Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 7,021
- 11,475
1. Siyo mzawa wa Mbeya kwa kuwa anatokea Rungwe. Hata ukisema Tanzania hakuna ukabila lakini Wasafwa ambao ndiyo wengi hawawezi kumpa kura Tulia Mnyakyusa, bora wampe Mpangwa Sugu.
2. Mfumo dume. Hata kwao Rungwe wasingempa mwanamke kutokana na mila zao.
3. Taswira ya Tulia kama Naibu Spika. Ametumika sana kuwakandamiza wapinzani kwa kuwanyima nafasi ya kuongea, kuwafukuza kwenye vikao na kupuuza hoja zao
4. Kura 100,000 za Sugu za mwaka 2015. Hawa watu waliomfanya Sugu awe the most voted MP bado wapo na Sugu hajawakwaza.
Sioni namna Tulia atapata kura za Mbeya Mjini.