Tulia Ackson: Wanaoamini nguvu ya dola ilitumika uchaguzi 2020 ni imani tu, hamna mtu ameona mahali. Auliza mbona hawakwenda mahakamani!

Tulia Ackson: Wanaoamini nguvu ya dola ilitumika uchaguzi 2020 ni imani tu, hamna mtu ameona mahali. Auliza mbona hawakwenda mahakamani!

Waende mahakama zipi, hizi hizi zinazoendesha kesi ya Covid 19 mwaka wa pili huu? Kenya hapo kulikuwa na kesi ya uchaguzi nafasi ya urais imeisha ndani ya muda mfupi, iweje hii ya Covid 19 ichukue zaidi ya mwaka?!
Hizohizo mkishinda zinatenda haki,mkishindwa hazifai, hopeless kabisa wewe
 
Wakati wa Mwendakuzimu nani angepewa haki kinyume na atakacho Magu?Rejea kesi ya Sugu na Lema kukaa rumande kwa miezi kadhaa.
Nchi ilikuwa na majaji wa michongo
 
HEKIMA za CCM)( Mambooz)
af644d714ea23a1a5e5dc7c7a0237b08.jpg
 
Spika Tulia amesema wanaoamini nguvu ya dola ilitumika 2020 kuwaingiza wabunge wa CCM bungeni ni imani tu na hakuna mtu ameona mahali. Amesema nchi hii ina utaratibu wa kwenda mahakamani kuonesha imani yako inaposimamia na maeneo mengi watu wanafunguliwa kesi za ubunge na wapo walioondolewa huko nyuma.

Amesema kuhusu yeye na jimbo la Mbeya, amewataka waandishi waende Mbeya waone mpango wa wananchi wa Mbeya mjini.

Chadema na chawa wao wanamdanganya Sugu 😂😂
 
Hata yeye mwenyewe Tulia Ackson anajuwa kuwa alitoa Tsh 100,000 kwa wajumbe wote 800 wa Mkutano wa Jimbo la Mbeya Mjini ambao ndiyo waliompitisha kugombea kwa Tiketi ya CCM.

Pamoja na kuwekewa kinda na hawara yake Magufuli bado alitumia kama Tsh 100 Milioni kupita kura za maoni za CCM


Kuhusu kwenda Mahakamani jibu ni kwamba kipindi cha Magufuli ilikuwa ni vigumu kwa vile Majaji na Mahakimu kwa kesi kama hiyo ingekuwa ni vigumu kushinda. Mahakama zilikuwa zinatishiwa na kufuata maelekezo ya mwendazake
siipend ccm ila sipendi udaku , una ushaid wa mahusiano kati ya jpm na Tulia? tukosoe vitu bila mihemko ni kwel mbeya waliiba kura ila tusifike hatua ya kuongeza chumv nying kweny taarifa
 
Sio enzi za Magufuli tu, hata sasa bado mahakama zinafuata amri za nje ya sheria. Rejea kesi ya Covid 19 na danadana zinazoendelea.
Acheni uhuni tatizo lenu CHADEMA mnapenda mshinde kesi nyie ndiyo ionekane haki imetendeka.
Suala la Uchaguzi mlipaswa muende Mahakamani kwa mujibu wa sheria mkaseme sheria fulani na fulani ilikiukwa Ili kumpa Ubunge Bwana fulani lakini bila kwenda Mahakamani hizo zinabaki kuwa taarabu ma majungu ya mtaani.
 
Huna ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu hapa jukwaani, kesi za malalamiko ya uchaguzi ni ndani ya miezi sita tu baada ya uchaguzi. Tuache hayo, kwa sasa kuna kesi ya Covid 19, ni kipi kinafanya hiyo kesi ichukue muda mrefu hivyo kama ushahidi wote upo? Kwa mpinzani kwenda kwenye mahakama hizi ni kupoteza muda.
Mulienda Mahakamani ndani ya iyo miezi sita?
 
Nakumbuka kulikuwa na maneno makuu matatu tu kutoka kwa jemedari;
1. Nipeni huyu mtu sitawaangusha akiwazingua ninammudu.
2. Nipeni koneksheni.
3. Msichanganye betri na gunzi tochi haitawaka.

Mchezo uliishia hapo.
Na yule demu aliyeshinda Ubunge Nkasi alipitaje?au Jiwe alikuwa ametoka madarakani kipindi hicho!!
 
Mahakama zipi?

Maana majaji wa mahakama zote wanateuliwa na mwenyekiti wa CCM
Kesi za Uchaguzi walizoshinda Lissu na Lema ziliamuliwa na Mahakama ya Burundi?Acheni utoto!
 
Acheni uhuni tatizo lenu CHADEMA mnapenda mshinde kesi nyie ndiyo ionekane haki imetendeka.
Suala la Uchaguzi mlipaswa muende Mahakamani kwa mujibu wa sheria mkaseme sheria fulani na fulani ilikiukwa Ili kumpa Ubunge Bwana fulani lakini bila kwenda Mahakamani hizo zinabaki kuwa taarabu ma majungu ya mtaani.
Wewe acha upumbavu, ulitaka waende kwenye mahakama gani hizo wakati unafahamu fika kwamba hizi Kangaroo Courts ni mali za ccm.

Mtu unaongea utafikiri unaishi Denmark au Sweden wakati uko tu hapo Vingunguti. Bure kabisa.
 
Kenya kesi zimeisha ndani ya muda mfupi na matokeo yake sasa hivi hadi Rais Mstaafu anashiriki vurugu mtaani kupinga hukumu ya kuhalalisha ushindi wa Ruto

Kuandamana na uwezo wa mahakama kutenda kwa wakati ni mambo mawili tofauti. Kwa umri wako ulipaswa kujua tofauti hiyo.
 
Hizohizo mkishinda zinatenda haki,mkishindwa hazifai, hopeless kabisa wewe

Umewahi kuona mtu akisifia mahakama ikitenda haki zaidi ya kushangaa imewezaje? Kwa taarifa Yako mahakama inapaswa kutenda haki na sio kubalance hisia za kiitikadi.

Baada ya uchaguzi wa 2020 ulioharibiwa na Magufuli kwa kiburi chake cha madaraka, Wafuasi wengi wa upinzani walifungwa na hizi mahakama kwa kubambikiwa kesi, hivi sasa wanaachiwa wengi, huku mahakama ikikiri kuwa walifungwa bila ushahidi kutosheleza/kimakosa! Hizo ndio Mahakama unazozitetea.
 
Back
Top Bottom