Tulia Ackson: Wanaoamini nguvu ya dola ilitumika uchaguzi 2020 ni imani tu, hamna mtu ameona mahali. Auliza mbona hawakwenda mahakamani!

Tulia Ackson: Wanaoamini nguvu ya dola ilitumika uchaguzi 2020 ni imani tu, hamna mtu ameona mahali. Auliza mbona hawakwenda mahakamani!

Kamelewa madaraka kiasi cha kufikiri Watanzania ni wajinga, na wasiofahamu mwenendo mzima wa huo uchaguzi wao wa magumashi.
 
Acheni uhuni tatizo lenu CHADEMA mnapenda mshinde kesi nyie ndiyo ionekane haki imetendeka.
Suala la Uchaguzi mlipaswa muende Mahakamani kwa mujibu wa sheria mkaseme sheria fulani na fulani ilikiukwa Ili kumpa Ubunge Bwana fulani lakini bila kwenda Mahakamani hizo zinabaki kuwa taarabu ma majungu ya mtaani.
Unakwenda kwenye mahakama ambazo tayari zilikuwa zinaagizwa na Magufuli aina ya hukumu za kutoa dhidi ya wapinzani?

Hii michezo ya viongozi hawa wenye mitazamo ya kijamaa ya kuchezea mahakama, ndio husababisha wawekezaji kutumia mahakama za nje, na matokeo yake mara zote serekali husindwa vibaya maana huko hawawezi kuziagiza mahakama hizo aina ya hukumu za kutoa.
 
Mulienda Mahakamani ndani ya iyo miezi sita?
Hakuna mahakama hapa Tanzania za kuwapa haki wapinzani kwa uhuni wanaofanyiwa na viongozi wa serikali. Huwa nawaelewa sana wazungu kwa kutumia mahakama za kimataifa, maana upuuzi wa mahakama zetu wanaufahamu vizuri.
 
Huna ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu hapa jukwaani, kesi za malalamiko ya uchaguzi ni ndani ya miezi sita tu baada ya uchaguzi. Tuache hayo, kwa sasa kuna kesi ya Covid 19, ni kipi kinafanya hiyo kesi ichukue muda mrefu hivyo kama ushahidi wote upo? Kwa mpinzani kwenda kwenye mahakama hizi ni kupoteza muda.
Mara ngapi wanaoshindwa uchaguzi wanakwenda mahakamani na wanashinda kesi?.

Tuwe na shukrani sio kulalamika kwa kila jambo. Hio kesi ya hao covid inao msingi tofauti na nyingine nyingi za kisiasa.
 
Umewahi kuona mtu akisifia mahakama ikitenda haki zaidi ya kushangaa imewezaje? Kwa taarifa Yako mahakama inapaswa kutenda haki na sio kubalance hisia za kiitikad...
Huo ni upande mmoja tu wa utendaji wa mahakama, kumbuka ni mara ngapi hizi hizi mahakama ziliwapa ushindi wabunge wa upinzani baada ya kuwa wameshindwa huko majimboni.
 
Mara ngapi wanaoshindwa uchaguzi wanakwenda mahakamani na wanashinda kesi?.

Tuwe na shukrani sio kulalamika kwa kila jambo. Hio kesi ya hao covid inao msingi tofauti na nyingine nyingi za kisiasa.

Mara kibao huwa tunaona mizengwe mikubwa huko mahakamani, hadi kuwe na shinikizo la nje ndio haki kutendeka. Na hata hizo mahakama zilizojaribu kwa mbali kuwapa haki wapinzani ilikuwa wakati wa JK na sio chini ya utawala wa kidhalimu wa Magufuli.

Msingi upi wa hiyo kesi ya Covid 19 hadi ichukue zaidi ya mwaka mmoja? Ni ushahidi gani unakosekana hadi kesi ichukue muda mrefu hivi? Acha kutetea mambo ya aibu.
 
Mara ngapi wanaoshindwa uchaguzi wanakwenda mahakamani na wanashinda kesi?.

Tuwe na shukrani sio kulalamika kwa kila jambo. Hio kesi ya hao covid inao msingi tofauti na nyingine nyingi za kisiasa.

Kutetea udhaifu ni jambo gumu sana. Kwahiyo kesi ya hao covid ni kubwa kuliko ya uchaguzi wa urais wa Kenya ambayo ilishafanyika na hukumu imetoka?
 
Hata yeye mwenyewe Tulia Ackson anajuwa kuwa alitoa Tsh 100,000 kwa wajumbe wote 800 wa Mkutano wa Jimbo la Mbeya Mjini ambao ndiyo waliompitisha kugombea kwa Tiketi ya CCM...
Wangeenda mahakama ipi ikiwa Watendaji wa vijiji na vitongoji pamoja na wakurugenzi wa halmashauri waliambiwa mmeajiriwa na Ccm ole wenu ccm isishinde?

Nilikuwa Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Masasi 2020 bado kidogo wanichinje
 
Kutetea udhaifu ni jambo gumu sana. Kwahiyo kesi ya hao covid ni kubwa kuliko ya uchaguzi wa urais wa Kenya ambayo ilishafanyika na hukumu imetoka?
Mazingira mazima ya kesi ni tofauti. Moja inahusisha sheria za bunge na nyingine ni ya moja kwa moja chini ya mahakama za Kenya.
 
Huo ni upande mmoja tu wa utendaji wa mahakama, kumbuka ni mara ngapi hizi hizi mahakama ziliwapa ushindi wabunge wa upinzani baada ya kuwa wameshindwa huko majimboni.
Nitajie hata wabunge watano wa upinzani waliowahi kutangazwa kushindwa kwenye uchaguzi, kisha wakaenda wakapata huo ubunge kupitia mahakama.
 
Mara kibao huwa tunaona mizengwe mikubwa huko mahakamani, hadi kuwe na shinikizo la nje ndio haki kutendeka. Na hata hizo mahakama zilizojaribu kwa mbali kuwapa haki wapinzani ilikuwa wakati wa JK na sio chini ya utawala wa kidhalimu wa Magufuli.

Msingi upi wa hiyo kesi ya Covid 19 hadi ichukue zaidi ya mwaka mmoja? Ni ushahidi gani unakosekana hadi kesi ichukue muda mrefu hivi? Acha kutetea mambo ya aibu.
Sio mambo ya aibu, ni taratibu tumejiwekea wenyewe.
 
Nitajie hata wabunge watano wa upinzani waliowahi kutangazwa kushindwa kwenye uchaguzi, kisha wakaenda wakapata huo ubunge kupitia mahakama.
Siwakumbuki ingawa najua wapo, mmoja kama sijakosea ni jimbo mojawapo la Mkoa wa Mara.
 
Mazingira mazima ya kesi ni tofauti. Moja inahusisha sheria za bunge na nyingine ni ya moja kwa moja chini ya mahakama za Kenya.

Kwahiyo hii kesi ya hapa inafanyikia bungeni na sio mahakamani?! Boss ndio umetoka kushiba Mida hii nini? Sijui hata unatetea nini. Kwahiyo hii ya hapa ina mazingira mazito sana kwa sababu ni ya wabunge, ila huko Kenya kwenye kwenye urais wa nchi nzima ni rahisi!
 
Spika Tulia amesema wanaoamini nguvu ya dola ilitumika 2020 kuwaingiza wabunge wa CCM bungeni ni imani tu na hakuna mtu ameona mahali. Amesema...
Sasa nimeamini Tulia huenda atakuwa mjinga wa kwanza mwenye PhD.

Anazungumzia watu kwenda mahakamani, hivi wakati wa awamu ya5 kulikuwa na mahakama?

Hivi wakati Rais Magufuli anasema japo kuna mihimili mitatu lakini wa kwake ndio uliojichimbia chini, Tulia alikuwa amelala usingizi? Wakati Magufuli anawateua maafisa wa TISS kuwa majaji ili aweze kuitumia mahakama kama idara ya Rais, Tulia alikuwa hospitalini Milembe?

Wapo wachache walikengeuka wakati wa awamu ya 5 lakini wameanza kujirudi, lakini Tulia amebakia kama alivyokuwa.

Ngoja ichaguzi wa haki, uwazi na uhuru ufanyike Mbeya, na jimbo lisigawanywe, tuone kama Tulia atafikisha hata 30%.
 
Back
Top Bottom