifutilie mbali ruzuku hii? Ni ufisadi
NB: Baadhi ya kauli kama hizi, zinasababisha curses, msije kushangaa watoa kauli kama hizi kuja kuwa cursed na kuchomoka kabla ya wakati kwa sababu neno milele ni mamlaka ya Mungu mwenyewe!.

Kidumu Milele Chama Cha Mapinduzi.
Pasco"

P
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa hakuna siku itatokea chama hicho kikaruhusu nafasi ya kuachia kuitawala nchi kwakuwa imejiwekea mizizi imara katika kuwatumikia wananchi wake...
Sababu ya kutoachia dola, ubora,umakini,weledi,magoli ya mkono,katiba,mazuio ya shughuli za kisiasa,matumizi yasiyo na usawa wa vyombo vya dola au,usawa katika masanduku ya kura au,sheria za mwekokasi kuhakikisha ushindi wenu.Tinahitaji majibu tasafali🤔
 
CCM imejipanga sana ,inagusa kote kote na inamgusa kila mtu kiasi Cha kumfikia kila mtu. Nakipongeza sana Chama Cha Mapinduzi kwa usimamizi, utekelezaji...
Sio kweli usemacho ccm imeshachokwa siku nyingi wanachofanya sasa ni kupora madaraka kwa nguvu tu wakijua wananchi hawatofanya chochote kwa sababu kupitia majeshi yao wapo tayari kufanya lolote ili mradi waendelee kubaki madarakani.
 
Spika ni mwanachama wa Chaka cha siasa na alikuwa ktk maadhimisho ya Chaka chake cha siasa

Ameeleza mengi ambayo wanaccm wana takiwa kujivunia na kutembea kifua mbele

Pia kama alivyo wahi kutamka Dr Bashiru, naunga mkono hoja ya Dr Tulia

Ccm haito hachia dola kamwe
 
Back
Top Bottom