Tulia Ackson: Wanaoamini nguvu ya dola ilitumika uchaguzi 2020 ni imani tu, hamna mtu ameona mahali. Auliza mbona hawakwenda mahakamani!

Tulia Ackson: Wanaoamini nguvu ya dola ilitumika uchaguzi 2020 ni imani tu, hamna mtu ameona mahali. Auliza mbona hawakwenda mahakamani!

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Spika Tulia amesema wanaoamini nguvu ya dola ilitumika 2020 kuwaingiza wabunge wa CCM bungeni ni imani tu na hakuna mtu ameona mahali. Amesema nchi hii ina utaratibu wa kwenda mahakamani kuonesha imani yako inaposimamia na maeneo mengi watu wanafunguliwa kesi za ubunge na wapo walioondolewa huko nyuma.

Amesema kuhusu yeye na jimbo la Mbeya, amewataka waandishi waende Mbeya waone mpango wa wananchi wa Mbeya mjini.

 
Waende mahakama zipi, hizi hizi zinazoendesha kesi ya Covid 19 mwaka wa pili huu? Kenya hapo kulikuwa na kesi ya uchaguzi nafasi ya urais imeisha ndani ya muda mfupi, iweje hii ya Covid 19 ichukue zaidi ya mwaka?!
 
Hata yeye mwenyewe Tulia Ackson anajuwa kuwa alitoa Tsh 100,000 kwa wajumbe wote 800 wa Mkutano wa Jimbo la Mbeya Mjini ambao ndiyo waliompitisha kugombea kwa Tiketi ya CCM.

Pamoja na kuwekewa kinga na hawara yake Magufuli bado alitumia kama Tsh 100 Milioni kupita kura za maoni za CCM


Kuhusu kwenda Mahakamani jibu ni kwamba kipindi cha Magufuli ilikuwa ni vigumu kwa vile Majaji na Mahakimu kwa kesi kama hiyo ingekuwa ni vigumu kushinda. Mahakama zilikuwa zinatishiwa na kufuata maelekezo ya mwendazake
 
Huu ushahidi unaupeleka lini mahakamani? Mnajua mlimnenea mangapi Makonda na sasa hamna ushahidi hata mmoja?
 
Kwanini hawakuenda mahakamani baada ya Magufuli kufariki
 
Kwanini hawakuenda mahakamani baada ya Magufuli kufariki

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
Huna ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu hapa jukwaani, kesi za malalamiko ya uchaguzi ni ndani ya miezi sita tu baada ya uchaguzi. Tuache hayo, kwa sasa kuna kesi ya Covid 19, ni kipi kinafanya hiyo kesi ichukue muda mrefu hivyo kama ushahidi wote upo? Kwa mpinzani kwenda kwenye mahakama hizi ni kupoteza muda.
 
Chadema ni wajinga sana
Ujinga kuliko huu??
IMG_20220928_174944.jpg
View attachment 2609361
 
Back
Top Bottom